Wakati wowote kuanzia sasa, viongozi wa nchi fulani wanaweza kuwekea vikwazo vya kusafiri katika nchi za Ulaya na Marekani kama sio kunyimwa misaada

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
38,709
2,000
Kwa yanayoendelea katika Taifa fulani,yanatoa kila sababu kwa Bwana wakubwa wa huu Ulimwengu kuingilia kati na kuchukua hatua.Hatu hizo zinaweza kuwa ni pamoja na kuwafungia viongozi wa nchi hiyo kutosafiri kwenda Marekani na baadhi ya nchi za ulaya au nchi wahisani kusitisha misaada na mikopo kwa nchi hiyo(jina kapuni).

Kadri siku zinavyokwenda,viongozi wa Taifa hilo wanaonekana kufanya mambo yasiyoendana na ustaarabu wa dunia ya leo hivyo sidhani kama watavumiliwa maana leo utasikia hili, kesho utasikia lile,mtondogoo lingine mradi ni bandika bandua.

Anyway,labda wamenyimwa maarifa na kutiwa upofu ili wao na chama chao waanguke.

Time will tell.
 

Kawe Alumni

JF-Expert Member
Mar 20, 2019
8,370
2,000
Tuliwahi kusema USA ni Nchi ya wajinga

Chukulia mfano Venezuela
USA alijitoa ufahamu wakamtambua mpinzani km kiongozi wa nchi wakamjaza ujinga hadi akaisaliti Nchi yake

Lkn wakashindwa kumtoa madarakani Rais

Leo hii Trump anaomba mazungumzo na maduro Rais wa Venezuela yule waliyekuwa wakimvizia usiku na mchana kumtoa madarakani

Nchi za Africa zijitambue ziachane na usa zishirikiane na Urusi, China, Brazil, Iran na North korea hawa wajinga wa USA wampoteze ushawishi sasa hivi duniani

Wameiangamiza libya imebaki gofu bado wanaleta ujinga wao tena

Zama za USA zimeisha kama hadi Iran imemweka kati atamtisha nani?

Zimbabwe amewekewa vikwazo miaka nenda rudi ila wanadunda tu, USA akajifie mbele kule zama zake zimeisha
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom