Wakazi wa bonde la Msimbazi hawapaswi kuonewa huruma | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wakazi wa bonde la Msimbazi hawapaswi kuonewa huruma

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mpayukaji, Dec 22, 2011.

 1. mpayukaji

  mpayukaji JF-Expert Member

  #1
  Dec 22, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 943
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Ingawa serikali yetu nayo inahusika kwenye upuuzi huu wa kuacha watu wajenge kwenye mkondo wa maji wakijua fikia kuwa siku ikifika ni mauti kwao, wakazi wa bonde la Msimbazi hawapaswi kutuumiza vichwa kwa yaliyowakuta kwani waliyataka wenyewe. Hivi unapojenga kwenye mkondo wa maji unategemea nini jamani? Tufikie mahali tuanze kutii sheria iwe ya nchi au maumbile. Leo barabara za Kariakoo zimefurika wamachinga. Hivi ikitokea gari likawagonga na kuua mamia tuanze tena kumlaumu Mungu? Kwanini tusifukuze wamachinga wa kihindi na kichina na kuwapa wetu sehemu za kufanyia biashara badala ya barabarani?
   
 2. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #2
  Dec 22, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  uko sahihi mkuu, siku zote nina huo mtazamo.wakati mwingine wanadiriki hata kulaumu serikali kwa mambo waliyoyafanya wenyewe kwa kupuuza tu kama hili la kujenga mabondeni. anyway!
   
 3. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #3
  Dec 22, 2011
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  lakini serikali si ndo inawauzia viwanja?? Serikali imepeleka umeme na maji!
   
 4. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #4
  Dec 22, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Kwel wewe mpayukaji,pole
   
 5. MwafrikaHalisi

  MwafrikaHalisi JF-Expert Member

  #5
  Dec 22, 2011
  Joined: Oct 12, 2011
  Messages: 1,746
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Unaitwa mpayukaji eh? Hawa watu wanalipa kodi ya jengo. Wamewekewa umeme na wanalipia. Kwanini serikali isilaumiwe?

  Serikali imefanya jitihada gani KUHAKIKISHA wanahama huko bondeni? Tusijisahaulishe Watanzania tuna hali ngumu ya maisha. Wewe unaona rahisi kumwambia ahame. Ila yeye anajiuliza akihama ataenda wapi? Na hapo kajibanabana kapata vyumba viwili?
   
 6. m

  mzawahalisi JF-Expert Member

  #6
  Dec 22, 2011
  Joined: Jan 11, 2010
  Messages: 744
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 45
  Jamani mimi nimezaliwa nakua nakuta hawa watu wanaambiwa wahame, lakini kilasiku wanjenga wapya. Yale ya elininyo yaliwakuta, serikali ikatoa msaada wa kuwaokoa huku ikipiga kelele za kuwahamisha. Sijui hata nisemeje. Nakuja Gundua ni kazi kwelikweli kuongoza uma wa watu.
  Je ww kama kiongozi utawafanyaaje hawa?
  Je utachukua kodi za wemgine ukawajengee hawa ilihali wengi mikoani hawana huduma za jamii? Huo si utakuwa ufisadi?
   
 7. mwakaboko

  mwakaboko JF-Expert Member

  #7
  Dec 22, 2011
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 1,841
  Likes Received: 253
  Trophy Points: 180
  wakazi wale pia ni tatizo, sawa serikali ina mapungufu yake
  lkn kwa hili la bonde la Msimbazi, wananchi nao wanapaswa kulaumiwa.
  Kwa wenye kumbukumbu nzuri, Mr.Makamba alilipigia kelele sn jambo hili
  mpaka akaamua awahamishe kwa nguvu sjui kitu gani kilitokea hakukamilisha
  plan yake. WALIONYWA mapema wakapuuzia, haya yote yasingewapata.
  POLENI SANA NDUGU ZANGU ILA UKWELI UNAUMA, BEAR WITH ME
   
 8. M

  Mike 1234 JF-Expert Member

  #8
  Dec 22, 2011
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 1,634
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  aisee unafikiria zaidi kuliko hata viongozi wako,nakuunga mkono upo sawa
   
 9. Kilahunja

  Kilahunja JF-Expert Member

  #9
  Dec 22, 2011
  Joined: Dec 19, 2011
  Messages: 1,497
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Ua very right friend
   
 10. N

  Ndevu mbili JF-Expert Member

  #10
  Dec 22, 2011
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 382
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  ukiwatoa huko kura zao utazikosa!
  Hiyo mitaji yao!
  Maeneo mazur ni tatizo wao kuyapata...majumba ya kupangisha wanapewa wenye uwezo japo zilijengwa kwa wenye hali duni. Sasa wenye hali duni ndio yanayowafika ya kuwafika. Muhim iwekwe sera kila mafuriko yakikaribia au kutokea wasaidiwa haraka na wapewe misaada muhim haraka pia.
   
 11. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #11
  Dec 22, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 17,966
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  Serikali haipimi viwanja vya kutosha na bei muafaka kwa wananchi wote kupata,akajenge wapi?
   
 12. m

  mariavictima Senior Member

  #12
  Dec 22, 2011
  Joined: Jul 8, 2010
  Messages: 180
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Usishangae baada ya mafuriko wote wakarudi tena maeneo yale yale.
   
 13. Consigliere

  Consigliere JF-Expert Member

  #13
  Dec 22, 2011
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 8,026
  Likes Received: 7,416
  Trophy Points: 280
  Siwasikitikii hao bali Ninasikitika kwa ajili ya watoto wao, pia nawasikitikia wale walioathirika ili hali hawakujenga mabondeni na ninsikitika kwa ajili ya miundombinu na usumbufu uliojitokeza na utakaofuata.
   
Loading...