SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 5,104
- 7,857
Mimi ni mtu ninayeamini kuwa changamoto kubwa katika sanaa ya Bongo inaanzia kwa wasanii wenyewe ingawa serikali inachangia sana kwa kiwango kikubwa kuwadumaza, na hii sidhani kama wanasiasa wnafanya kwa bahati mbaya.
Hivi karibuni niliwahi kuleta uzi hapa nikimkosoa Diamond kwa mambo kadhaa, kuna watu wakanishambulia sana kuwa nina chuki binafsi. Ukweli mimi sipo kwenye 'team' yoyote, I just like good entertainment haijalishi ni nani. Ningependa niwaone Diamond, Ali Kiba, Darassa, Harmonize na wengine wanapiga shows MSG na Las Vegas. Ule uzi niliuleta ukiwa nusu ni utani lakini kuna mawazo ya msingi niliyotaka kuwayasilisha. Watu waliuchukulia too serious!
Kuna changamoto kubwa sana katika kushindana na wasanii wa Nigeria katika muziki. Ukiacha suala la uwekezaji mkubwa waliyofanya kwenye industry yao tofauti na sisi, lakini kuna suala la ukaribu kufika Marekani kutoka Nigeria (kwa maana hiyo gharama ziko chini). Wakati sisi tunakwenda Afrika Kusini kurekodi audio na video, wao wanakwenda Marekani.
Pia Sina uhakika mfumo wao wa usambazaji uko vizuri kiasi gani ila ninachojua kuna Wanigeria wengi kwenye vyombo mbalimbali vya entertainment na wanasaidiana kweli kuanzia fursa za shows zinapojitokeza, kutengeneza programs wanazoziita za muziki wa Afrika lakini kiukweli wanapiga za kwao tu, nk. Hili nakumbuka kumsikia Vanessa Mdee akiliongelea. Kuna kazi kubwa ya kufanya kwenye hili suala.
Pia binafsi sidhani kama ni mbinu nzuri kwa wasanii wetu wakubwa kujaribu kufanya kazi na wasanii wakubwa wa Marekani kama Rick Ross, Omarion. Ukiacha faida za kinyumbani za kufanya hivyo (kupata deals za Vodacom, Tigo na ASAS Dairies), sioni hili likiwasaidia kimauzo huko nje wala kuongeza kujulikana kwao. Tusiwaige kina Davido na Wiz Kid, wao wana mikakati yao, na sisi inabidi tuweke ya kwetu.
Kwa maoni yangu, wasanii wetu wangejikita kufanya kazi na underground artists wa nje (kuna ambao wana fans kibao online ila hawasikiki kwenye mainstream media na wanafanya shows nyingi). Nakumbuka Sugu aliwahi kufanya collabo na wasanii fulani underground wa Marekani. Hii kitu inabidi iwe endelevu ili iwe na matokeo chanya. Mdogo mdogo tukifanya hivyo, kwanza itawajengea wasanii wetu ufahamu fulani, network, ubunifu na asikwambie mtu hot tracks zinatengenezwa kwenye studio za kitaa. Wasanii wengi wakubwa wananunua na kuiba nyimbo na styles zilizotengenezwa na wasanii wa underground. Huko ndiyo kwenye ubunifu hasa na watu wenye njaa.
Kingine kujikita kutafuta fursa za kufanya shows kwenye festivals mbalimbali duniani. Hii ni fursa kubwa sana ambayo wasanii wangekaa chini wakaifanyia kazi. Inabidi kutengeneza Swahili Movement itakayoanzia chini chini isambae taratibu halafu ifike siku sisi ndiyo tuwe watu waku set trends kwenye muziki wa Afrika badala ya kuwa watu wa kuiga tu.
La mwisho, hakuna haja ya kuiga umarekani si katika uvaaji wala uimbaji. Inabidi tuwe na utambulisho wetu. Sishauri turudi kuvaa majani na kucheza miguu peku kama kina Mrisho Mpoto, ila tunaweza kuja na vitu fulani tofauti vitakavyotutofautisha na wanigeria na tamaduni zingine. Tuna makabila zaidi ya 100, kuna madini mengi sana ya sauti, beats, rhythm, choruses, uchezaji hadi fashion ambayo bado kabisa hatujayachimbua.
Tujadiliane kwa ustaarabu, leo sijamshambulia mtu.