Wakazi wa Dar Es Salaam wanakwamisha Mageuzi Tanzania. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wakazi wa Dar Es Salaam wanakwamisha Mageuzi Tanzania.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by JACADUOGO2., Apr 29, 2012.

 1. J

  JACADUOGO2. JF-Expert Member

  #1
  Apr 29, 2012
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 930
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Ni ukweli usiopingika kuwa wakazi wa jiji la Dar Es Salaam ndo wanaokwamisha mageuzi ya kweli hapa Tanzania kwani Dar kila mtu anajifanya yuko bize na mambo yake eti wanatafuta hela! Kwani mikoani watu hawajui kutafuta hela?

  Wakazi wa Dar wanapenda kufuatilia sana mambo ya UDAKU kama mambo ya Kanumba, Lulu, Wema, Diamond, Johari, Jokate. UBITOZI NA USHAROBARO kwa kwenda mbele.

  Mara nyingi mageuzi yanaanzia kwenye majiji makubwa kama Dar, wakazi wa Dar badilikeni.....!!!!
   
 2. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #2
  Apr 29, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Lema anatinga huko kuwaamsha waliolala
   
 3. k

  kula kwa tindo JF-Expert Member

  #3
  Apr 29, 2012
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 1,330
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Vijiwe (hasa vya Bao na Kahawa) vilivyo pandikizwa na MAGAMBA ndivyo chanzo cha watu kutokuwa ma mzuka huo.. wengi wapo Humu JF mabingwa wa kulalama lakini ikitokea tuingie front ,utasikia NIKO BIZE BANA.......
   
 4. munisijo

  munisijo JF-Expert Member

  #4
  Apr 29, 2012
  Joined: Apr 10, 2012
  Messages: 868
  Likes Received: 172
  Trophy Points: 60
  Mmmh, mi nita jamani though, kuna ukwel katika yote mnayosema! Dah
   
 5. Highlander

  Highlander JF-Expert Member

  #5
  Apr 29, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 3,094
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Umekosea sana ndugu. vyama vingi vya siasa chimbuko lake Dar es Salaam. Dar ndiyo chimbulo la mageuzi Tanzania. Mkutano wa kwanza wa mageuzi ulifanyika Motel Agip Dar es Salaam, siyo Arusha. Mtei, Mareale, Makani na timu yake walianzisha chadema Kisutu Dar es Salaam.

  Magazeti kama Shaba, Watu, Family Mirror, Majira ndiyo vyombo vya habari vya mwanzo kutoa elimu ya uraia kuhamasisha watu kufikiri kimageuzigeuzi ndipo wewe ukapata elimu inayokupa werevu katika siasa.

  Hawa watu wote wanakaa Dar es Salaam. Dar es Salaam ndiyo msingi wa mageuzi Tanzania. Kwa sasa ni kama baba ambaye kajichokea kwa mahangaiko ya muda mrefu na umri kwenda sana, wanae wameshakuwa wakubwa ndio wanahangaika sasa huko pembezoni kumsaidia baba.

  Nina hakika baba huyu akiitazama Arusha leo, na Mwanza, na Mbeya, Tandahimba, na Songea, Iringa mjini nasikia eti hata Dodoma? moyo wake unapata faraja! Ipe Dar es Salaam sifa inayostahili.

  Ni kweli vijana wana nguvu sana sasa. Lakini halikuanza jana Arusha, mkuu!
   
 6. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #6
  Apr 29, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,671
  Trophy Points: 280
  Haa haaa haaaa! Dar es Salaam watu hawana akili za kushikiwa mwambie aje halafu aitishe mkutano ndio atajua labda aende Kimara..
   
 7. M

  Makupa JF-Expert Member

  #7
  Apr 29, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,742
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Mkuu wakazi wa dar wameathiriwa sana na nyoto kiasi kwamba hata uwezo wa kufikiri unakuwa mdogo
   
 8. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #8
  Apr 29, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,671
  Trophy Points: 280
  Nadhani umri wako ni mdogo siwezi kukulaumu hivi unajua kuwa Dar ndio kila kitu ndio chimbuko la siasa za mageuzi Tanzania wewe unadhani siasa zimeanza baada ya Lema kushinda Arusha...fuatilia mdogo wangu historia ya Dar es Salaam.
   
 9. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #9
  Apr 29, 2012
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  siamini kihivyo kwa sababu;
  • Dar ilitoa wabunge watatu ie MNYIKA,(kijana) MDEE(kijana Mwanamke) na MPENDAZOE (awali alikuwa Kishapu via CCM - Ingawa alichakachuliwa)
  • M4C haijapita Dar hata tuka evaluate mwitikio wao
  • etc
   
 10. p

  popobaawa Member

  #10
  Apr 29, 2012
  Joined: Mar 19, 2007
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Wakazi wa Dar wanaelewa vizuri kuwa wanasiasa ni sawa na wafanyabiashara tu, wote wanatafuta pesa, umaarufu na sifa. Tofauti ni kuwa mfanyabiashara anauza bidhaa na huduma, mwanasiasa anauza maneno, ahadi na uongo.

  Tumekataa kuwa wateja wa wanasiasa. Tofauti ya CCM, Chadema, CUF, TLP, UDP n.k ni sawa na tofauti ya biashara ya mafuta, vifaa vya ujenzi, duka la mapambo, saloon n.k Chapa kazi, hakuna mwanasiasa atakaekuletea maendeleo kwa hapa kwetu. Ndio ajira zao hao
   
 11. The Listener

  The Listener JF-Expert Member

  #11
  Apr 29, 2012
  Joined: Feb 5, 2012
  Messages: 977
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  mageuzi ya kweli hutoka moyoni mkuu na wala si suala la kuiga. Dar es salaam ina watu toka sehemu tofauti nchini na matatizo yao yaonekana kutowaingia mioyoni mwao kama sehemu nyingine zenye watu wenye uchungu na maeneo yao kama vile arusha/arumeru na matatizo ya ardhi/maji kanda ya ziwa na uamko halisi wa kutaka maendeleo yaliyo sawa na kanda zilizoendelea zaidi yake nk.
   
 12. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #12
  Apr 29, 2012
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  leo umefunguka big up
   
 13. Graph Theory

  Graph Theory JF-Expert Member

  #13
  Apr 29, 2012
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 3,803
  Likes Received: 1,112
  Trophy Points: 280
  Safi sana Dar muendelee hivyo hivyo kupinga hao wavunja amani wa nchi, endeleeni kuchagua chama makini(CCM).
  .
  "WASIOSOMA NI CHAKULA CHA WASOMI".
   
 14. KASHOROBANA

  KASHOROBANA JF-Expert Member

  #14
  Apr 29, 2012
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 3,249
  Likes Received: 406
  Trophy Points: 180
  Natumai pia naamini hauko sahihi, mwamko wa mageuzi ni mkubwa sana dar, mfano kiduchu ni ofisini kwangu tuko kama 300 ivi ccm ni km 2% ya wote tatizo naloliona dar hatulindi kura zetu.

  Majuzi umefanyika uchaguzi wa udiwani vijibweni hatukulinda kura zetu ccm wakaweza kuzichakachua (pia watu toka temeke walikuja na kuipiga kura ccm) ivo mgombea wetu wa chadema akashindwa lkn ukweli ndo alokuwa ameongoza ata ccm wanalijua ilo na kulikubali kwani kampeni zao ccm zilidolola sana yani hawakuungwa mkono kabisa.

  Ata wakati wa ubunge mama komu wa cdm alishindwa kwa margin ndogo wakati vituo vingi tu hakukuwa na mawakala wa cdm hii ni wazi kama kawaida yao ccm walifanya kweli.

  Hayo ni machache tu.

  My take: Viongozi wa chadema dar waache tabia za kuonekana wakati wa kampeni tu, wajipange wazunguke kila kona hasa mda huu wa m4c waamasishe kuwa wanachama hai pia jinsi ya kuzilinda kura zao nakuhakikishia mabadiliko makubwa na ya ajabu yatatokea dar asa
   
 15. Chaimaharage

  Chaimaharage JF-Expert Member

  #15
  Apr 29, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 211
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  You're absolutely right. Dar people are obsessed with nonsense issues like the likes of Kanumba and many more. They keep busy in the name of searching for money and yet they're poor.

  They don't sit down and dig deep to know the sourse of their poverty. Up country people have known that and now they are eager for change. Once freedom comes then I think the capital city must be shifted to any of the serious region from these LAZY Dar dwellers.
   
 16. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #16
  Apr 29, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,788
  Likes Received: 3,877
  Trophy Points: 280
  Kuanzisha vita si issue ! issue ni kupigana vita hadi ushinde! Dar mageuzi yameanzia huko fine mbona hamkuyaendeleza??mmekaa tu kimya mambo ya hovyo hovyo yanafanyika hajuwahi kusikia hata mkitishia kwenda ikulu ambayo mpo nayo huko! wanaharakati juzi wakati wa mgomo wa madaktari waliandamana hamuwaunga mkono! amkeni acheni kulala!!
   
 17. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #17
  Apr 29, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,788
  Likes Received: 3,877
  Trophy Points: 280
  wewe ni debe tupu hujui siasa afadhali ujiunge na vikundi vya taarabu!!
   
 18. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #18
  Apr 29, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,046
  Likes Received: 13,260
  Trophy Points: 280
  Dar Jimbo ambalo bado litaendelea kusumbuwa mabadiliko ni jimbo la Ilala lililojaa Wahindi na Waswahili kama Faiza Foxy na jimbo la Kinondoni lililojaa makahaba, mafuska, mateja, wezi, Matapeli, Wasanii na kila aina ya machukizo machoni pa Mungu.

  Jimbo la Kinondoni wengi wao hawaoni hata umuhimu wa kuwepo Serikali na ingewezekana kwa amri yao basi Rais wa Ngwasuma ndiyo huyo huyo angekuwa Rais wa Nchi.

  Majimbo yaliyobaki kama Kawe na Ubungo hapa somo linaeleweka vyema, Temeke na Kigamboni, wakazi wake wengi ni wandengereko na wamatumbi, Uislamu na uswahili ni sehemu ya advatage ya kushinda jimbo hili.

  Ukonga na Segerea ni majimbo ambayo yapo kibla ni Chadema tu inayopaswa kujenga mtandao imara ili kuyachukuwa majimbo haya mawili, hakuna tatizo lolote kwenye haya majimbo.
   
 19. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #19
  Apr 29, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,788
  Likes Received: 3,877
  Trophy Points: 280
  You are absolutely right!
   
 20. KASHOROBANA

  KASHOROBANA JF-Expert Member

  #20
  Apr 29, 2012
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 3,249
  Likes Received: 406
  Trophy Points: 180
  UKO SAHIHI SANA Duble Chris, HUO NDO UKWELI
   
Loading...