Wakazi wa Buzwagi watawanywa kwa risasi, mabomu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wakazi wa Buzwagi watawanywa kwa risasi, mabomu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Tuandamane, Apr 23, 2008.

 1. T

  Tuandamane JF-Expert Member

  #1
  Apr 23, 2008
  Joined: Feb 2, 2008
  Messages: 1,220
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Huu si ndio ule unaodaiwa kuwa ni wa mkapa??
  Mkapa umefikia hatua hii???  WANANCHI waliohamishwa kupisha ujenzi wa Mgodi wa Buzwagi, wilayani Kahama jana

  walitawanywa kwa risasi na mabomu ya kutoa machozi yaliyokuwa yakipigwa na Polisi kuzima jaribio lao la kutaka kurudi kwa nguvu katika makazi yao.


  Jaribio hilo ambalo lilitangazwa juzi na wananchi hao lilianza alfajiri jana
  baada ya wananchi hao kukusanyika kwa wingi wakiwa na mabango mbalimbali wakitaka
  kurudi kwa nguvu kwenye makazi yao ambayo yapo ndani ya uzio wa Mgodi wa Buzwagi.


  Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Magesa Mulongo alisema kuwa kabla ya wananchi hao kutaka
  kuvamia kurudi kwenye makazi yao walisambaza ujumbe kwenye simu za mikononi
  ikiwemo simu yake unaodai kuwa umetoka kwa mtu mwenye nguvu ya kushawishi wananchi.


  Mulongo alisema katika ujumbe huo, wananchi walidai kwa kuwa hawana uwezo wa kuinunua dola(serikali) ili iwatusaidie, watadai haki yao kwa kuweka rehani damu yao na kwamba ujumbe huo ulisambazwa kwa viongozi mbalimbali wa Serikali.


  Alisema wananchi hao tayari wamelipwa fidia kwa asilimia 98, lakini baada ya kutumia vibaya fedha hizo, wamerudi kudai upya kwa maelezo kwamba walipunjwa wakati wa kuingia mkataba wa fidia na Kampuni ya Barrick.


  Kufuatia tukio la jana, ambapo watu14 wanashikiliwa na polisi wilayani hapa, Mulongo alifahamisha kuwa wananchi hao walivamia mgodi huo kwa lengo la kuuhujumu.


  Alisema licha ya Kamati ya Ulinzi na Usalama kuwazuia kuvamia eneo hilo, waligoma kuondoka kwa madai ya kwamba mpaka Mbunge wao James Lembeli afike mgodini hapo.


  Wananchi hao waliokuwa wakipiga makelele wakidai kuwa wamiliki wa mgodi huo
  ni makaburu na mafisadi, walidai kuwa mbuge wao aliwaagiza kuwa warudi katika maeneo yao ambayo tayari walikwishalipwa fedha na nyumba zao kubomolewa kupisha ujenzi wa mgodi huo.


  Kwa mujibu wa Mkuu wa Wilaya, kampuni ya Barrick ilikwishajenga nyumba 205 za fidia kwa wananchi walioondolewa, lakini nyumba 50 kati ya hizo bado zipo wazi baada ya wenyewe kugoma kuhamia, kwa sababu zisizoeleweka.


  Mgodi huo wa Buzwagi umejumuisha vijiji vitatu, ambapo katika kijiji cha Mwendakulima tayari wote wameondoka na Mwime, familia tisa zimegoma huku zikiwa zimelipwa fidia na bado zimo ndani ya uzio wa kampuni hiyo.


  Mulongo alisema kuwa katika Kijiji cha Chapulwa familia nne zimegoma kuondoka zikiwa zimelipwa fidia isipokuwa moja ambayo ilikataa kupokea.


  Katika tukio la jana wananchi hao wapatao zaidi ya 500 walikuwa wamezingira lango kuu la kuingia mgodini hapo.


  Licha Mkuu Wilaya kuwata waondoke wakafanye mkutano katika ofisi za Serikali za Vijiji vyao ili kupata mwafaka wa haki zao, wananchi hao waligoma.

  Baada ya kuona vurugu zinakuwa kubwa polisi waliingilia katina walianza kurusha risasi na mabomu ya kutoa hewani ili kuwatawanya wananchi.Katika vurugu hizo watu 14walikamatwa, lakini vinara wa vurugu hizo walitimua mbio kukwepa mkono wa sheria na polisi wanaendelea kuwasaka.


  Kuanzia jana mgodi huo upo chini ya ulinzi mkali wa Jeshi la Polisi kutoka Shinyanga wakishiriana na wa wilayani Kahama.

  http://www.mwananchi.co.tz/newsre.asp?id=5633
   
 2. M

  Mwafrika wa Kike JF-Expert Member

  #2
  Apr 23, 2008
  Joined: Jul 5, 2007
  Messages: 5,194
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Huu ni mgodi wa Kikwete kupitia kwa rafiki yake mkubwa Karamagi. Nadhani wale wanaoshauri wanafunzi wa chuoni kukaa kimya tu wakati haki zao zikipotea, wawashauri pia wakazi wa Buzwagi kukaa kimya na kukubali kunyanyaswa na polisi.
   
 3. T

  Tuandamane JF-Expert Member

  #3
  Apr 23, 2008
  Joined: Feb 2, 2008
  Messages: 1,220
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Asante sana Mwafrika wa kike, hivi hawa wananchi wakiamua kutotishika na hiyo mitutu watu wangapi watapoteza maisha, naomba kuomba msaada kwa aliekuwepo eneo la tukio atuambie kama kweli kulikuwa na ulazima wa kutawanya watu kwa risasi??? basi hata kuiga kwenye TV jinsi askari wa nchi zilizo indelea wanavowazuia watu na ngao???
   
 4. M

  Mwafrika wa Kike JF-Expert Member

  #4
  Apr 23, 2008
  Joined: Jul 5, 2007
  Messages: 5,194
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Kuna mtu atawashauri hapa kuwa wafuate taratibu za kuomba vibali vya polisi na wasiulize maswali chochote kile kinachofanywa na serikali yao.

  Ni suala la muda tu kabla wananchi hawajasema kuwa imetosha
   
 5. T

  Tuandamane JF-Expert Member

  #5
  Apr 23, 2008
  Joined: Feb 2, 2008
  Messages: 1,220
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Halafu huwezi kuamini kabisa hawa jamaa bado wamelala, hawaoni kabisa kama hii inakuja na imekaribia
   
 6. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #6
  Apr 23, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  CCM bwana .Yaani wazungu wanatucheka .Magesa analeta longo longo sawa na kule UD jamani fedha fedheha na haya yana mwisho .Laana hii inatambaa kwa kasi .Nchi ni yetu sote .
   
 7. Single D

  Single D JF-Expert Member

  #7
  Apr 23, 2008
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 459
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Hawa maafande wetu hawajajijua kuwa wamekuwa watumwa wa mafisadi.
  Kwa nini wasijifunze kwa wenzao Ulaya?Ulaya watu hawatumii glucose nyingi kutawanya maandamano.Tena utaona wanatumia akili kuzuia ili wasisababishe maafa.
  Haki za binadamu nadhani ni wakti muafaka wa kuwahubiri hawa maafande wetu watumie mbinu za vita vya majimaji.Yaani akili sana kuliko kutumia glucose nyingi.

  Wale wananchi wamedhulumiwa na kila kukicha huyu mkuu wa Wilaya na mbunge wanaimba wimbo usiokoma masikioni mwao kuwa serikali inashughulukia matatizo yenu.

  Basi tunakoelekea maafande wengi nao watavunjika miguu kama jana kule UDSM,Maana risasi zitakuwa za kawaida tu kwa wananchi na hawataziogopa.
   
 8. M

  Mwafrika wa Kike JF-Expert Member

  #8
  Apr 23, 2008
  Joined: Jul 5, 2007
  Messages: 5,194
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Wao bado wanaamini kuwa watanzani watachukua tisheti na kofia za kijani toka kwa mwizi na mkoloni mwenye uraia wa utata Rostam Azizi wakati wa uchaguzi na ccm itashinda tena kwa 'Kishindo'
   
 9. M

  Mwafrika wa Kike JF-Expert Member

  #9
  Apr 23, 2008
  Joined: Jul 5, 2007
  Messages: 5,194
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Serikali ya ccm haijali wananchi wake. Kikwete yuko bize anazunguka dunia, Shein yuko bize na mikasi akifungua bucha za nyama. Pinda ndiyo hivyo tena anajichanganya bungeni kila siku.

  Yaani hakuna kinachoendelea. Wanajua jeshi na polisi vipo na ndio maana wamefikia hatua ya kuingilia chaguzi za wanafunzi wa vyuo vikuu ili waweke mapandikizi yao kupitia kwa wasomi ambao pia ni mafisadi na madikiteta (wauaji?) kama Mkandara
   
 10. T

  Tuandamane JF-Expert Member

  #10
  Apr 23, 2008
  Joined: Feb 2, 2008
  Messages: 1,220
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Yani hilo jina tu nikiliona moyo wangu unalipuka kwa hasira, iko siku..... na sema iko siku.....
   
 11. M

  Mwafrika wa Kike JF-Expert Member

  #11
  Apr 23, 2008
  Joined: Jul 5, 2007
  Messages: 5,194
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  HIyo siku inakuja kwa kasi na mipango inaelekea kukamilika!
   
 12. T

  Tuandamane JF-Expert Member

  #12
  Apr 23, 2008
  Joined: Feb 2, 2008
  Messages: 1,220
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Ningewashauri waanze kuhangaika kumfata Balali aliko na kutuachia nchi yetu...... tumechoka kutukanwa na kuonwa wajinga
   
 13. mwanatanu

  mwanatanu JF-Expert Member

  #13
  Apr 23, 2008
  Joined: Jan 22, 2008
  Messages: 850
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 45
  Mwafaka mwafaka mwafaka...mpaka lini? next karne?
  mbona walichukua migodi hiyo kirahisi na sasa mwafaka...big up buzwagians
   
 14. M

  Mwafrika wa Kike JF-Expert Member

  #14
  Apr 23, 2008
  Joined: Jul 5, 2007
  Messages: 5,194
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Sidhani kama wanaweza kufanya hili as longer as wana polisi na jeshi na huku wakiwa wamejazana bungeni na spika wao mzee wa vimada - Six
   
 15. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #15
  Apr 23, 2008
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  yaani inaaibisha. tanzania kila leo tunasifiwa kwa amani tuliyonayo, lakini wanachoshindwa kuelewa hao wanaosifu ni kuwa sio amani ya khiari, kuna uvunjaji wa haki za binaadamu wa kila aina ila mtanzania ni mnyonge sana kulinganisha na nguvu za dola kiasi cha kuwa anabaki kuwa na 'amani'
  si tulisikia tume ya haki za binaadamu kutangazwa na kikwete kwa kicheko kingi kwenye picha alipozungukwa na akina mama warembo kila kona, sasa tuone hii tume itafanya kazi gani?
  langu jicho
   
 16. M

  Mwafrika wa Kike JF-Expert Member

  #16
  Apr 23, 2008
  Joined: Jul 5, 2007
  Messages: 5,194
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Kumbe uliona hili gaijin? kazi kweli hapa na kisha risasi zitatembea hadi wakome kwa kumzomea Kikwete alivyotembelea Shinyanga kipindi kile!
   
 17. Icadon

  Icadon JF-Expert Member

  #17
  Apr 23, 2008
  Joined: Mar 21, 2007
  Messages: 3,589
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  Kabla ya kwenda mbali ni kweli hao wananchi wamelipwa fidia?
   
 18. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #18
  Apr 23, 2008
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Ukisoma gazeti za leo, kuna listi za watuhumiwa wa kuongoza zali hili.

  Funny enough "viongozi" hawa ni watu influencial katika jamii, Waalimu, Shekhe, Wachungaji, Viongozi wa vyama na kazwalika.

  Hii ni ishara kamili ya umoja wa Wananchi kutetea haki zao.

  Chakusikitisha, hawa jamaa wamepelekwa mahakamani, wakakataa makosa waliyotajiwa, wamewekwa Lupango!

  Sasa twapotoza fedha za nini kushikilia waandamanaji Lupango?
   
 19. M

  Mwafrika wa Kike JF-Expert Member

  #19
  Apr 23, 2008
  Joined: Jul 5, 2007
  Messages: 5,194
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Hili ni swali gumu sana Rev,

  Serikali inabidi ijifunze kuwa matumizi ya nguvu sio suluhisho la matatizo ya nchi yetu.
   
 20. Mdau

  Mdau JF-Expert Member

  #20
  Apr 23, 2008
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,771
  Likes Received: 251
  Trophy Points: 180
  shame on you mkapa,damu za watanzania wote wanaokufa kwa matatizo ya umaskini zipo juu yako!!!
   
Loading...