Wakazi wa Arusha walazimishwa kwenda kuwatazama JK na Mafisadi..

Crashwise

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
22,227
8,735
Kitendo cha kutuambia tufunge biashara zetu kisa kikwete anakuja kwenye shughuli za kisiasa kimeni kera sana...Jana tumepokea taarifa tukiambiwa tusifungue ofisi zetu kuanzia saa saba mchana kwa majengo yenye gorofa yaliyo karibu na uwanja wa sheikh Amri Abeid...eti kwa usalama wa JK...cha kushangaza soko la crocon lilioko umbali wa takribani km 1 nalo limeamliwa kufungwa eti waka msikilize JK na CCM yake, je hizi siyo njia chafu zinazotumiwa na CCM kuhakikisha wana pata watu wengi mikutano yao kwani hata Dar tulishuhudia CCM ikikodisha magari ili yasafirishe watu kwenda na kurudi kwenye uwanja wa jangwani...sijui mikoani anatumia mbinu gani zingine...
 
Attachments

  • kwaheri.jpg
    kwaheri.jpg
    53.3 KB · Views: 148
CCM kulazimisha watu wakamsikize JK, inaonyesha kwamba wameshazidiwa. Maana wanaona mikutano ya Slaa inapata wafuasi wengi ajabu, kwa hiyo wanatafuta kulazimisha ili waonekane na wenyewe wana watu wengi. Lakini mwaka huu CCM ikubali au ikatae, hali yake ni mbaya kwani umati wa watu wanaohudhuria kwenye mikutano ya Dr Slaa bila kuletwa na magari wala kuamrishwa kufunga biashara ni wengi sana. Si ajabu kama CCM ingewapa watu uhuru wa kuhudhuria mikutano kutokana na utashi wao isingepata watu wa kuja kwenye mikutano.
 
Mkifunga biashara zenu mtalipwa bei gani??? CCM acheni upuuzi wa kuwalazimisha watu wafunge kazi zao kisa Mzee wa kuaidi anamkutamo lol mnatia aibu. mmeona Arusha hawadanganyiki kwa kukodiwa magari ya kuwabeba na posho za kushangilia sasa mnawaambia watu wafunge biashara zao.

Ama kweli siku ya kufa nyani miti yote huteleza na bado kivumbi ni Octoba 31 hakuna kuchackachua kura
 
hee sasa mfunge biznec zenu mkale wapi? serikali ambayo haiwajali kwa moja wala mbili ndio inawaambia mfunge biznec....mie hii nchi imenichosha.
 
Hii picha inaonyesha genge la watu waliokata tamaa, kila mmoja anawaza chake hakuna mwenye kusikiliza muhutubi.
 
Hii post yako mbona haieleweki mkuu? sasa hicho kichwa cha nguruwe na Kuruan zinatafuta nini kwenye post yako? Naamini hukutarajia kuiweka hivyo, iedit halafu uondoe hiyo attachment inayoharibu post yako.
Kuhusu CCM kulazimisha watu wakamsikize JK, .
Nikweli mkuu sikutarajia..pole kwa usumbufu ulioupata..
 
Kha! hii nakumbuka ilikuwaga zamani kama kuna kiongozi anakuja basi siku hiyo inaharibika na shughuli zinasimama kumbe bado inaendelea! poleni sana jamani
 
CCM wanajua popularity yao inaelekea zero..
Hii ni baada ya kuwaongezea wananchi umaskini wa kipato..maana kifikra wanaanza tajirika..
 
Hapa Arusha wale Boda boda (waendesha biashara ya kubeba abiria kwa pikipiki) hulipwa 5000 hadi 10000 kushiriki misafara ya kampeni na kulazimishwa kupeperusha bendera za ccm. hili la kufunga biashara sioni ajabu sana maana pia wanatishwa.
 
Mbaya zaidi jiji la Arusha lilivyo na miundo mbinu barabara moja tu ikifungwa mji mzima unataabika leo watakapofunga sijui itakuwaje... Kikwete na CCM yake ameshindwa kututatulia halafu wanatuambia kafanya mengi yapi?..barabara hakuna, wameshindwa hata kujenga stand ya mabasi..stand iliyoko hata kampuni moja ikiamua kupaki mabasi yake yote haitoshi (Mtei) halafu eti wanaita stand kuu, stand ndogo naenye hafai yaani hata vibasi vya sakina havitoshei..sijui ni vigezo gani vilitumika wapa uizinisha kuwa jiji au fance za matairi...
 
kweli ukistaajabu ya musa utaona ya filauni,,,,,
na mpango wa kwenda kulala niamke siku ya kumpigia kura dr. slaa.
 
Kitendo cha kutuambia tufunge biashara zetu kisa kikwete anakuja kwenye shughuli za kisiasa kimeni kera sana...Jana tumepokea taarifa tukiambiwa tusifungue ofisi zetu kuanzia saa saba mchana kwa majengo yenye gorofa yaliyo karibu na uwanja wa sheikh Amri Abeid...eti kwa usalama wa JK...cha kushangaza soko la crocon lilioko umbali wa takribani km 1 nalo limeamliwa kufungwa eti waka msikilize JK na CCM yake, je hizi siyo njia chafu zinazotumiwa na CCM kuhakikisha wana pata watu wengi mikutano yao kwani hata Dar tulishuhudia CCM ikikodisha magari ili yasafirishe watu kwenda na kurudi kwenye uwanja wa jangwani...sijui mikoani anatumia mbinu gani zingine...

Mi nimevurugwa akili na haya mahelikopta ma3 ya hicho chama, yani yana kelele za ajabu..kuna limoja nadhani ni libovu kabisa na ndo kubwa kuliko yote, yamepita eneo ninayofanyia shughuli imebidi tupoteze kama dakika10 za muda wa tija!
Kweli tunahitaji mabadiliko!...Ufujaji wa pesa usio na sababu kama huu, kweli inahitaji akili za kushikilia na supa gluu!
 
Mwaka huu watajiju ha ha maji mushingo na watu wa arusha mukakubali ha ha ha mumelala kweli pole zenu,
 
ukifunga biashara wanakusubiri nje? si ufunge kisha ukanywe mbege yako au ukale trupa yako?
 
Kitendo cha kutuambia tufunge biashara zetu kisa kikwete anakuja kwenye shughuli za kisiasa kimeni kera sana...Jana tumepokea taarifa tukiambiwa tusifungue ofisi zetu kuanzia saa saba mchana kwa majengo yenye gorofa yaliyo karibu na uwanja wa sheikh Amri Abeid...eti kwa usalama wa JK...cha kushangaza soko la crocon lilioko umbali wa takribani km 1 nalo limeamliwa kufungwa eti waka msikilize JK na CCM yake, je hizi siyo njia chafu zinazotumiwa na CCM kuhakikisha wana pata watu wengi mikutano yao kwani hata Dar tulishuhudia CCM ikikodisha magari ili yasafirishe watu kwenda na kurudi kwenye uwanja wa jangwani...sijui mikoani anatumia mbinu gani zingine...

this is unfair!!!!!!!!!!!!!!!
 
Watu wamehamasishwa na si kwamba wamelazimishwa. Mimi niko Arusha, eneo nilipo sijaona mtu aliyelazimishwa kwenda uwanjani ila magari ya matangazo yanasikika, sijui tafsiri ya kulazimishwa ni ipi. Kama wewe ni mpangaji kwenye maeneo ya CCM ni wajibu wala siyo hiari kwenda uwanjani kumsikiliza landlord wako
 
REAL? You must be kidding
 
Back
Top Bottom