Wakati wa waastafu kuokoa jahazi

lukala

JF-Expert Member
Jun 6, 2017
575
565
Ndugu wanabodi,habari za asubuhi!!!!!!!!!!!!!

Kwahali inayoendelea sasa katika nchi yetu kuna muhimu umuhimu kwa waastafu wote kwa kila idara waje watusaidie kutoa ushauri jinsi kuendeleza gurudumu hili,

Hali inayoendelea katika nchi inatia shaka haiwezekane kila siku watu wanakuwa na taharuki na ukiangalia ndani ya miaka miaka miwili hali imebadilika hivyo na hali mbaya zaidi

Kwanza kabisa nahofu matokeo ya huduma inaweza kuporomoka vibaya sana , tukianzia na Elimu kwa uchungu mkubwa naiona matokea ya kuhitimu elimu zetu kuanzia darasa la saba na kidato cha nne kitaporomoka muda sio mrefu, kwa tafiti yangu ndogo niliyoifanya nimegundua walimu wengi wameshuka morali ya kufundisha , kuna sababu mbili

(1) walimu wengi waliopo mashuleni ni vijana na wengi wao walipitia chuo kwa mikopo then walipopata ajira na kutimizi masharti ya mikopo walienda benk na kuacha moja ya tatu. Serikali ilipotunga sheria mpya hawa watu wanahali mbaya wanaenda kazin basi .

(2) Jambo jingine linalowasumbua hawa walimu hali ya kiuchumi linavyoyumba , mfano wakati serikali inaingiza makato hayo imesahau kuingiza nyongeza ya kawaida huku ikijua kwamba gharama zinapanda siku hadi siku, chukulia mfano mwalimu aliyeajiliwa 2015 hadi kufikia sasa wengi wao tayar wanawatoto na mke , je hao wanahudumiaje ? Huyo mwl akiingia darasan atafundisha au atafikiria familia?

Sekta afya hapa panatatizo kubwa lakini watu hawapaangalii, kiukweli kwenda hospitali za serikali huku mikoani ni hatari, madawa hakuna unaambia ukanunue maduka ya nje sasa hapo kuna huduma kweli?

OMBI KWA SERIKALI
Serikali ijaribu kuwatumia waastaafu katika ushauri wa uendeshaji nchi , mfano Mzee Kikwete kwenye suala la kiuchumi alifanikiwa sana ndicho kipindi chake katengeneza madaraja makubwa hapa nchini.

Kipindi cha mzee Kikwete ndio kipindi ambacho nchi yetu imetengeneza mabarabara bila kuharibu uchumi wa mtu binafsi, ni wakati wa awamu hii kujifunza manzuri kutoka kwake asili ya mafanikio.

Tukija katika swali la mazao ,hapa hapahitaji nguvu kubwa serikali ijaribu kuangalia nn alikuwa anafanya waziri wa kilimo kipindi cha awam ya nne, kwann hapakuwa na malalamiko kama ilivyo sasa ,kwanini kipindi cha mh Kikwete pembejeo ilikuwa juu kidogo lkn masoko yalikuwa na uhakika hata wafanyakazi wengi waliingia sekta ya kilimo.

Pia kwenye hii tetesi za kudodoro uchumi serikali ijaribu kutumia wachumi kama pr Lipumba ,Zitto , Ndullu hata waliopo nje ya nchi kama alivyojitahidi mh Kikwete.

Asanteen kada mtiifu wa ccm
Kutoka Masasi
 
Swissme
 
Attachments

  • 22601493_596609610509364_2579867725199310848_n.mp4
    4.2 MB · Views: 58
Kuna Naibu Waziri alinukuliwa akisema "....binti asiozwe wala kuolewa mpaka awe na cheti cha kidato cha nne...", nikajiuliza hiyo elimu wanayotoa ni ipi hasa? Au wao kwao kupata cheti ndio kuelimika? Hadi nikaumkumbuka msemo wa dada yangu Faiza Foxy "huko shule huwa mnaenda kujifunza ujinga?"

Kiwango cha elimu kimekuwa kikishuka na kuporomoka kwa zaidi ya miaka 15 sasa. Tiba sahihi ni tukae kama nchi tutafakari na kuchambua kisha tuchague sera na malengo ya elimu kwa watoto wetu. Hii elimu ya kila Waziri au Utawala kuja na lwake imechangia sana kudidimiza na hata kuua elimu bora kwa watoto wetu.
 
Yap
 
Haaambiliki ukimwambia anafanya makusudi kukukomoa.......ujinga!! Akivuruga miezi 6 anaenda kujisifia kwa wabibi na kuongeza charge.....anarudi anavuruga..!! Hakuna nchi Africa imepigana vita y uchumi ya miaka 10 ikashinda......hakuna strategy hiyo....never unajivuruga mwenyewe na kuharibu uchumi kama ilivyo sasaa tumekosea sanaa!!! Marais waandaliwe wajengw watengenezwe.....wajue siasa uchumi diplomasia....jeshi propaganda........waandaliwe!!!
 
Kweli Lambardi
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom