Wakatoliki: Hili ni bomu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wakatoliki: Hili ni bomu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Jan 30, 2008.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Jan 30, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,760
  Likes Received: 83,063
  Trophy Points: 280
  Wakatoliki: Hili ni bomu

  Mwandishi Wetu Januari 23, 2008
  Raia Mwema

  Sheikh Gorogosi: Sote tutalizwa kwa Mungu
  KWA mara nyingine Kanisa Katoliki nchini limetoa kauli kwamba linashitushwa na kiwango cha ufisadi, na sasa limesema “kuna bomu kubwa” zaidi ya lililokwisha kulipuka nchini Kenya.

  Akizungumza katika kipindi kipya cha televisheni kinachotarajiwa kurushwa hewani hivi karibuni, Padri Victus Sichwale, kutoka Baraza la Makanisa Tanzania (CCT), alisema hali nchini imebadilika na rushwa imeanza kuleta mgawanyiko mkubwa katika jamii.

  “Rushwa inakuzwa na wataalamu na wasomi na wengine wanaofuatia. Wapo wema wachache lakini wapo ambao (kwa vitendo vyao) wametengeneza makundi; la wenye nacho na wasio nacho. Kuna hatari ya kulipuka kwa bomu kubwa la walio nacho na wasio nacho. Bomu la hasira kubwa kuliko Kenya ,” alisema Padri Sichwale.

  Kipindi hicho kilichowashirikisha viongozi wa dini, wasomi na wanataaluma, kilihudhuriwa pia na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Utawala Bora, Philip Marmo, ambaye Padri Sichwale alimuomba radhi kabla ya kutoa kauli hiyo. Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) liliwakilishwa na Sheikh Suleiman Gorogosi.

  Washiriki katika kipindi hicho kipya kinachojulikana kwa jina la Changamoto, kilichoendeshwa na mwandishi mkongwe, Jenerali Ulimwengu na kuongozwa na Maria Sarungi, walikuwa wakijadili mada: “Je, rushwa na ufisadi ni tatizo la kimaadili ama kisheria?”

  Awali Padri Sichwale alisema moto wa chuki dhidi ya “walionacho” sasa ni mkubwa na akaonya, “siasa makini haziwezi kupatikana kwa viongozi wetu ambao ni lazima wawalinde wale waliowafikisha walipo.”

  Padri Sichwale alizungumzia pia sakata la ufisadi ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) akisema: “Tunateteana mno na watu tunalindana. Hivi kutatua tatizo mpaka Ballali (Daudi) augue na kwenda nje?”

  Hata hivyo, Padri Sichwale alisema hakuna utaratibu wa kuwatenga ama kuwaonya mafisadi kanisani pamoja na kusema kwamba upo utaratibu usio rasmi wa kuwapa ushauri na maonyo kwa maelezo kwamba wanaoungama huwa hawasemi moja kwa moja walikula rushwa bali huishia kusema, “niliteleza tu.”

  Wakili maarufu, Fatma Karume, yeye aliweka wazi kwamba tatizo la rushwa si la watu wa chini bali huanzia juu ‘kileleni’ na kwamba athari zake ndio hushuka chini.

  Akichangia Sheikh Gorogosi alisema ni lazima viongozi wa dini na viongozi wa familia wakemee rushwa kwa dhati akinukuu vitabu vya dini vinavyoeleza kwamba, “wote ni wachunga na tutaulizwa.”

  Kwa upande wake, Waziri Marmo alisema rushwa mbali ya kuwa tatizo la kimaadili ni tatizo la kisheria na serikali imechukua hatua kadhaa kuimarisha sheria za kupambana na rushwa na sasa makosa ya rushwa yameongezeka kutoka manne hadi 24.

  Marmo aliwashukuru viongozi wa dini na wananchi kwa kuonyesha mwamko katika mapambano dhidi ya rushwa na kuongeza; “Nimefarijika kuona kwamba tunaliona tatizo la rushwa kwa mtazamo mmoja. Umiliki wa mapambano haya ni wetu sote, ikiwa ni serikali, viongozi wa dini na wananchi. Rushwa ni saratani, tusichoke.”

  Katika siku za karibuni viongozi wa dini wamekuwa wazi kukemea rushwa na ufisadi na katika moja ya matoleo ya gazeti la Raia Mwema, Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Methodius Kilaini, alisema kwamba baadhi ya viongozi wa Serikali wanapokea pesa kutoka kwa wawekezaji wa nje, na hivyo kumfanya Rais Jakaya Kikwete awe na wakati mgumu katika kuongoza vita dhidi ya ufisadi wa kimataifa.

  Wiki iliyopita, Rais wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki nchini (TEC), Thadeus Ruwa’ichi alieelezea kukerwa kwake na hali ya mambo nchini hivi sasa, inayoonyesha kukithiri kwa vitendo vya rushwa, ufisadi na uroho wa madaraka, vinavyofanywa na baadhi ya viongozi serikalini.

  Askofu huyo alitoa kauli hiyo mbele ya Waziri Mkuu, Edward Lowassa, aliyekuwa mgeni rasmi katika hafla aliyoihutubua na kuweka wazi kwamba matatizo ya rushwa na ufisadi yanayoikabili nchi kwa sasa yanatokana na baadhi ya viongozi serikalini kuwa wabinafsi na wasiowajibika, hali ambayo alisema inachochea umasikini miongoni mwa jamii na taifa kwa ujumla na kusababisha kaulimbiu ya Maisha bora kwa kila Mtanzania ionekane haina maana yoyote.

  “Nchi yetu inakabiliwa na matatizo ya rushwa na ufisadi, ambayo yanasababishwa na ubinafsi na kutowajibika kwa baadhi ya watu waliopewa majukumu ya kuwatumikia wananchi. Mambo haya machafu yanazidisha umasikini kwa jamii na taifa na kusababisha kaulimbiu ya Maisha Bora kwa kila Mtanzania isiwe na maana,” alisema.
   
 2. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #2
  Jan 30, 2008
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Kuna Taifa moja kubwa zaidi ya miezi sita iliyopita liliwaambia raia wake watafute Makazi karibu na maeneo ya Yatch Club, ili iwe rahisi kuwahamisha ikibidi kwani kuna dalili za kutokea machafuko Tanzania. Kiongozi mmoja alisema, "alama zote za shari zinazotokea katika mataifa ya Afrika zimekwisha kutokea Tanzania tena kwa kiwango cha juu zaidi."
   
 3. M

  Mwendapole Old JF-Expert Member

  #3
  Jan 30, 2008
  Joined: Dec 4, 2006
  Messages: 249
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Mungu apishe mbali!
   
 4. Mwanamalundi

  Mwanamalundi JF-Expert Member

  #4
  Jan 30, 2008
  Joined: Aug 30, 2007
  Messages: 3,034
  Likes Received: 396
  Trophy Points: 180
  ..Tatizo kubwa tulilonalo binadamu ni kwamba yanapozungumzwa haya tunaweka pamba masikioni.

  ...Hata wakati wa nuhu, binadamu hawakuamini kuwa kuna gharika kubwa linainyemelea ardhi. Walikunywa na wakasaza.

  ...Ruth aliambiwa usigeuke nyuma, utageuka uvinza. Yeye akapuuza. Guess what happened.

  ...Leo hii akina makamba wanapoelezwa ukweli wanaukataa, wanaendelea kunywa na kusaza.

  ...Kila mtu anajua ufisadi wa BOT, umefanywa na CCM. Sita anakanusha.

  ...Kwa hivyo, si ajabu machafuko kutokea tanzania. Hata kama sio kwa kupitia mlango wa ukabila, machafuko yanaweza kupitia mlango wa udini.

  ....Mwenye sikio na asikie, mwenye ubongo na afanye tafakuri ya yanayoendelea kenya.

  ...Yako njiani yanakuja. Najua mtabisha. Tusipokuwa makini, hayakwepeki. Ni swala la muda tu. Anatakiwa kupatikana mmoja wa kulianzisha, kama kibaki alivyolianzisha huko kenya.

   
 5. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #5
  Jan 30, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Nchi inaelekea kubaya .Je do we need a new jemadari ?
   
 6. mpenda pombe

  mpenda pombe JF-Expert Member

  #6
  Apr 23, 2017
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 1,188
  Likes Received: 387
  Trophy Points: 180
  Tumeshampata jemedari..
   
 7. Automata

  Automata JF-Expert Member

  #7
  Apr 23, 2017
  Joined: Mar 3, 2015
  Messages: 1,680
  Likes Received: 1,512
  Trophy Points: 280
  Kabisaa
  Na amewaweza sana the so called watoto wa mjini, walio tesa kuanzaia kwenye serikari mpaka kwenye chama
   
Loading...