Wakati wowote kuanzia sasa Watanzania wataanza kufukuzwa Kenya. Mshahara wa dhambi ni mauti

me najua wananchi wa kawaida upande zote mbili wanapendana tu sana na wala hamna shida yoyote .ila tatizo ni viongozi wetu upande zote mbili.sijui wanamatatizo gani.
 
... haikuwa sahihi kuwachoma wale vifaranga au kupiga mnada wale ng'ombe! Kitendo kile kilionyesha chuki ya waziwazi kabisa dhidi ya Kenya na wakenya; leo wameamua kujibu mapigo. Sijui kwanini busara ilikosenaka kwa kiwango kile. Let's pray for our nation and our people, let's pray for peace and love in East Africa.
Nchi karibu zote duniani huwezi kuingiza mimea au viumbe hai bila kufuata utaratibu wa kuhakiki vitu kama chanjo au wanaingiza mbegu ya aina gani.
Hii huepusha magonjwa kama mafua ya ndege n.k.
Ugonjwa ukiingia na kuuwa watu mnakuja kuitukana na kulaumu serikali haifanyi kazi yake.
Unajuaje kama hao kuku wamefanyiwa genetic hacking maabara hivyo wanaweza kuleta madhara ya kiafya? Au kuuwa kabisa mbegu yetu ya kuku na kutegemea wa njetu kiasi cha kuathiri uchumi wetu?
Zile sheria zipo kwa sababu maalum,sio wajinga walio tunga.
Jaribu kuingiza chakula, ndege, nyama au mnyama yeyote kienyeji nchini UK,Australia, na USA uone itakuwaje. Kuna mambo yanayo husu maisha ya watu hakuna uswahili wa kusema itumike busara.
 
Yeyote anayesababosha au anayeshabikia ugomvi wa aina yoyote Kati ya Kenya na Tanzania.namchukia Kama mjinga na Mpuuzi wa kwanza kuwahi kutokea ktk Nchi hii.
 
Kuna Mtu wangu wa karibu anafanya biashara Kenya, yeye ni Mtanzania. Anasema kwa sasa hali siyo shwari kabisa, wanafanya biashara kwa wasi wasi mkubwa wakihofia kuvamiwa na Magenge ya Wahuni, hawa inaonekana Kama ni Magenge ya Wahuni lakini ukweli ni kwamba ni watu walioandaliwa kufanya hayo ambayo yatafanyika.

Nimesikiliza pia Bunge la Kenya, baadhi ya wabunge wakimuunga Mkono Jaguar kwa kauli zake za kuwafukuza wageni wote wanaofanya biashara Kenya.

Wabunge wameonyesha Chuki za wazi wazi kwa Serikali ya Tanzania iliyo Madarakani sasa. Wamekumbusha juu ya Vifaranga vya Kenya vilivyoteketezwa na Moto wakati Vikitaka kuingia Tanzania, wamekumbusha Juu ya Ngombe zao Kukamatwa na kutaifishwa na Tanzania. Pia wameongelea Meneja mmoja mwanamke alitekataliwa na Serikali ya Tanzania kuwa Meneja wa Vodacom.

Wamelalamikia juu ya Maziwa ya kenya kutokuruhusiwa kuingia Tanzania pamoja na Mambo mengi Sana. Na hii inaonekana hata kwa wao kusema wageni wanaofanya biashara Kenya wanatakiwa Kuondoka, hao wengine ni Geresha tu, ila Anayelengwa Haswa Ni Mtanzania.

Sasa ni Vema sana kwa viongozi wetu wanapotuongoza wawe wanatumia Busara sana ktk kutuongoza. Kwa Sababu, maamuzi Yao yasiyo na Busara yatawaingiza Watanzania wenzetu Ktk dhiki kubwa sana pamoja na Hatari kubwa sana. Kuna Mengi Mabaya sana yatawatokea Watanzania wanaoishi Kenya. Viongozi wetu wametujengea uadui mkubwa sana na majirani zetu Wakenya. Mimi sijui wao Wananufaika nini, na uadui Huu. Mshahara wa Dhambi ni Mauti.
I would like to tell you that.....Kenyan's hawata wafukuza Tanzanian's kwao but in this tulikosea mwanzoni sisi na serikali yetu
 
Nchi karibu zote duniani huwezi kuingiza mimea au viumbe hai bila kufuata utaratibu wa kuhakiki vitu kama wa chanjo au inaingiza mbegu ya aina gani.

Hii huepusha magonjwa kama mafua ya ndege n.k.
Ugonjwa ukiingia na kuuwa watu mnakuja kuitukana na kulaumu serikalibaifanyi kazi yake.

Unajuaje kama hao kuku wamefanyiwa genetic hacking maabara hivyo wanaweza kuleta madhara ya kiafya? Au kuuwa kabisa mbegu yetu ya kuku na kutegemea wa njetu kiasi cha kuathiri uchumi wetu?

