Wakati Watanzania wakikosa madawa na tiba, Faru Fausta anatumia Bil 1 kama gharama za matunzo. Je anaingiza kiasi gani?

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
Mamlaka Hifadhi Ya Ngorongoro (NCAA) imeanza kuzalisha majani aina ya Lusuni, ambayo ni chakula cha Faru Fausta Ili kupunguza gharama za kumtunza faru huyo. Nyasi hizo kwa sasa huagiziwa nchini Kenya na hutumia kiasi cha shilingi milioni 5 kwa kwa mabandali matano kila zinapoagizwa. Faru huyo mzee zaidi duniani mwenye miaka 54 anakadiriwa kula bandali 250 kwa miezi minne ambapo gharama yake ni kama shilingi milioni 250 za kitanzania.

Faru huyu ajuza anahifadhiwa na Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) chini ya uangalizi maalumu ili kumlinda dhidi ya majangili na wanyama wengine wa mwitu. Faru huyo amabye ni chongo baada ya kutobolewa jicho lake moja na watu wasiojulikana, ni kivutio Kizuri kwa watalii, kwani ndiye faru mzee zaidi duniani akiwa na umri wa miaka 54 akifuatiwa na faru Macite mwenye umri wa miaka 48 anayeishi Audubon Zoo huko New Orleans, nchini Marekani.

Mamlaka ya Ngorongoro imetenga eneo kwa ajili ya kuzalisha nyasi hizo aina ya Lusini ambazo ni chakula cha Faru Fausta, na wanategemea ziwe tayari kuvunwa baada ya miezi 7. Meneja Idara ya Malisho na Usimamizi wa Wanyama NCAA, Hillary Mushi amesema mamlaka imeandaa shamba lenye ukubwa wa ekari mbili na imepanda mbege za lusini na yataanza kuvunwa ndani ya miezi saba kutoka sasa.

Gharama za kumtunza Faru huyu kikongwe zimekuwa zikitajwa kuwa kubwa sana kutokana na hali yake ya kiafya na kiusalama. April 7 mwaka huu mamlaka hiyo ilieleza kutumia zaidi ya shilingi Milioni 43 kwa ajili ya kumjengea Fausta banda maalumu la kumhifadhi.

Fausta ambaye anatunzwa peke yake tofauti na Faru wengine anatajwa kutumia mamilioni ya fedha kwa matibabu kutokana na afya yake kiafya kutokuwa ya kuridhisha. Lakini pia ana ulinzi mkali wa askari wa wanyama pori wenye silaha amabao humlinda kila siku kwa saa 24.

Mwezi April pia mamlaka hiyo ilieleza kutumia Shilingi milioni 64 kwa mwezi kama gharama za kumtunza Faru huyo ambazo ni makadirio ya shilingi milioni 768 kwa mwaka.

Hii ni kusema kwamba gharama za kumtunza Fausta (Chakula, matibabu, ulinzi etc) kwa mwaka mmoja zinaweza kukadiriwa kufikia Shilingi Bilioni moja.

Nini maoni yako??
 
huku dogo janja kule nyalandu huku mange kule fausta tushike lipi jamani
 
Back
Top Bottom