Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 47,014
- 144,371
TAARIFA KWA UMMA
Tunazo taarifa zilizothibitishwa kwamba viongozi wetu watatu wa Ngome ya Vijana Jimbo la Kigoma Mjini Wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Wilaya ya Kigoma Mjini.
Viongozi hao wa Ngome ya Vijana Jimbo la Kigoma Mjini; Said Mlindwa (Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana Jimbo), Wakili Mubanga (Katibu wa Vijana Jimbo) na Ntakije Ntanena (Katibu Mwenezi wa Ngome ya Vijana Jimbo) walikuwa wanapeleka taarifa kwa jeshi la polisi kuhusu maandamano ya amani ya kumpongeza Mbunge wa Kigoma Mjini Ndugu Zitto Kabwe na Madiwani wa Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa kazi kubwa wanayoifanya kuwaletea wananchi maendeleo.
Ni jambo la aibu na kusikitisha kwa Jeshi la Polisi kuwakatamata na kuwaweka ndani watu waliofika Polisi wenyewe kufuatilia utekelezaji wa masharti ya kisheria ya kufanya maandamano ya amani.
Wakati viongozi wetu na wanasheria wakifuatilia kwa karibu kuhakikisha viongozi hao wanapata haki yao, tunalitaka jeshi la polisi la polisi liwaachie huru viongozi hao mara moja.
Ado Shaibu,
Katibu wa Itikadi, Mawasiliano na Uenezi, ACT Wazalendo
07 Januari 2019
Huu hapa chini ndio ujumbe aliouandika Zitto katika mtandao wa twitter: