Wakazi wa Dar es Salaam wahaha shida ya maji na umeme

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
13,495
51,089
Kufeli kwa serikali ya CCM sasa kumegonga pentagoni. Jiji la Dar es laam sasa limegeuka jiji la uhaba wa maji na umeme.

Kwenye ishu ya maji, kuna mgao wa siku tatutatu na maji yanatoka masaa machache kisha yanakatika.

Hali hiyo imefanya watu waanze kuhangaika na ndoo na madumu kutafuta maji

Tumerudi enzi zile za Mzee Mwinyi, jiji lilikuwa na uhaba wa maji wa kufa mtu

Wakati hayo yakiendelea, umeme nao umekuwa bidhaa adimu.

Waziri wa Nishati, yeye anatoa majibu rahisi kwa suala nyeti, eti zamani umeme ulikuwa haukatiki kwa sababu watu waliogopa kukata umeme wasifukuzwe kazi. Sasa kwa nini ssa hivi umeme usipatikane?, hoja ya maintenance ni hoja mfu kwa sababu nchi nyingine zinafanya maintenence na umeme unaendelea kupatikana

CCM walitwambia katiba mpya siyo hitaji la msingi bali hitaji la msingi ni maji, Sasa hayo maji yako wapi?

Umeme uko wapi?
 
Maji na umeme ni biashara za watu.

Watu wanarudisha biashara zao kwa kuhonga dawasco wakate maji ili wao watuuzie na ma water boozer truck yao
Magufuli amewahi kutudokeza kuwa kuna watu walikuwa wabafungulia maji kwenye mabwawa ya kuzalishia umeme ili maji yapungue kisha tushindwe kuzalisha umeme ili Wauze Majenerta yao!

Hii ishu ya maji haikubaliki, Watu mpaka wananuka, maji ya kuoga hakuna!
 
Januari Makamba waziri wenu wa Nishati , yeye anachojua ni kupost mitandaon akiwa kwenye vikao vya kahawa na wale mabeberu wa Asia.

Baada ya kuhangaika kushughulikia masuala mtambuka ya ukosefu wa umeme
Huyu waziri hamna kitu..kaenda kuteua washikaji zake Maharage..Mafuru..et al...ukimuona utasema mtu smart si ndio huyu....kumbe sinema tu
 
Kufeli kwa serikali ya CCM sasa kumegonga pentagoni. Jiji la Dar es laam sasa limegeuka jiji la uhaba wa maji na umeme.

Kwenye ishu ya maji, kuna mgao wa siku tatutatu na maji yanatoka masaa machache kisha yanakatika.

Hali hiyo imefanya watu waanze kuhangaika na ndoo na madumu kutafuta maji

Tumerudi enzi zile za Mzee Mwinyi, jiji lilikuwa na uhaba wa maji wa kufa mtu

Wakati hayo yakiendelea, umeme nao umekuwa bidhaa adimu.

Waziri wa Nishati, yeye anatoa majibu rahisi kwa suala nyeti, eti zamani umeme ulikuwa haukatiki kwa sababu watu waliogopa kukata umeme wasifukuzwe kazi. Sasa kwa nini ssa hivi umeme usipatikane?, hoja ya maintenance ni hoja mfu kwa sababu nchi nyingine zinafanya maintenence na umeme unaendelea kupatikana

CCM walitwambia katiba mpya siyo hitaji la msingi bali hitaji la msingi ni maji, Sasa hayo maji yako wapi?

Umeme uko wapi?
Kwenye umeme kumedoda Hana mpango nako, amejikita kwenye Gesi na mafuta ndo Kuna pesa na atazipiga huko, hiyo TANESCO waendelee kukata wameachiwa uhuru
 
Kimara baruti maji yapo 24hrs
TAARIFA KWA UMMA

KUPUNGUA KWA UZALISHAJI MAJI MTAMBO WA RUVU CHINI

23.10.2021
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) inawataarifu wananchi na wakazi wa Bagamoyo Mkoani Pwani hadi Kigamboni Jijini Dar es salaam kuwa, kutakuwa na upungufu wa huduma ya maji .

Sababu: Upungufu wa maji katika chanzo cha Mto Ruvu.

Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Wizara ya Maji kupitia Bonde la Wami Ruvu, kina cha maji cha mto Ruvu kimepungua kufuatia kiangazi cha muda mrefu.

Kufuatia upungufu wa maji mtoni, uzalishaji wa Maji umepungua kutoka lita milioni 520 kwa siku hadi kufikia lita milioni 460. Upungufu huo unatokana na kupungua kwa uzalishaji katika mtambo wa Ruvu Chini ambao husambaza maji kwa asilimia 70 ya eneo la huduma la DAWASA. Mtambo wa Ruvu Chini kwa kawaida huzalisha lita milioni 270 kwa siku na hivi sasa unazalisha kiasi cha lita milioni 210 kwa siku.

DAWASA kwa kushirikiana na Ofisi za Bonde la Wami Ruvu wanaendelea na zoezi la kusitisha matumizi ya maji kwa watumiaji wengine katika mto huo ikiwa ni pamoja kusitisha vibali vya umwagiliaji ili kuruhusu maji kufika mitamboni.

Ili kuhakikisha kuwa maji yanapatikana kwa usawa katika eneo linalohudumia na mtambo wa Ruvu Chini, DAWASA imehamisha sehemu ya maji ya Ruvu Juu ili yatumike kwa maeneo yaliyokuwa yanahudumiwa na Mtambo wa Ruvu Chini. Mabadiliko haya yanapelekea kupungua kwa msukumo wa maji kwa baadhi ya maeneo.

Maeneo yatakayo athirika: Maeneo yote yanayohudumiwa na mtambo wa Maji Ruvu chini, kuanzia Bagamoyo hadi Kigamboni.

DAWASA inawaomba wananchi kutumia maji kwa uangalifu katika kipindi hiki.

Tupigie kupitia kituo cha huduma kwa wateja 0800110064 au ujumbe mfupi 0735202121 (WhatsApp)

Imetolewa na
Kitengo cha Mawasiliano na Jamii- DAWASA
 
Magufuli amewahi kutudokeza kuwa kuna watu walikuwa wabafungulia maji kwenye mabwawa ya kuzalishia umeme ili maji yapungue kisha tushindwe kuzalisha umeme ili Wauze Majenerta yao!

Hii ishu ya maji haikubaliki, Watu mpaka wananuka, maji ya kuoga hakuna!
Na joto hili😑😑
 
Back
Top Bottom