Kuna Mtu wangu wa karibu anafanya biashara Kenya, yeye ni Mtanzania. Anasema kwa sasa hali siyo shwari kabisa, wanafanya biashara kwa wasi wasi mkubwa wakihofia kuvamiwa na Magenge ya Wahuni, hawa inaonekana Kama ni Magenge ya Wahuni lakini ukweli ni kwamba ni watu walioandaliwa kufanya hayo ambayo yatafanyika.
Nimesikiliza pia Bunge la Kenya, baadhi ya wabunge wakimuunga Mkono Jaguar kwa kauli zake za kuwafukuza wageni wote wanaofanya biashara Kenya.
Wabunge wameonyesha Chuki za wazi wazi kwa Serikali ya Tanzania iliyo Madarakani sasa. Wamekumbusha juu ya Vifaranga vya Kenya vilivyoteketezwa na Moto wakati Vikitaka kuingia Tanzania, wamekumbusha Juu ya Ngombe zao Kukamatwa na kutaifishwa na Tanzania. Pia wameongelea Meneja mmoja mwanamke alitekataliwa na Serikali ya Tanzania kuwa Meneja wa Vodacom.
Wamelalamikia juu ya Maziwa ya kenya kutokuruhusiwa kuingia Tanzania pamoja na Mambo mengi Sana. Na hii inaonekana hata kwa wao kusema wageni wanaofanya biashara Kenya wanatakiwa Kuondoka, hao wengine ni Geresha tu, ila Anayelengwa Haswa Ni Mtanzania.
Sasa ni Vema sana kwa viongozi wetu wanapotuongoza wawe wanatumia Busara sana ktk kutuongoza. Kwa Sababu, maamuzi Yao yasiyo na Busara yatawaingiza Watanzania wenzetu Ktk dhiki kubwa sana pamoja na Hatari kubwa sana. Kuna Mengi Mabaya sana yatawatokea Watanzania wanaoishi Kenya. Viongozi wetu wametujengea uadui mkubwa sana na majirani zetu Wakenya. Mimi sijui wao Wananufaika nini, na uadui Huu. Mshahara wa Dhambi ni Mauti.