Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wakatoliki watembea kwa miguu ‘kuhiji’ Butiama

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Rutashubanyuma, Jan 16, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Jan 16, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 62,135
  Likes Received: 636
  Trophy Points: 280
  Wakatoliki watembea kwa miguu ‘kuhiji’ Butiama

  Imeandikwa na Christopher Gamaina, Butiama; Tarehe: 15th January 2011 @ 23:45 Imesomwa na watu: 130; Jumla ya maoni: 0


  [​IMG]
  Baadhi ya waumini 180 wa Kanisa Katoliki Parokia ya Shirati, Rorya, mkoani Mara, wakisali kwenye kaburi la Mwenye Heri Julius Nyerere, kuomba Mungu awape baraka itakayofanikisha ukamilishaji wa jengo la Kanisa la Parokia hiyo. (Na Mpigapicha Wetu).  WAUMINI 180 wa Kanisa Katoliki Parokia ya Shirati, Rorya, mkoani Mara, wamehiji nyumbani kwa Baba wa Taifa, marehemu Mwalimu Julius Nyerere, kijijini Butiama, kuomba Mungu awape baraka itakayofanikisha ukamilishaji wa jengo la Kanisa la Parokia hiyo.

  Pia, mahujaji hao wameombea uimarishaji wa nguvu ya kiroho ya Bikira Maria anayeaminika kukabidhiwa na viongozi wa dini hiyo usimamizi wa amani na umoja katika Parokia ya Shirati na Tanzania kwa jumla.

  Mahujaji 97 kati yao, walisafiri kwa miguu umbali wa zaidi ya kilometa 100, waliondoka Shirati alfajiri ya Januari 12 na kuwasili kwa mwasisi huyo wa Taifa mchana Januari 14 mwaka huu.

  Paroko wa Parokia ya Shirati, Padri Konrad Caputa, aliongoza mahujaji waliosafiri kwa miguu akisaidiana na Mwenyekiti wa Parokia hiyo, Alex Wagara na Katibu wake, Sixtus Ogweyo.

  Baada ya kushiriki ibada katika Kanisa Katoliki Parokia ya Butiama na kuhiji kwenye kaburi la Mwalimu Nyerere, mahujaji hao walifanya mazungumzo mafupi na mjane wa Mwalimu, Mama Maria.

  Padri Caputa alisema anaamini maombi yao kupitia kwa Mtumishi wa Mungu, Mwalimu Nyerere, yatapokewa na Mungu na kufanikisha upatikanaji wa Sh milioni 400 zinazohitajika kugharimia ukamilishaji wa jengo hilo.

  Kwa upande wake, Mama Maria aliziombea mafanikio nia za mahujaji hao, huku akihimiza jamii nzima kuzidi kuiombea Tanzania amani, umoja na uadilifu kwa viongozi mbalimbali.

  Aidha, mjane huyo, alimkabidhi Padri Caputa kwa niaba ya mahujaji hao, vitabu na kadi kadhaa vinavyoelezea historia ya uongozi, uadilifu na maisha ya Mwalimu Nyerere.

  Kwa sasa, mamlaka husika duniani zinaendelea na maandalizi ya kumtangaza Mtumishi wa Mungu, Mwalimu Nyerere, kuwa Mwenye Heri chini ya imani ya Kanisa Katoliki.

  Kwa mujibu wa mwumini wa Kanisa Katoliki Parokia ya Shirati, Ngoje Ongati, hiyo ni mara ya pili kwa waumini hao kuhiji nyumbani kwa Mwalimu Nyerere.

  “Januari 14, mwaka jana tulikuja kuhiji hapa kwa Mtumishi wa Mungu (Nyerere) na Februari tulipata neema ya kuchangiwa Sh milioni 30 za kuendeleza ujenzi wa Kanisa letu la Shirati,” alisema Ongati.
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Jan 16, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 62,135
  Likes Received: 636
  Trophy Points: 280
  Hivi wanamwomba Munug au wanawaomba wanasiasa ili wawape misaada...................Mungu yupo kila mahali huhitaji kwenda kwenye kaburi la Nyerere ili kuwasiliana na Muumba wetu Mwenyezi Mungu............................
   
 3. Asante

  Asante JF-Expert Member

  #3
  Jan 16, 2011
  Joined: Dec 18, 2009
  Messages: 1,729
  Likes Received: 117
  Trophy Points: 160
  Huwa wanasema maneno gani makaburini?
   
 4. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #4
  Jan 16, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,573
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  nafikiri walienda kutalii tu na wakatumia fursa hiyo kupiga sala kidogo. but nasikia kuna mchakato wa kumtakatifuza huyo marehemu anayehusika na hilo kaburi
   
 5. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #5
  Jan 16, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 145
  :thinking::A S confused:
   
 6. October

  October JF-Expert Member

  #6
  Jan 16, 2011
  Joined: Oct 5, 2009
  Messages: 2,147
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  :faint::faint:
   
 7. k

  kibananhukhu JF-Expert Member

  #7
  Jan 16, 2011
  Joined: Jul 6, 2009
  Messages: 368
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Huwa wakatoliki wanasemaa {Eee Mungu wa Mwalimu Nyerere Tusaidie.....................}
   
 8. Tangawizi

  Tangawizi JF-Expert Member

  #8
  Jan 16, 2011
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 2,231
  Likes Received: 514
  Trophy Points: 280
  Jambo usilolijua ni kama usiku wa giza
   
 9. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #9
  Jan 16, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,573
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  huu nao naona ni upotovu wa imani. naona kama ushirikina vile. kama ni utalii waweke wazi sasa sala kwenye makaburi ya wanasiasa wapi na wapi? na mwingine hapo kulia ndio kapiga magoti utadhani kakutana na Mwenyezi Mungu kabisa!
   
 10. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #10
  Jan 17, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,971
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Mambo ya ajabu kweli kweli.
   
 11. Q

  Qadhi JF-Expert Member

  #11
  Jan 17, 2011
  Joined: Oct 27, 2009
  Messages: 235
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Aisee....!
   
Loading...