Wakati wapigania uhuru na ukombozi wa Afrika waliwapinga wazungu, wapinzani wa Tanzania wanasema eti tusiwabeze wazungu maana wanatulisha

ZALEMDA

JF-Expert Member
Aug 15, 2017
792
1,000
Hii ndiyo tofauti ya Mwanafrica Mzalendo. Wapigania uhuru babu zetu hawakuwatetea wazungu, bali waliwasema hadharani na hata kuuawa ndipo tukapatata uhuru ambao sasa tunautumia kuongea hovyo, kutetea mimba za utotoni, kutetea wezi wa rasilimali zetu, kutetea wanaume koana wao kwa wao Nk.

Wakati babu zetu wakiuawa kwa kupigania uhuru wanakuona haya Kumkea mzungu mkoloni ambaye kiuhalisia alikuja kututawawala ili aibe Mali zetu. Wapinzania hasa CHADEMA na ACT Wazalendo wanasema eti tusiwabeze wazungu maana wanatulisha!! Wanasahau kuwa hicho wanachotulisha ni Matokeo ya Mali zetu walizotupora kwa kuwakata vichwa babu zetu walipojaribu kuwazuia wasiibe Mali zetu. Kwa hili la kuwatetea wazungu limenishangaza sana.Hapo ndipo ninapoamini kuwa kuna watu wametumwa kuja kutuvuruga.

Mtanzania mwenzangu usidanganyike mwaka huu. Ukikosea kuchagua utarudishwa nchi ya utumwani ili uwanyenyekea wazungu ambao watakulazimisha ushoga,kutoa mimba,madawa ya kulevya nk.

Hatudanganyiki
 

minyoo

JF-Expert Member
May 25, 2013
19,590
2,000
Bora Mzungu mara 10000 kuliko Mkoloni mweusi tokea chato mpenda Kesi kesi kuwabambikia kesi kuwapiga risasi wapinzani, hawa makaburu weusi ni balaa kuliko wakoloni wa aina zote Duniani.

Mkoloni kachukua pesa za viwanda kwenda kujenga Chato Airport kienyeji pasipo idhini ya bunge na hakuna Ndege inatua zaidi ya Ndege yake pekee.

Mkoloni mweusi anatumia uchonganishi kuongoza Nchi kwa njia za kishetani amechukua pesa ya walipa kodi kumlipa Shibuda, Lipumba na jaji kaijage waandae mapingamizi ni matumizi mabaya ya pesa za viwanda na umma, bora Mzungu kuliko Mkoloni mweusi .
 

Aridhi tukufu

Member
Aug 10, 2020
24
45
Tuanze na hiyo simu unayotumia uliipata toka Kiwanda Cha kushonea ndala kwako siyo? Huna uwezo ukitaka kujua jaribu kukohoa au fanya Kama unajikuna tuone Kama hayajatokea ya Ghafafi kunyofolewa darajan.
 

Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
9,154
2,000
Acha kuonyesha ujinga wewe, hudanganyiki na nani? Tanzania hatujawahi kupinga wazungu kwa kuwa huo ni ubaguzi ambao sisi tuliupinga. Hatukuwa na ugomvi na wazungu wa South Afrika, tulikuwa na ugomvi na serikali ya Makaburu ya South Africa iliyokuwa ya kibaguzi.

Kwa filosofia ya Nyerere, hata kama serikali ya Afrika Kusini ingekuwa ni ya waafrika wachache wanaowabagua wazungu sisi tungewasaidia wazungu.

Kwani tulipowaunga mkono Biafra dhidi ya ukandamizaji wa serikali ya Nigeria ilikuwa serikali ya Nigeria ni ya Wazungu?

Kama tuliwapinga wazungu, ilikuwaje tulishirikiana na watu kama Joe Slovo ambao walikuwa wazungu katika ANC? Na ilikuwaje tulipigana kwa kushirikiana na Cuba na Urusi kukomboa nchi za kusini ambao ni wazungu?

Kuna watu mnaongea ujinga hadi mnakera. JF sio lazima upost thread. Unaweza kuwa mtu wa kusoma tu, sio kuleta hoja za vitu usivyoelewa ili mradi unataka kuridhisha ashiki zako za ushabiki wa siasa dhidi ya wapinzani. Ongea sera tuelewe sio huu upuuzi.
1598285125700.png
 

mliberali

JF-Expert Member
Jul 13, 2012
8,306
2,000
Hii ndiyo tofauti ya mwanafrica mzalendo.wapigania uhuru babu zetu hawakuwatetea wazungu,bali waliwasema hadharani na hata kuuawa ndipo tukapatata uhuru ambao sasa tunautumia kuongea hovyo,kutetea mimba za utotoni,kutetea wezi wa rasilimali zetu,kutetea wanaume koana wao kwa wao Nk...
Mabeberu wametukopesha hela ya kujengea sgr na stiglers
 

andjul

JF-Expert Member
Dec 14, 2013
17,420
2,000
Hao babu zako walio pigania uhuru na rasilimali kutokuibiwa ndio waliwatuma muingie mikataba ya hovyo na Wazungu baada ya uhuru?
TANU iliyopigania uhuru ndio hii hii CCM iliyo madarakani na viongozi wake ndio hao hao walio sababisha hayo yote unayo yalalamikia kwa upinzani.
 

imhotep

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
24,655
2,000
Bila mzungu kutunyooshea mambo tungebaki tunarogana mpaka karne ya mwisho
 

Intel5500

JF-Expert Member
Oct 22, 2019
743
1,000
Tuanze na hiyo simu unayotumia uliipata toka Kiwanda Cha kushonea ndala kwako siyo? Huna uwezo ukitaka kujua jaribu kukohoa au fanya Kama unajikuna tuone Kama hayajatokea ya Ghafafi kunyofolewa darajan.
Hajaipata bali kanunua..... tofautisha kununua na kupata.....ukinunua ni mali yako.....
 