Zile sheria zipo kwa sababu maalum,sio wajinga walio tunga.

Jaribu kuingiza chakula, ndege, nyama au mnyama yeyote kiennyeji nchini UK,Australia, na USA uone itakuwaje. Kuna mambo yanayo husu maisha ya watu hakuna uswahili wa kusema itumike busara.
Kwani wakati vinaingizwa kulikuwa na adhari yoyote Africa Mashariki juu ya ugonjwa wowote wa Mafua ya Ndege?. Acha kuleta siasa uchwara kwenye mambo ya hatari wewe!
 
... haikuwa sahihi kuwachoma wale vifaranga au kupiga mnada wale ng'ombe! Kitendo kile kilionyesha chuki ya waziwazi kabisa dhidi ya Kenya na wakenya; leo wameamua kujibu mapigo. Sijui kwanini busara ilikosenaka kwa kiwango kile. Let's pray for our nation and our people, let's pray for peace and love in East Africa.
Kwani hao ng'ombe walifuatwa kenya ama walikutwa kwenye aridhi ya tanzania? Na je ulikuwa unanufaikaje na hao mifugo ikiwa walikuwa wanalipiwa kodi kenya.
 
Inaonekana hujui mambo mengi sana ya biashara juu ya Tanzania na Kenya. Ila nikujulishe tu kwamba, kuna wafanyabiashara kwa mamilioni ambao wananufaika sana na Huu ujirani wetu. Kwa hiyo ujue. Chako choko Zozote zitakazotokea, ni Kuwatia umasikini mamilioni ya Watanzania bila Sababu yoyote ya Msingi, au kwa chuki binafsi tu za viongozi wetu

Tutauza bidhaa DRC
 
Kwa wewe ambaye hujawahi kutoka nje ya Tanzania huwezi kumwelewa mleta mada...

Rais wetu angekuwa mtu wa kutembembea angajua umhumi wa nchi kushirikiana.

Hii ndio gharama ya kuchagua viongozi washamba wanawaza ndani ya mipaka nchi tu...
Mkuu upumbavu wa viongozi wetu ndio upi. Kulinda mipaka yetu na kujali afya za watu wao ama?
 
mkuu nimekuelewa na uko sawa lakini kuchoma viumbe hai Iyo ukatili ndio nimeshindwa kuelewa.si bora wangeirudisha tu aliko toka. kwanin ichomwe?
Nchi karibu zote duniani huwezi kuingiza mimea au viumbe hai bila kufuata utaratibu wa kuhakiki vitu kama wa chanjo au inaingiza mbegu ya aina gani.

Hii huepusha magonjwa kama mafua ya ndege n.k.
Ugonjwa ukiingia na kuuwa watu mnakuja kuitukana na kulaumu serikalibaifanyi kazi yake.

Unajuaje kama hao kuku wamefanyiwa genetic hacking maabara hivyo wanaweza kuleta madhara ya kiafya? Au kuuwa kabisa mbegu yetu ya kuku na kutegemea wa njetu kiasi cha kuathiri uchumi wetu?

Zile sheria zipo kwa sababu maalum,sio wajinga walio tunga.

Jaribu kuingiza chakula, ndege, nyama au mnyama yeyote kiennyeji nchini UK,Australia, na USA uone itakuwaje. Kuna mambo yanayo husu maisha ya watu hakuna uswahili wa kusema itumike busara.
 
Kenya hawawezi kuathirika kwa Chochote bro, sana sana Waalimu wanaofanya kazi Tanzania ndiyo wataathirika na ni wachache sana, Watanzania wanaofanya biashara Kenya ni Mamilioni. Ni Jambo baya sana Litatokea.
Mamilioni umefanya lini sensa. Na wenye nchi yao hawawataki mnalialia nini?
 
... hoja ya mleta mada uliyem-quote ni ku-save maisha ya watanzania walioko Kenya just in case anything happens no matter how may they are. Kwa majibu yako unamaanisha ni sawa tu hata wakiuwawa as long as we have access to kill more Kenyans than they will do for Tanzanians. Mawazo ya ajabu kabisa! Hatuhitaji hata damu ya mtu mmoja imwagike.

Nategemea Kabudi awe kwenye ndege muda huu akielekea Nairobi ku-resolve hii issue before it becomes too late.
Kusolve ili iweje mbona mnawabembeleza sana hao watu.
 
Kuna Mtu wangu wa karibu anafanya biashara Kenya, yeye ni Mtanzania. Anasema kwa sasa hali siyo shwari kabisa, wanafanya biashara kwa wasi wasi mkubwa wakihofia kuvamiwa na Magenge ya Wahuni, hawa inaonekana Kama ni Magenge ya Wahuni lakini ukweli ni kwamba ni watu walioandaliwa kufanya hayo ambayo yatafanyika.

Nimesikiliza pia Bunge la Kenya, baadhi ya wabunge wakimuunga Mkono Jaguar kwa kauli zake za kuwafukuza wageni wote wanaofanya biashara Kenya.

Wabunge wameonyesha Chuki za wazi wazi kwa Serikali ya Tanzania iliyo Madarakani sasa. Wamekumbusha juu ya Vifaranga vya Kenya vilivyoteketezwa na Moto wakati Vikitaka kuingia Tanzania, wamekumbusha Juu ya Ngombe zao Kukamatwa na kutaifishwa na Tanzania. Pia wameongelea Meneja mmoja mwanamke alitekataliwa na Serikali ya Tanzania kuwa Meneja wa Vodacom.

Wamelalamikia juu ya Maziwa ya kenya kutokuruhusiwa kuingia Tanzania pamoja na Mambo mengi Sana. Na hii inaonekana hata kwa wao kusema wageni wanaofanya biashara Kenya wanatakiwa Kuondoka, hao wengine ni Geresha tu, ila Anayelengwa Haswa Ni Mtanzania.

Sasa ni Vema sana kwa viongozi wetu wanapotuongoza wawe wanatumia Busara sana ktk kutuongoza. Kwa Sababu, maamuzi Yao yasiyo na Busara yatawaingiza Watanzania wenzetu Ktk dhiki kubwa sana pamoja na Hatari kubwa sana. Kuna Mengi Mabaya sana yatawatokea Watanzania wanaoishi Kenya. Viongozi wetu wametujengea uadui mkubwa sana na majirani zetu Wakenya. Mimi sijui wao Wananufaika nini, na uadui Huu. Mshahara wa Dhambi ni Mauti.
hujui unachokieleza, serikali ya Tanzania imekuwa na mashauriano mengi sana na serikali ya kenya kuhusu biashara lakini kenya imekuwa ikifunga masikio, TANZANIA KAMWE HAIWEZI KUKAA KIMYA HUKU KUKIWA NA TRADE IMBALANCE!
 
Mkuu upumbavu wa viongozi wetu ndio upi. Kulinda mipaka yetu na kujali afya za watu wao ama?
Nimezungumzia kuhusu lugha ya Diplomasia....hivi unafikiiri leo watanzania walioko Kenya wakifurushwa ni mitaji kiasi gani itapotezwa na watu kurudi kwenye lindi la umaskini...

Kwa hiki kinachoendele usishangae Watanzania wengi walioko Kenya wameanza kufungasha chochote kitakachopatikana...

Usiombe uwe unafanya biashara kwenye nchi za watu halafu itokee hali hiyo ....maana utaondoka wewe kama wewe.
 
Wajaribu ndo watajua Tanzania Ndo Baba Wa East Africa
Nilitaka kuandika hivyo hivyo mkuu. Tanzania inaweza kuishi vizuri kabisa bila uwepo wa Kenya, Uganda, Rwanda hata na Burundi but for sure Kenya, Uganda hazina ubavu wa kuishi vizuri bila Tanzania. Wajaribu halafu labda na huyu wa kwetu awaondoe Wakenya wote Tanzania na pia Tanzania iache kununua chochote from Kenya the tuone nani ataomba POO. We all know the Samuel Sitta Saga wakati ule akiwa waziri wa mambo ya EAC, Kenya ilijifanyaga kuzuia magari yetu kwenda kuchukua wageni/watalii kwenye uwanja wao wa ndege, JK akiwa rais wa wakati huo, alipunguza idadi ya safariza ndege za KQ kutua uwanja wetu wa Dar from 42 times per week hadi 14 times per week, nakumbuka Uhuru aliomba POO tena wakiwa Zimbabwe. Naitamani sana hi kiti itokee but asiuawe mtu na huyu wetu awapelekee majibu ya hili Saga
 
... hoja ya mleta mada uliyem-quote ni ku-save maisha ya watanzania walioko Kenya just in case anything happens no matter how may they are. Kwa majibu yako unamaanisha ni sawa tu hata wakiuwawa as long as we have access to kill more Kenyans than they will do for Tanzanians. Mawazo ya ajabu kabisa! Hatuhitaji hata damu ya mtu mmoja imwagike.

Nategemea Kabudi awe kwenye ndege muda huu akielekea Nairobi ku-resolve hii issue before it becomes too late.
Hizi ni political games. Watu wanataka kutoka kisiasa. Tukianza kuumizana, nani atakayenufaika?
Tanzania hakuna mtu aliyesema wakenya washambuliwe au kuondolewa kwa lazima
 
Ila Kenya kwa miaka mingi sana wamekuwa wakiizadharau tz, mfn nilifanya kampun moja ilianzia Tz na pia ipo kenya, sales team ya kenya ilipokuja tz moja ya speech yao walisema tz ni pig team na wao ni lion team na kusema sisi ni legelege tulimtukana sana na kidog apigwe,Wakenya waache dharau na kujifanya wao wako juu sote tunategemeana
 
Back
Top Bottom