Wakati Watanzania ‘ tukijidanganya ‘ kwamba Wachezaji wetu wa Serengeti Boys ni wazuri ‘ Mawakala ‘ bado hawajaona anayefaa.

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,462
108,617
Kila Siku huwa navikosoa mno kama siyo sana Vyombo vya Habari nchini Tanzania na hasa hivi vya Michezo kwa tabia yake ya Kupenda Kusifia vitu ‘ Kipuuzi ‘ huku vikiwajaza Watu ‘ Ujinga ‘ kinyume hata na uhalisia wake hali ambayo baadae huja kuharibu kabisa.

Wakati Watanzania nasi pia tukiingizwa katika ‘ Upuuzi ‘ huo huo wa hawa Wanahabari wa Michezo jana nilikaa na Mawakala wakubwa tu ambapo hadi mpira ule unamaliza hawakuona Mchezaji yoyote mzuri kutoka Serengeti Boys. Walichosema tu ni kwamba wengi wao wanajitahidi tu Kucheza mpira ila bado hawaujui Mpira.

Kuna Wakala Mmoja ndiyo alinimaliza kabisa na Kukubali kuwa kweli ' Wazungu ' huwa hawabahatishi na hawana ' Unafiki ' katika maelezo yao pale alipomchambua Mchezaji Mshambuliaji Kelvin John ambaye kwa Watanzania na hivyo Vyombo vya Habari vya Tanzania ' vinamtukuza ' kuliko hata Messi na Ronaldo kuwa hajui Mpira na anacheza mpira wa Jukwaani na siyo wa Kiufundi hali ambayo itamuwia vigumu kwa Yeye kupata Klabu kubwa huko Ng'ambo ( Ulaya )

Na ili muone kwamba hawa Mawakala hasa wa Kizungu huwa hawana ' Uswahili Uswahili ' wetu kama tulionao wakati Watanzania wengi tokea jana ' tukimlaumu ' Golikipa wa Serengeti Boys Mwinyi Yahaya kuwa ' alituchomesha ' hadi Kufungwa vile Mawakala wawili walisema kuwa kwa uzuri wa Timu ya Nigeria ulivyo kama kuna Mchezaji ambaye Kwao Wao jana alifanya vyema na alijitahidi basi alikuwa ni Golikipa huyo na wakasema kuwa ' Kiufundi ' ana Vitu vichache sana vya Kuongezewa ila huko mbele wakamtabiria kuwa atakuja kuwa Golikipa mzuri mno hapa Tanzania.

Baada ya Kauli hizi na Mitazamo hii ya hawa Mawakala wa Kizungu sasa nimeamini kuwa Watanzania wengi ( ukimuondoa GENTAMYCINE ANTIBIOUTIQUE ) ni Mashabiki tu wa Mpira ila siyo Watu wa Mpira. Na kwa tabia hii ya Vyombo vya Habari vya Tanzania kupenda Kusifia hata ' Upuuzi ' au vitu ambavyo sivyo vya Kiuhalisia Tanzania itaendelea kubaki hapa hapa japo mwaka huu Taifa Stars ' tumebahatisha ' tu Kufuzu AFCON nchini Misri baada ya Waganda kutuonea huruma na kuweka Ujirani mwema ila nina uhakika kama Uganda wangeamua ' Kukaza ' basi kama kawaida Watanzania AFCON 2019 tungeisikia tu katika ' Bomba ' huku tukiendelea na zile tabia zetu za Kuchagua Timu za Kushangilia na Mataifa ya Wenzetu.

Nawasilisha.
 
mawakala uchwara hao kwamba hata hawakumuona kindoki mdogo.

kuna dogo kelvini na Ngoda wale vijna wanajitahidi, sema mikia washatia gundu hadi kwa madogo ko nimwendo wa kuchakazwa tu
 
Simba SC hapa imeingiaje? Usisababishe ' nikakuchenjia ' na kukujibu hovyo hadi ukajuta sawa? Uzi unaongelea Serengeti Boys Wewe unakuja na Kuizungumzia Simba SC kama hapa hutafuti matatizo ya ' Kilazima ' na Mimi utakuwa unataka nini? Nasisitiza tena Kwako kuwa hao ' Mawakala ' kwa Mchezo wa jana hawajamuona Mchezaji yoyote anayefaa wa Tanzania ( Serengeti Boys ) na huyo Mshambuliaji Kelvin wamemchambua vizuri sana kuwa hajui Mpira bali anajitahidi tu Kucheza Mpira.
 
Yule kipa ni hamna kitu, hata ukiitisha kombaini tu ya michezo sekondari Dsm tu utapata makipa hata zaidi ya watano wenye uwezo zaidi yake. Inashangaza eti ndio kipa wa Tz nzima, mimi naamini yule kipa ana ndugu TFF au benchi la ufundi anayembeba maana kwenye mechi zote hata yale mashindano ya juzi ya Rwanda alikuwa anaonekana ni kimeo ila bado yupo tu.

Mwisho, hata kocha wa Serengeti boys amekiri kipa ni tatizo la wazi ila bado naamini Tz tunaingia semi final na World Cup. Uganda na Angola wote wanafungika na hakuna yoyote mwenye uwezo wa kumfunga Nigeria kati yao.
 
Yule dogo Kelvin yupo vizuri sana, amefunga goli na ametengeneza goli moja pia, akitunzwa vyema atakuja kuwa msaada mkubwa baadaye.
 
Simba SC hapa imeingiaje? Usisababishe ' nikakuchenjia ' na kukujibu hovyo hadi ukajuta sawa? Uzi unaongelea Serengeti Boys Wewe unakuja na Kuizungumzia Simba SC kama hapa hutafuti matatizo ya ' Kilazima ' na Mimi utakuwa unataka nini? Nasisitiza tena Kwako kuwa hao ' Mawakala ' kwa Mchezo wa jana hawajamuona Mchezaji yoyote anayefaa wa Tanzania ( Serengeti Boys ) na huyo Mshambuliaji Kelvin wamemchambua vizuri sana kuwa hajui Mpira bali anajitahidi tu Kucheza Mpira.
Nilikuwa nazungumzia gundu lililoletwa na mikia bro. kwa kuchakazwa ndo madogo nao wanapita humo humo
 
Yule kipa ni hamna kitu, hata ukiitisha kombaini tu ya michezo sekondari Dsm tu utapata makipa hata zaidi ya watano wenye uwezo zaidi yake. Inashangaza eti ndio kipa wa Tz nzima, mimi naamini yule kipa ana ndugu TFF au benchi la ufundi anayembeba maana kwenye mechi zote hata yale mashindano ya juzi ya Rwanda alikuwa anaonekana ni kimeo ila bado yupo tu.

Mwisho, hata kocha wa Serengeti boys amekiri kipa ni tatizo la wazi ila bado naamini Tz tunaingia semi final na World Cup. Uganda na Angola wote wanafungika na hakuna yoyote mwenye uwezo wa kumfunga Nigeria kati yao.
mechi ya angola na uganda nimeiona kusema ukweli hatuna uwezo wa kumfunga si angola wala uganda na nigeria kwa angola anaweza kalishwa. kwenye hili kundi nawapa nafasi nigeria na angola sisi tutakuwa wa mwisho kwa point 1 (draw na uganda) ama tuchakazwe mazima kama kaka zetu mikia fc
 
Kila mtu na Jicho Lake.. Sir Ferguson alimkataa Zidane akiwa Marseille. . Wenger alitaka Zlatan afanye trial kwanza Arsenal. . Zlatan akakataa kufanya hivyo.. . dunia yote inajuwa kilichofuata.. Hao maagent uchwara sio kipimo. .. Nigeria wenyewe hawana natural striker kama Kevin
 
Kwahiyo kwa Lugha nyepesi na iliyo nyoofu kabisa hapa unataka kusema nini labda?
 
Kevin anaweza. . Kwa uzoefu wangu wakuona tournament za watoto Ulaya . . kevin anaweza kwenda Academy yoyote Ulaya na wakamchukua. Umesema anacheza na jukwaa . Ana miaka 16 tu. . Makocha wanauwezo wa kumtengeza ndani ya miaka 3..kwangu Kevin ni zaidi ya Samatta. . . Sky is the limit
 
Kwahiyo umeshakubaliana na hao Mawakala ' Wataalam ' kabisa wa Kizungu kuwa hajui Mpira bali anajitahidi tu Kucheza Mpira?
 
Tusiwavunje moyo watoto, bado wana nafasi ya kuwa wachezaji wazuri siku za usoni

Sent using Jamii Forums mobile app

Sijawavunja moyo ila nimewasilisha tu ukweli wa Mawakala huwa hawa tunaowasifia hawajui Mpira kama ambavyo Media za Tanzania zinavyohangaika na kujitahidi Kutuaminisha hivyo. Hakuna Watu ninaowakubali na kuwaamini hasa kwa kuwa Jicho la Kuchunguza, Kutathimi, Kuchambua na kusema Ukweli na Uwazi wote kama Wazungu Mkuu na katika 100% ukiona Mzungu amekosea ni kwa 5% tu ila zote 95% huwa wako sahihi.
 
Kwahiyo umeshakubaliana na hao Mawakala ' Wataalam ' kabisa wa Kizungu kuwa hajui Mpira bali anajitahidi tu Kucheza Mpira?
Huyo mtoto bado yuko mafunzoni. . Akigraduate ndio useme mengine.. Ajax, PSG, Barcelona mmoja wao watamchukua Kevin. . Nitarudi kukumbusha
 
Hizo Ajax, PSG na Barcelona ni za hapa hapa Tandale Dar es Salaam au ni zile za Ulaya ambazo nazijua Mimi kuwa hazina utaratibu wa kuchukua Wachezaji ' Takataka ' kutoka baadhi ya nchi ambazo zinapambana Kuendelea ambazo nyingi ziko katika Jangwa la Kusini mwa Sahara?
 
