Wakati wa kuacha na wakati wa kushikilia....nataka jibu

Babu anatafakari, maneno kuyashikia,
Mistari kukariri, ujumbe kuupatia,
Japo bado anakiri, ukweli hajaujua...
Mento hii ni hadithi, au kweli watwambia?

Kama ni kweli ntalia,
Sitoweza vumilia,
Ubaya lokufanyia,
Kamwe hauvumiliki.

Unyama gani jamani,
Umejiri mapenzini,
Kuumizana moyoni,
Kamwe hakuvumiliki.
 
toilet-paper.jpg
...mkongwe, tatizo nini kaka? ...ya nini kujitoa thamani kama karatasi ya chooni?!
 
Mentor we kama unataka kuambiwa uendelee kuhangaika nakwambia MENTOR MFUATILIE MPAKA UMRUDISHE MIKONONI MWAKO.Jana alikupima na mimba ukapata presha ya dakika...leo anakupima kwa kukwambia penzi limehama kwa muda...kesho na kesho kutwa atakapokuja kukwambia mtoto "wenu" sio wako utapata BP ya kweli ai hata uzime kabisa sijui atakwambiaje ilikua utani.Kama kweli anachofanya ni utani she needs to GROW UP.Hata akirudi akakwambia alikua anakutania tu inabidi na wewe umwonyeshe uanaume wako...mwambie kwamba hajamature na huo mchezo wa kurushana roho kila siku utajaishia pabaya.Mwambie unampa muda AKUE akishakua ndo aje muendelee.Kumpenda isiwe sababu ya wewe kufanywa mjinga bwana....!

nadhani hapo ndo umenena dadangu..haika sana!
though ni kama umenipa klorokwini na pilipili nashukuru.
Na ingawa inabidi nikiri nimempenda sana binti huyu, sina budi kuuchukua uamuzi huu.

Btw, na wewe pia unaungana na Mokoyo hapo juu kwamba there is never a time for fighting for love!??
 
Babu anatafakari, maneno kuyashikia,
Mistari kukariri, ujumbe kuupatia,
Japo bado anakiri, ukweli hajaujua...
Mento hii ni hadithi, au kweli watwambia?

Kama ni kweli ntalia,
Sitoweza vumilia,
Ubaya lokufanyia,
Kamwe hauvumiliki.

Unyama gani jamani,
Umejiri mapenzini,
Kuumizana moyoni,
Kamwe hakuvumiliki.

Babu kweli metokea, japo sikusitahili
mjukuu meumia, moyo pingilipingili
binti niliyempenda, kapata bwana mwingine
kisa mimi niko mbali, sijui mimi genuine!
 
Najua linalo kuumiza ni yy kuwa wa mwanzo kukuacha but kuwa mvumilivu angalia mbele japo ningumu sana kwani mipia yalinikuta japo nilikuwa jeuri wa maamuz na kila m2 anawazo lake wakt kama huu ukimfikia. chamsing u2livu na maamuzi ya busara kupigana hakuna maana pale kwenye ukweli. poleee
 
Mwj1....:pray:...Forget the bite, I sing for you;
♫ nalia kwa furaha
A%20S-heart-2.gif
Klynn ft Bushoke ♫

Mbu, nilinogewa na wimbo, nikasahau the bite...inauma kaka!!!
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Mwj1....:pray:...Forget the bite, I sing for you;
♫ nalia kwa furaha:A S-heart-2: Klynn ft Bushoke ♫

Mbu, nilinogewa na wimbo, nikasahau the bite...inauma kaka!!!

...naelewa machungu yake,...lakini kwanini ana ku 'beep' kila mara?
Hayo makovu si salama kuingia nayo kwenye ndoa,...

Amini usiamini, kwa msingi huu nyumba yenu itakuwa na nyufa kila mahala
na hamtakuwa na amani.

Upo tayari kuishi hivyo mpaka mwisho wa maisha yako?
 
Kusema ukweli wengine wapigane tu....mimi simo.

Kwa nini hasa? dont you think sometimes inabidi upigane mwenzio ajue how worthy they are to u?
labda ni ka-situation alichopo ndo kanampa giza kushindwa kuona mbali.
Labda ni upweke akaona haitawezekana..
sometimes mtu unajisahau tu..

**PS** am not trying to justify anything..nauliza tu.
 

Upo tayari kuishi hivyo mpaka mwisho wa maisha yako?

Sipo tayari mkuu,
my dream married life is not that way...haiko hivyo kabisa!\
I guess nimekupata mkuu.

Vipi na wewe, would you fight for love?
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Babu kweli metokea, japo sikusitahili
mjukuu meumia, moyo pingilipingili
binti niliyempenda, kapata bwana mwingine
kisa mimi niko mbali, sijui mimi genuine!
Mapenzi haya ya mbali, usiyatie manani,
Utawekwa namba mbili, utolewe na moyoni,
Yauma kama shubili, au mkwamo kooni,
Sasa piga moyo konde, yaliyospita si ndwele.
 
Sipo tayari mkuu,
my dream married life is not that way...haiko hivyo kabisa!\
I guess nimekupata mkuu.

Vipi na wewe, would you fight for love?

Kama ni mimi kujibu hilo swali, I will fight for love only if it's worth..Else, I will move on(ofcourse maumivu hayakosekani)!..
Mind you kama mtu anakuchezea akili, amekuchoka na anakufanya kama mpira wa dana dana hiyo siyo fair na huwezi ku-fight kwa such love.Pole sana Mentor!
 
Back
Top Bottom