Wakazi Kigilagila waandamana kupinga vumbi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wakazi Kigilagila waandamana kupinga vumbi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Sep 17, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Sep 17, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,608
  Trophy Points: 280
  WAKAZI wa maeneo ya Kigilagila Wilayani Ilala wameandamana kupinga vumbi linalowaathiri afya zao linalotokana na kampuni iliyopewa tenda ya ujenzi wa uwanja wa ndege wa jijini. Wakazi hao waliandamana jana hadi katika kampuni hiyo ijulikanyo kama Interbetton ya nchini Uholanzi iliyopewa tenda hiyo ya ujenzi wa uwanja huo kupinga kusimamishwa kwa ujenzi huo.

  Jana wakazi hao walifika katika geti kuu la kampuni hiyo na kuchoma matairi kuashiria kuwa wamechoshwa na vumbi linalotoka kiwandani humo na kuwaathiri wakazi hao .

  Wakazi hao waliilalamikia kampuni hiyo kwa kusababisha vumbi kali ambalo linalosambaa kwenye makazi ya watu na kuwaathiri afya zao kwa kipindi kirefu sasa.

  Kutokana na malalamiko hayo wakazi hao Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Evans Balama aliamuru shughuli zinazofanywa na kampuni hiyo zisimame kwa muda hadi hapo mitambo itakaporekebishwa na kutotoa vumbi la kuwaathiri wakazi hao.

  Wakazi hao walilalama pia kuitaka serikali wapewe mafao yao ili waweze kuondoka maeneo hayo kupisha ujenzi wa uwanja huo.


  Source: Nifahamishe.com
   
 2. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #2
  Sep 17, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Kama wapo waliokwisha athirika na vumbi hilo basi wanahaki kabisa kufungua kesi ya madai kudai fidia.

  Wanasheria Tanzania mpo? wasaidieni wakazi hawa wapate haki zao kisheria
   
 3. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #3
  Sep 17, 2009
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Hilo vumbi la kigila gila ni ufisadi wa mbunge wenu Mahanga. Kama mna akili timamu lazima huyu bwana mumfukuze kazi mwaka kesho.; kawahadaa sana kwa siku nyingi!!
   
Loading...