Wakazi wa asili wa Zanzibar ni watu gani?

Red Giant

JF-Expert Member
Mar 9, 2012
15,237
2,000
Maana miaka ya 1800 Sultani alianzisha kilimo cha karafuu Zanzibar. Biashara hii na ile ya utumwa ilikuwa ya pesa nyingi. Mwishowe akaamua yeye mwenyewe kuhamia Zanzibar.

Hapo waarabu kibao kutoka Oman wakahama naye. Wakaanzisha mashamba ya karafuu na kuweka watumwa kibao kufanya kazi. Hata leo wakazi wengi unakuta wanaasili ya wanyamwezi, wayao, hadi wamanyema kutoka Congo. Mababu zao walikuwa watumwa.

Sasa wakazi wa asili kabisa wa Zanzibar ni watu gani? Lugha yao ni ipi? Au kulikuwa hakuna watu, maana visiwa vingi vya bahari ya hindi vilikuwa haviishi watu miaka watu wameanza kusafiri huku na huko baharini.
 
Jumbe Brown

JF-Expert Member
Jun 23, 2020
10,331
2,000
Maana miaka ya 1800 Sultani alianzisha kilimo cha karafuu Zanzibar. Biashara hii na ile ya utumwa ilikuwa ya pesa nyingi. Mwishowe akaamua yeye mwenyewe kuhamia Zanzibar. Hapo waarabu kibao kutoka Oman wakahama naye. Wakaanzisha mashamba ya karafuu na kuweka watumwa kibao kufanya kazi. Hata leo wakazi wengi unakuta wanaasili ya wanyamwezi, wayao, hadi wamanyema kutoka Congo. Mababu zao walikuwa watumwa.

Sasa wakazi wa asili kabisa wa Zanzibar ni watu gani? Lugha yao ni ipi? Au kulikuwa hakuna watu, maana visiwa vingi vya bahari ya hindi vilikuwa haviishi watu miaka watu wameanza kusafiri huku na huko baharini.
Mbona waarabu wa Oman wamekuja miaka ya karibuni tu.

Visiwa huwa havina watu wa asili....wananchi walianza kuhamia huko karne nyingi tu zilizopita....mathalani Uislam uliingia Zanzibar karne ya 7 kwa kuletwa na WAFANYABIASHARA wa Persia/Uajemi....na ndio maana walio wengi ni wafuasi wa madhehebu ya SUNNI na si IBADHI(OMAN).

Hata ukristo uliingia Zanzibar karne nyingi mno kabla ya hao waarabu wa Oman.

Wenyeji wa Zanzibar wametokea Tanganyika,Pwani ya Kenya ,Sudan,Uganda Comoro,Malawi,Msumbiji na DRC.

Ni miaka ya hivi karibuni wakati wa utawala wa hayati Abeid Amani Karume kuwataka WAZANZIBARI waitwe WASHIRAZI ili kuondoa UBAGUZI NA MATABAKA.

#SiempreJMT
 
GwaB

JF-Expert Member
Mar 19, 2014
2,210
2,000
Maana miaka ya 1800 Sultani alianzisha kilimo cha karafuu Zanzibar. Biashara hii na ile ya utumwa ilikuwa ya pesa nyingi. Mwishowe akaamua yeye mwenyewe kuhamia Zanzibar. Hapo waarabu kibao kutoka Oman wakahama naye. Wakaanzisha mashamba ya karafuu na kuweka watumwa kibao kufanya kazi. Hata leo wakazi wengi unakuta wanaasili ya wanyamwezi, wayao, hadi wamanyema kutoka Congo. Mababu zao walikuwa watumwa.

Sasa wakazi wa asili kabisa wa Zanzibar ni watu gani? Lugha yao ni ipi? Au kulikuwa hakuna watu, maana visiwa vingi vya bahari ya hindi vilikuwa haviishi watu miaka watu wameanza kusafiri huku na huko baharini.
Hii mada imeisha jadiliwa sana humu, mara zote mjadala huishia kutupiana madongo kati ya ng'ambo hii na ng'ambo ile kule.

Hebu pitia hapa upate ilmu zaidi.
 
Attachments

  • File size
    594.8 KB
    Views
    13

Science Priest

JF-Expert Member
Mar 7, 2019
2,260
2,000
Zanzibar a land of black people, utashangaa mto Uzi atakuambia amesoma na amenaliza degree na vitu kama hivi vya kawaida avijui watanzania wengi wanasoma ili kupata vyeti
 
mfianchi

JF-Expert Member
Jul 1, 2009
10,803
2,000
Maana miaka ya 1800 Sultani alianzisha kilimo cha karafuu Zanzibar. Biashara hii na ile ya utumwa ilikuwa ya pesa nyingi. Mwishowe akaamua yeye mwenyewe kuhamia Zanzibar. Hapo waarabu kibao kutoka Oman wakahama naye. Wakaanzisha mashamba ya karafuu na kuweka watumwa kibao kufanya kazi. Hata leo wakazi wengi unakuta wanaasili ya wanyamwezi, wayao, hadi wamanyema kutoka Congo. Mababu zao walikuwa watumwa.

Sasa wakazi wa asili kabisa wa Zanzibar ni watu gani? Lugha yao ni ipi? Au kulikuwa hakuna watu, maana visiwa vingi vya bahari ya hindi vilikuwa haviishi watu miaka watu wameanza kusafiri huku na huko baharini.
Zanzibar haina watu wa asili wote ni wahamiaji (mabaharia) nikisiwa kilichotumiwa na wavuvi kupumzika, ndio maana Zanzibar haina wenyewe utasikia tu Wamakunduchi hao wanatoka Makunduchi mkoa wa Kaskazini, Wapemba wanatoka Pemba, Watumbatu kuna wanyamwezi ,Wamalawi,Wanyamwezi,Wakongo,Wangoni, Wakurya,Waarabu,Wacomoro,Wachina,Wahindi, Wazaramo,Wamakonde nk.
 
mfianchi

JF-Expert Member
Jul 1, 2009
10,803
2,000
Wazazi wake walitokea huko....

Ila hata baadhi ya makabila ya Tanzania yametokea huko....Nyakyusa ,Wamwera ,Wayao n.k
Wanyakyusa hawajatoka Zenj bana wao asili yao Morogoro ,Mahenge, ambapo baba alitoka Afrika ya Kusini akaoa mtoto wa kipogoro ndio likawa zao la Wanyakyusa, na hata majina mengi ya vijiji vya Mahenge/Kilombero yanafanana na majina ya vijiji vya wakazi wa Rungwe , Kyela , Busokelo na Ileje ambako ndio ngome ya Wanyakyusa ambao wamevuka hadi Malawi wanakoitwa Wangonde.
 
dos.2020

JF-Expert Member
Feb 17, 2009
5,024
2,000
Unatakiwa utafautishe ujio wa Sultan kutoka Oman na ujio wa waarabu hivo ni vitu viwili tofauti, Waarabu wapo zanzibar zaidi ya miaka 1000 kabla ya kuja huyo Sultan unaemzungumza.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom