Wakati wa kuacha na wakati wa kushikilia....nataka jibu

Mentor

JF-Expert Member
Oct 14, 2008
20,328
23,879
FlasMwenzenu yamenikuta, yaloukuta mtete
nilijiona ukuta, yasingenifika mentor
kaniona wa kupita, nimebaki hali tete
sijui nipigane, au kipepeo nimuache.



Labda nianze hivi...

"I wanna be with you.
I want us to make it work.
I dont know how, but we can try.
Am saying yes, Mentor.
I wanna be ur gal & only urs.
Bt u also have to promise to love me only.
I really do love you..."


disemba mbili na kumi, aliutuma ujumbe
masomo nilimaliza sasa narudi nyumbani
kamuaga wangu hani japo tutakuwa mbali
penzi silibadili siku moja tule wali.

Na machozi akalia nami kaona huruma
kweli mi nilimpenda ukweli siezi ficha
nikajua tamuoa ndani awe wangu mke
sijui nipigane, au kipepeo nimuache!




Flash back...

ilikuwa septemba nilimuona mrembo
marafiki si tukawa tukazidisha upendo
mcheshi, mzuri moyo, msafi dharau kando
kaniteka taratibu kwake nikashindwa toka.

nikaufungua moyo yote nikamueleza
pengi nimeshajaribu kaishia kuteleza
kwake sitaki sababu nitapigana kupata
sijui mi nipigane, au kipepeo nimuache!

naye akanieleza, alivyonipenda tangu
alikuwa kwa gereza, tena amefungwa pingu
nikaja nikalegeza, moyo wake kauteka
kaniahidi upendo, na vyote vitavyopatika.


fast forward....

september
october
november
december
january
february
march
april
may
june
july...

wiki ya jana...

simu nampigia mwenzangu hakupokea
nikapatwa na simanzi nini kimemtokea
kauliza marafiki wote wakanigomea
moyo ukanisinyaa kuwaza lilotukia.

ghafla kapata ujumbe ulonitatiza moyo...

"I hate that I have to do this bcz i know ur genuine with me.
Im sory.
But u and I cant be!"



Paa!
ni kama vile gobole limepiga moyo wangu
sikuyaamini macho limenitokea kwangu
sababu hataki nipa yote imekula kwangu
sijui nipiganie, au kipepeo nimuache!

Wahenga walishasema ukipendacho pigana
kwani si ndo walifanya Romeo na julieta
Julius Kaisari na kaka Valentino
wengine nimesahau ila nataka wafuata.

Wahenga tena wakanena ukipendacho kiache
kama chako kitarudi si chako kitapepea
mapenzi kama kipepeo ukifuata charuka
sijui nipiganie, au kipepeo nimuache!

Hilo ndo langu tatizo kwani bado nampenda
nimuache bila vita taonekana mnyonge
ila nitapopigana na hakuwa wangu kweli
mwisho itakula kwangu na pweke nijibakie.

GENUINE:

nini alimaanisha ati mimi kwake genuine
kwani alitaka feki bado sijamuelewa
ama yeye ndiye feki kwangu asingeliweza
sijui nipiganie au kipepeo nimuache!

Jana usiku manane, tanesco weshaniudhi
nikapokea mwingine, ujumbe kanitumia...

"I blv ur a truly genuine guy
& the last thing i wanna do is is hurt ur filingz.
U deserve beta than that.I'm seeing another guy
been wit him a month noW!"

Sikulihitaji hili na sidhani ni faraja
nilimkosea nini au umbali ndo shida
lakini tuliafiki kupendana bila hoja
kweli umeniumiza, na moyo kanipondea.

swali moja nauliza na hili nataka jibu
wakati upi wakuacha na upi wa kupigana
niendelee shikilia ama kamba niachie
sijui nipiganie au kipepeo nimuache!


 
Mentor kaka yangu pole saaana.... Mimi kwa jinsi nilivyo msoma ni kua mapenzi
yake juu yako sasa basi! Na inawezekana ni mda mrefu alikua anatafuta jinsi ya kukueleza
but akawa anashindwa tu namna ya kukwambia... na kama ujuavyo huwezi lazimisha
kupenda ama kupendwa... Hiyo hakua formular kwamba sasa mpigane sasa muachane...

Itakua ni ngumu but with time believe me things will get beta and you will surely meet
someone who you deserve and deserves you back....
 
Mentor kaka yangu pole saaana.... Mimi kwa jinsi nilivyo msoma ni kua mapenzi
yake juu yako sasa basi!
Na inawezekana ni mda mrefu alikua anatafuta jinsi ya kukueleza
but akawa anashindwa tu namna ya kukwambia... na kama ujuavyo huwezi lazimisha
kupenda ama kupendwa... Hiyo hakua formular kwamba sasa mpigane sasa muachane...

Itakua ni ngumu but with time believe me things will get beta and you will surely meet
someone who you deserve and deserves you back....

"Jus know that What I said earlier I meant it. Jus didnt want to hurt u...am sor."
 
How do you tell?
Well unless uliyoandika hapo juu sio sahihi endelea kupigana...thats all I can say.Maana kama mwenzako ameshakwambia hana muda na wewe na kwamba anatoka na mtu mwingine sasa sijui utakua unataka nini kuendelea kumfukuzia.Maybe another ‘heartbreak in the future?!Kama uko tayari kwa hilo mbembeleze mpaka akurudie alafu siku ukimkuta kitandani na mwanaume mwingine akwambie “ulijua kabisa sikufeel ukaning‘ang‘ania kwahiyo amua utakavyo.“
 
Mentor! Pole. Unaweza kuwa anakupima imani, km unadhani bdo unampenda go and fight 4 her since u dont hv anythng to loose ukijaribu kupambana. U knw women smtimes wanapenda kupima maji na huyo anatamani kujua hlo pendo lako ni kubwa kiasi gani. Ukikausha bs atajua haukumpenda na utampoteza wakati bdo anakupenda nawe unampenda.
 
Mentor! Pole. Unaweza kuwa anakupima imani, km unadhani bdo unampenda go and fight 4 her since u dont qhv anythng to loose ukijaribu kupambana. U knw women smtimes wanapenda kupima maji na huyo anatamani kujua hlo pendo lako ni kubwa kiasi gani. Ukikausha bs atajua haukumpenda na utampoteza wakati bdo anakupenda nawe unampenda.
Huwezi kumchezea mtu unaempenda mchezo wa aina hiyo kwa zaidi ya wiki.Kama unataka kumpima mtu tumia siku moja then mwambie ulichogundua sio unamvunja mwenzako moyo for weeks alafu baada unakuja kulia eti sijui ulikua unampima...amekua ngano?!
 
hakuna wakati wa kupigana kwenye mapenzi. Kuna wakati wa kupenda, kuacha na kuachwa tu. Full stop
 
Huwezi kumchezea mtu unaempenda mchezo wa aina hiyo kwa zaidi ya wiki.Kama unataka kumpima mtu tumia siku moja then mwambie ulichogundua sio unamvunja mwenzako moyo for weeks alafu baada unakuja kulia eti sijui ulikua unampima...amekua ngano?!
may be hajabembeleza ungekuta ameshajua kuwa amemwagwa jumla au matani.
 
may be hajabembeleza ungekuta ameshajua kuwa amemwagwa jumla au matani.
Sasa huo ni utoto...Kama hajabembeleza kama alivyotakiwa ina maana huyo dada angeshaona kwamba hapendwi na angeshamwambia ukweli.SUMU HAIONJWI....either unaitaka uinywe au hutaki ukae nayo mbali.Mambo ya kutishana kwenye mapenzi na kupimana kwa vipimo kama hivyo vya sijui asiponibembeleza basi ni ujinga...PERIOD.
 
Sasa huo ni utoto...Kama hajabembeleza kama alivyotakiwa ina maana huyo dada angeshaona kwamba hapendwi na angeshamwambia ukweli.SUMU HAIONJWI....either unaitaka uinywe au hutaki ukae nayo mbali.Mambo ya kutishana kwenye mapenzi na kupimana kwa vipimo kama hivyo vya sijui asiponibembeleza basi ni ujinga...PERIOD.

Dadae, kidonge changanya na sukari basi! unasema ukweli lakini unamuma sana...punguza makali.

Then, alishawahi kunifanyia hivi samtym ago kama unakumbuka nikiweka post moja hapa! baadaye akaja niambia kuwa alikuwa anacheki my reaction kama angekuwa na mimba kweli.
This tym ni ngumu hata kumtafuta maana hawa Airtel ni kama wameniweka mtaji wao, nikipiga wanani-charge kama nini sijui. And yeye akipiga bado na mimi nakatwa..inakuwa ngumu kupata ujumbe kamili from sms peke yake.
Kiukweli bado nampenda, nilijaribu kupotezea weekend lakini wapi..nikilala nikiamka...i just kant!
 
may be hajabembeleza ungekuta ameshajua kuwa amemwagwa jumla au matani.

Unabembeleza kama umeachwa kwa makosa yako..sasa nikianza kubembeleza sasa hivi si nitaonekana weak xana...mi nimejifanya wala haijanitouch kivile ingawa moyo ndo wajua yote!
 
hakuna wakati wa kupigana kwenye mapenzi. Kuna wakati wa kupenda, kuacha na kuachwa tu. Full stop

Is this for real!??
"And nothing in love is free,
So if it's not worth fighting for,
It's worth nothing at all."
- White Town
 
Dadae, kidonge changanya na sukari basi! unasema ukweli lakini unamuma sana...punguza makali.Then, alishawahi kunifanyia hivi samtym ago kama unakumbuka nikiweka post moja hapa! baadaye akaja niambia kuwa alikuwa anacheki my reaction kama angekuwa na mimba kweli.This tym ni ngumu hata kumtafuta maana hawa Airtel ni kama wameniweka mtaji wao, nikipiga wanani-charge kama nini sijui. And yeye akipiga bado na mimi nakatwa..inakuwa ngumu kupata ujumbe kamili from sms peke yake.Kiukweli bado nampenda, nilijaribu kupotezea weekend lakini wapi..nikilala nikiamka...i just kant!
Mentor we kama unataka kuambiwa uendelee kuhangaika nakwambia MENTOR MFUATILIE MPAKA UMRUDISHE MIKONONI MWAKO.Jana alikupima na mimba ukapata presha ya dakika...leo anakupima kwa kukwambia penzi limehama kwa muda...kesho na kesho kutwa atakapokuja kukwambia mtoto “wenu“ sio wako utapata BP ya kweli ai hata uzime kabisa sijui atakwambiaje ilikua utani.Kama kweli anachofanya ni utani she needs to GROW UP.Hata akirudi akakwambia alikua anakutania tu inabidi na wewe umwonyeshe uanaume wako...mwambie kwamba hajamature na huo mchezo wa kurushana roho kila siku utajaishia pabaya.Mwambie unampa muda AKUE akishakua ndo aje muendelee.Kumpenda isiwe sababu ya wewe kufanywa mjinga bwana....!
 
Back
Top Bottom