Wakazi kata za Kalamba, Haubi watembea kilomita 100 kufuata matibabu Kondoa Mjini

Kande

Senior Member
Mar 15, 2016
116
106
Serikali imetoa milioni 600 kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya kitakachengwa katika kitongoji cha Itongwi kata ya Kalamba wilayani Kondoa ili kutatua changamoto ya upatikanaji wa huduma za afya.

Wakazi wa kata za Kalamba na Haubi wilayani Kondoa mkoani Dodoma wanalazimika kutembea umbali wa kilomita 100 kufuata huduma za afya mijini Kondoa kwasababu kata zao hazina kituo cha afya kama inavyoelekezwa katika Sera ya Afya ya mwaka 2007 ambayo inataka kila kijiji kiwe na Zahanati.

Kata hizo zenye wakazi wapatao 30,000 kwa muda mrefu sasa hawajafikiwa na huduma za uhakika za afya licha ya ahadi nyingi za kisiasa ambazo zimekuwa zikitolewa. Kutokana na ubovu wa miundombinu ya barabara wakazi hutumia rasilimali nyingi kufika Kondoa mjini ambako nako hakuna hospitali ya Wilaya kuweza kuhudumia wakazi wote.

Kutokana na hali hiyo wakazi hao kwa kushirikiana na viongozi wa vijiji vyao wametenga eneo la ekari sita kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya ambapo wamejitolea nguvu zao kusafisha eneo hilo ili kuepukana na adha ya muda mrefu ya kufuata huduma za afya Kondoa mjini.

Juhudi hizo zimewashawishi baadhi mawaziri na viongozi wa halmashauri hiyo kujitokeza na kutembelea eneo hilo kutekeleza wajibu wao wa kutoa huduma muhimu ikiwemo afya.

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kondoa Vijijini, ameguswa na jitijada za wananchi hao na ameishawishi serikali kutoa milioni 600 kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya katika kitongoji cha Itongwi.

Zaidi, soma => Wakazi kata za Kalamba, Haubi watembea kilomita 100 kufuata matibabu Kondoa Mjini | FikraPevu
 
Back
Top Bottom