Hivi kwa nini hakuna matangazo barabarani au hata wana habari na wengi hawaipaishi hili jambo? Ukimya kweli matangazo yapo wapi.. hata watalii waone.. haya yakipita kwa amani hawajui kwamba ni sifa kwa nchi na watalii kutaka kuja kwa wingi mbeleni. 'Word of mouth' ina nguvu sanaaaa pia.. wajiongeze wahusika
 
Kila Siku huwa navikosoa mno kama siyo sana Vyombo vya Habari nchini Tanzania na hasa hivi vya Michezo kwa tabia yake ya Kupenda Kusifia vitu ‘ Kipuuzi ‘ huku vikiwajaza Watu ‘ Ujinga ‘ kinyume hata na uhalisia wake hali ambayo baadae huja kuharibu kabisa.

Wakati Watanzania nasi pia tukiingizwa katika ‘ Upuuzi ‘ huo huo wa hawa Wanahabari wa Michezo jana nilikaa na Mawakala wakubwa tu ambapo hadi mpira ule unamaliza hawakuona Mchezaji yoyote mzuri kutoka Serengeti Boys. Walichosema tu ni kwamba wengi wao wanajitahidi tu Kucheza mpira ila bado hawaujui Mpira.

Kuna Wakala Mmoja ndiyo alinimaliza kabisa na Kukubali kuwa kweli ' Wazungu ' huwa hawabahatishi na hawana ' Unafiki ' katika maelezo yao pale alipomchambua Mchezaji Mshambuliaji Kelvin John ambaye kwa Watanzania na hivyo Vyombo vya Habari vya Tanzania ' vinamtukuza ' kuliko hata Messi na Ronaldo kuwa hajui Mpira na anacheza mpira wa Jukwaani na siyo wa Kiufundi hali ambayo itamuwia vigumu kwa Yeye kupata Klabu kubwa huko Ng'ambo ( Ulaya )

Na ili muone kwamba hawa Mawakala hasa wa Kizungu huwa hawana ' Uswahili Uswahili ' wetu kama tulionao wakati Watanzania wengi tokea jana ' tukimlaumu ' Golikipa wa Serengeti Boys Mwinyi Yahaya kuwa ' alituchomesha ' hadi Kufungwa vile Mawakala wawili walisema kuwa kwa uzuri wa Timu ya Nigeria ulivyo kama kuna Mchezaji ambaye Kwao Wao jana alifanya vyema na alijitahidi basi alikuwa ni Golikipa huyo na wakasema kuwa ' Kiufundi ' ana Vitu vichache sana vya Kuongezewa ila huko mbele wakamtabiria kuwa atakuja kuwa Golikipa mzuri mno hapa Tanzania.

Baada ya Kauli hizi na Mitazamo hii ya hawa Mawakala wa Kizungu sasa nimeamini kuwa Watanzania wengi ( ukimuondoa GENTAMYCINE ANTIBIOUTIQUE ) ni Mashabiki tu wa Mpira ila siyo Watu wa Mpira. Na kwa tabia hii ya Vyombo vya Habari vya Tanzania kupenda Kusifia hata ' Upuuzi ' au vitu ambavyo sivyo vya Kiuhalisia Tanzania itaendelea kubaki hapa hapa japo mwaka huu Taifa Stars ' tumebahatisha ' tu Kufuzu AFCON nchini Misri baada ya Waganda kutuonea huruma na kuweka Ujirani mwema ila nina uhakika kama Uganda wangeamua ' Kukaza ' basi kama kawaida Watanzania AFCON 2019 tungeisikia tu katika ' Bomba ' huku tukiendelea na zile tabia zetu za Kuchagua Timu za Kushangilia na Mataifa ya Wenzetu.

Nawasilisha.
Leo mzee nakukubali kwenye hili!!! Vyombo vya habari vinaua soka letu na michezo kwa ujumla!!!

Tunaweza kuwalaumu ama tusiwalaumu kwani wapo kibiashara zaidi. Ila mimi nawalaumu kwa kutumia ujinga wetu kuturisha matango pori badala ya kusaidia kututoa kwenye lindi la ujinga kama sehemu ya majukumu yao !!!
 
yaan hao wazungu unaowaona sio wanafiki ndio walimwambia Dimaria na deepay hawafai kucheza man utd na hao hao ndio walimfukuza debruine, roben na mata pale chelsea eti hawana uwezo.. lakini pia ndio hao hao walimnunua sanchez kwa pesa nyingi mwisho wa siku anasugua bench.... KUNA WAZUNGU NI WEUPE KUANZIA NGOZI HADI AKILI...believe me..

Sent usingJamii Forums mobile app
 
Mbona wote uliowataja wametemwa na wazungu na wakaenda kuaminiwa na wazungu? Au kuna yeyote alikuja kucheza Africa!!!!

WAPO WANANIELEWA MPAKA HAWAJIELEWI
 
Back
Top Bottom