Wakati watanzania wengi wakiwa wanadai katiba watusisahau kudai tume huru ya uchaguzi kabla 2015 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wakati watanzania wengi wakiwa wanadai katiba watusisahau kudai tume huru ya uchaguzi kabla 2015

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by HISIA KALI, Apr 15, 2011.

 1. HISIA KALI

  HISIA KALI JF-Expert Member

  #1
  Apr 15, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 694
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kutokana na mwenendo wa mswaada wa kubadilisha katiba naona kuna kamchezo CCM na serikali yake wanacheza kuwaadaa watanzania kuhusu katiba mpya. Mimi naona CCM na serikali yake haina nia ya kuwa na katiba mpya Tanzania.

  Kuna uwezekano mkubwa sana kuwa Mswaada uliondolewa leo bungeni ulitayarishwa kwa jinsi ulivyo kwa makusudi kabisa na Serikali ya CCM wakijui wananchi wengi wataupinga na baadaye watauondowa bungeni kwa kizingizio cha makerebisho. Na hayo marekebisho yatachukua muda mrefu kufanyika. Huu ni ujanja wa kuchelewesha katiba mpya.

  Kimsingi hoja ya katiba mpya sio ya CCM na serikali yake, na katiba mpya mara nyingi huwa haina faida sana kwa watu wanaotawala kwa tumia katiba iliyopo. Kwa nini waweke katiba inayowabana wao wakati wanatawala sasa sheria zilizopo?

  Cha msingi mimi ninapenda kutumia hili jukwaa la JF kushauri vyama vya upinzani (haswa CDM) na wanaharakati wengine kuanza kudai kwa nguvu kubwa tume huru ya uchaguzi sasa. Ninasema hivi kwa sababu kuna kila dalili kuwa Tanzania haitakuwa na katiba mpya kabla ya uchaguzi mkuu wa 2015. Hivyo basi wakati bado tunaendelea kushinikiza serikali kuhusu katiba mpya lazima pia tudai kwa nguvu zote tume huru ya uchaguzi kabla ya mwaka 2015.

  Ningefurahi kama wadau wa demokrasia kama UDASA na wengine wangeitisha makongomano ya kujadili na kudai tume huru ya uchaguzi.

  Vyama vya siasa vya upinzani vifanye mikutano na maandamano nchi nzima sasa kudai tume huru ya uchaguzi.

  Tukumbuke katika uchaguzi uliopita kuna kila dalili kuwa uchaguzi ule ulikuwa na kasoro za hata kubadilisha ushindi wa vyama vya upinzani kwa faida ya CCM. Hii yote ilitokana na tume tulionayo sasa. Ni vyema tukianza sasa kudai tume huru ya uchaguzi kwa kuweka pressure kubwa kwa serikali.

  Kimsingi hakuna haja ya kwenda kwenye uchaguzi wakati tunajua fika kuwa tume ya uchaguzi sio huru.Timu ya mpira haiwezi kwenda kucheza mechi wakati wanajua kuwa refa ameletwa na timu mpinzani na pia kuishi kwake kunategemea fadhila za hiyo timu pinzani. Katika hali kama hii ni lazima refa atapendelea tu ile timu iliyomleta.
   
Loading...