Jankoliko

JF-Expert Member
Nov 26, 2018
451
500
Hii ndiyo tofauti ya mwanafrica mzalendo.wapigania uhuru babu zetu hawakuwatetea wazungu,bali waliwasema hadharani na hata kuuawa ndipo tukapatata uhuru ambao sasa tunautumia kuongea hovyo,kutetea mimba za utotoni,kutetea wezi wa rasilimali zetu,kutetea wanaume koana wao kwa wao Nk...
Kama muafrika mzalendo ni yule anae sema/kemea maovu hadharani, je nini kimewatokea wanaokemea maovu ya serikali yao wakiwemo hao CDM, ACT wazalendo na wengineo?

Ni haki wapinzani kuuawa/kuteswa kwa sababu wazungu pia waliwaua wapinzani wao (babu zetu) kwa kupigania haki?
Kuuawa na mzungu mkoloni ama kuuawa na ndugu yako muafrika tena uliye muamini sana, kipi kinatia uchungu sana?

Babu zetu hawakuwa na mipaka ya umri, walio leta utaratibu wa mimba za utotoni ni hao hao wazungu kwa kupanga umri mkubwa uanzie miaka 18.

Wazungu hao hao ndio waliolazimisha mwanafunzi akisha jifungua aendelee na masomo, kitu ambacho babu zetu huko nyuma walikikataa. Hatuwezi kuendesha mambo yetu wenyewe bila ya hao wazungu ambao tunawaita wahisani/wadau wa maendeleo.

Yaani yote hayo tunakubaliana nayo lakini bado mzungu kwetu ni adui?

Kama ni rasilimali walituacha nazo.
Lakini tangu waondoke na sisi kuwa huru tumefaidika nini na rasilimali zetu? Miundombinu, mashamba na viwanda walivyotuachia vimekwenda wapi adi tumefika miaka zaidi ya 50 ya uhuru lakini bado tunaishi kwa misaada ya wazungu?

Elimu yetu, afya zetu na kila kinachotuzunguuka katika maisha yetu ya kila siku tunategemea wazungu.

Sasa hoja ya kuwakataa wazungu inakujaje kwa mfano?
 

Don Nzoko

Senior Member
Jan 6, 2020
177
250
Hii ndiyo tofauti ya mwanafrica mzalendo.wapigania uhuru babu zetu hawakuwatetea wazungu,bali waliwasema hadharani na hata kuuawa ndipo tukapatata uhuru ambao sasa tunautumia kuongea hovyo,kutetea mimba za utotoni,kutetea wezi wa rasilimali zetu,kutetea wanaume koana wao kwa wao Nk...
nikukumbushe kitu Mandela alipata urais kwa msaada wa haohao wazungu na bila USA na uk kuweka Nguvu yawezekana mpk Leo makaburu wangekuwa wanatawala south Afrika
 

Tigershark

JF-Expert Member
Oct 9, 2018
6,500
2,000
Acha kuonyesha ujinga wewe, hudanganyiki na nani? Tanzania hatujawahi kupinga wazungu kwa kuwa huo ni ubaguzi ambao sisi tuliupinga. Hatukuwa na ugomvi na wazungu wa South Afrika, tulikuwa na ugomvi na serikali ya Makaburu ya South Africa iliyokuwa ya kibaguzi....
Umemaliza kabisaaa,thread closed
 

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
148,610
2,000
Beberu ni nani? Siku hizi tangu tupate ufafanuzi hatumjadili tena beberu

Jr
 

Magonjwa Mtambuka

JF-Expert Member
Aug 2, 2016
23,420
2,000
Hii ndiyo tofauti ya mwanafrica mzalendo.wapigania uhuru babu zetu hawakuwatetea wazungu,bali waliwasema hadharani na hata kuuawa ndipo tukapatata uhuru ambao sasa tunautumia kuongea hovyo,kutetea mimba za utotoni,kutetea wezi wa rasilimali zetu,kutetea wanaume koana wao kwa wao Nk..
Hawa vijana akina Lisu na Zitto hawajielewi.
 

FUSO

JF-Expert Member
Nov 19, 2010
20,951
2,000
Hii ndiyo tofauti ya mwanafrica mzalendo.wapigania uhuru babu zetu hawakuwatetea wazungu,bali waliwasema hadharani na hata kuuawa ndipo tukapatata uhuru ambao sasa tunautumia kuongea hovyo,kutetea mimba za utotoni,kutetea wezi wa rasilimali zetu,kutetea wanaume koana wao kwa wao Nk..
kwa nini Mwalimu alichangisha hela kwenda UNO, kwa nini Mwalimu baada ya uhuru tu alifanya ziada ya kiserikali Marekani na uingeleza....?

Kwa hiyo Unatuaminisha kwamba Mwalimu alikuwa anashirikiana na mabeberu kuja kuzidi kutuibia eee
 

FUSO

JF-Expert Member
Nov 19, 2010
20,951
2,000
Unakuwa na kiongozi wa kitaifa miaka mitano yote mwisho wake Mkuranga!!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom