babayah67
JF-Expert Member
- Mar 28, 2008
- 493
- 79
Ukizingatia yaliyotokea Zanzibar baada ya Uchaguzi mkuu yaani kuwepo kwa serikali ya umoja wa kitaifa huko Zanzibar, na ukiangalia performance ya CUF kwenye uchaguzi mkuu kwa upande wa TZ-Bara, wenye akili watagundua kuwa Umuhimu wa wapenzi wa CUF wa TZ-Bara, kujiengua toka CUF-ZNZ kwa sasa ni wa 100%. Muafaka wa CCM na CUF Zenji, umewafanya CUF-bara wasiweze kukubalika tena miongoni mwa raia wa TZ. Sio siri kwa sasa CUF bara inaonekana kama vile ni chama kinachoishi kwa hisani ya CCM, sintoshangaa katika baraza la mawaziri lijalo JK akamteua mmoja wa wabunge toka CUF kuingia serikalini. Hali hii ina maanisha nini kwa wengi wa vijana wapenzi na wakereketwa wa CUF bara????. Ombi langu kwa vijana wengi mlio ndani ya CUF TZ-Bara, kujiengua toka CUF Zenji hivi sasa na kuunda chama chenu kitakachokuwa na malengo na mitazamo ya kueleweka kwa ndugu zenu wengi wa bara. Nawakilisha