Wakati wa kumpongeza Rais Magufuli haujafika bado.

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
5,372
2,000
Rais wetu ameonyesha dalili za kutaka kuwasaidia watanzania lakini matamanio take haya bado kuzaa matunda yanayokusudiwa. Watanzania bado wanataabika kwa kukosa maji, chakula, mavazi safi, mahali safi pa kulala, matibabu, usafiri, ajira, umeme wa uhakika, mikopo ya shule na utawala bora. Hivyo, muda wa kumpongeza bado, bali tumuunge mkono katika kuipanga upya nchi take. Safari ya kuipanga upya LAZIMA ianze na kuipanga upya Katiba na Sheria zilizopo. Maana mambo mengi kama sio yote yalifanyika kwa mujibu wa ama katiba au Sheria zetu zilizopo ziwe nzuri au mbaya. Yaani garbage in garbage out. Hivyo kama tunataka kumpongeza Rais lazima tumpongeze kwa mtiririko wa namna anavyofanikisha yaliyomo kwenye orodha (check list) ya mahitaji ya wananchi. Wananchi wanataka maji sio makinikia, wanafunzi wanataka mikopo na elimu nzuri sio madini.
 

South

JF-Expert Member
Jan 11, 2016
3,483
2,000
Sidhani kama kuna alichotimiza zaidi ya kufanya ambayo hakuyaahidi na kwa kuvunja katiba
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom