Wakati wa Klabu ya Yanga kuuzwa rasmi kwa Manji umefika

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
125,744
239,393
Inasemekana huyu ndiye mlipaji mkuu wa Yanga , ndiyo benki ya timu , ni Mwenyekiti lakini zaidi ni mgombea pekee wa Uenyekiti kwenye uchaguzi ujao .

Katika kipindi chake tumeona Yanga ikipaa kimataifa .

Kama wanachama wengine hamtoi chochote kwanini msibaki kama washabiki tu , ili timu imilikiwe na mtu mwenye uwezo moja kwa moja ?

Kila mwenye macho ameshuhudia Kibopa Abramovic alivyoibadilisha Chelsea , mifano ni mingi sana ! Hapo jirani DRC , PDG Katumbi hakuna asiyeujua mchango wake kwenye harakati za TP MAZEMBE kutawala soka la Africa .

Shime wana Yanga wakati ni huu , yale mambo ya kudai " nilichangia tofali au sijui nilibeba mchanga " yamepitwa na wakati .
 
Inasemekana huyu ndiye mlipaji mkuu wa Yanga , ndiyo benki ya timu , ni Mwenyekiti lakini zaidi ni mgombea pekee wa Uenyekiti kwenye uchaguzi ujao .

Katika kipindi chake tumeona Yanga ikipaa kimataifa .

Kama wanachama wengine hamtoi chochote kwanini msibaki kama washabiki tu , ili timu timu imilikiwe na mtu mwenye uwezo moja kwa moja ?
Hayo ndiyo maneno boss sio Mimi Yanga damu hata mchango huna
 
Inasemekana huyu ndiye mlipaji mkuu wa Yanga , ndiyo benki ya timu , ni Mwenyekiti lakini zaidi ni mgombea pekee wa Uenyekiti kwenye uchaguzi ujao .

Katika kipindi chake tumeona Yanga ikipaa kimataifa .

Kama wanachama wengine hamtoi chochote kwanini msibaki kama washabiki tu , ili timu timu imilikiwe na mtu mwenye uwezo moja kwa moja ?

Daaa! ukweli unaumaaa!
Tatizo kubwa la klabu zetu hizi za Yanga na Simba pamoja na wanachama wao ni kuendekeza njaa na utegemezi!, ukiwa na mpunga tu unaweza kuiweka mkonono mwako klabu nzima, wazee wa klabu na hata makomandoo wake....Lakini ukitafakari kwa kina kule jangwani Manji anaihitaji Zaidi Yanga kuliko Yanga inavyomuhitaji na sababu zipo nje nje hata asiyeona anazijua!
 
imefika wakati hizi timu mbili (Simba na Yanga) zisonge mbele kiuchumi ili soka la nchi yetu liende hatua moja zaidi mbele. njia pekee ni kuondoa Uswahili kwenye hizi klabu na kuzi-commercialise. wafanya biashara walio interested wapewe nafasi ya ku-bid for the majority shareholding. Waswahili wa-retain some shares for loyalty.

kibiashara these are very attractive brands. nionavyo mimi ziko much stronger than Manji, Mo & Bakhresa all rolled into one.

so, Yanga wanaweza kuanza na the Manji's of this world. Simba kuna Mo ambaye tayari ameonyesha interest kubwa.

Chelsea, Liverpool, ManCity, Man U, Arsenal, TP Mazembe au hata Azam - oneni zinavyoendeshwa kwa mafaninikio na kuwafurahisha wapenzi wao.

wito kwa ninyi wanachama wa hizi timu 2: chukueni hii ajenda (seriously) muende nayo kwenye mkutano mkuu. ama sivyo kutoka hapo mlipo ni ndoto ya alinacha!
 
Daaa! ukweli unaumaaa!
Tatizo kubwa la klabu zetu hizi za Yanga na Simba pamoja na wanachama wao ni kuendekeza njaa na utegemezi!, ukiwa na mpunga tu unaweza kuiweka mkonono mwako klabu nzima, wazee wa klabu na hata makomandoo wake....Lakini ukitafakari kwa kina kule jangwani Manji anaihitaji Zaidi Yanga kuliko Yanga inavyomuhitaji na sababu zipo nje nje hata asiyeona anazijua!
Kivipi ?
 
Mimi nauliza tu, mbona biashara za Manji zinakuwa na kupanuka lakini Yanga haina biashara licha ya asset ilizonazo?

Manji ni walewale tu yupo Yanga kutimiza ajenda zake, kwahiyo akifa Manji na Yanga kwishney?
 
Kapongo my friend... Unalalama tu ! Huchukui action! Mnasema watu wanaendekeza njaa... Sasa kama hamtaki Manji aongoze Yanga, wapeni maskini waiongoze. Mtaweza lipa wachezaji wa hadhi kama ya Ngoma nyie! Mtaishia kusajili magarasa kila siku kama Chura Fc! tumechoka miaka na miaka Yanga imeongozwa na wajasiriamali wa kawaida wakaishia kuinyonya Yanga zaidi kuliko kuisadia. Wanachama na wapenzi wa Yanga tumeumia na kuhuzunika muda mrefu mno tukikosa furaha kwa timu yetu kufanya vibaya. Eti leo mnatupa ushauri feki wa kutaka turudi tulikotoka! Mnatakiwa muone aibu nyie! Manji, Manji, so what......!
 
Mimi nauliza tu, mbona biashara za Manji zinakuwa na kupanuka lakini Yanga haina biashara licha ya asset ilizonazo?

Manji ni walewale tu yupo Yanga kutimiza ajenda zake, kwahiyo akifa Manji na Yanga kwishney?
Nimecheka sana !
 
Tunachokitaka kutoka kwake ni kuona timu inafanya vyema kwenye michuano mbalimbali kama ilivyokuwa mwaka huu.

Biashara zake hazituhusu.

Chochote kitacho tokea ni cha ziada tu... au mbwembwe!
 
Nani amewadanganya klabu kumilikiwa na mtu ndio inapata mafanikio ?

Kama klabu haiwezi kugharamia gharama za klabu then akaja mtu mwenye pesa zake bila shaka itafanikiwa.....

TP mazembe & AS vita.! Zingatia hizi klabu.

Simaanishi Mafanikio ya Yanga SC yameletwa na Manji. La hasha, bali uwepo wake umeongeza ubora zaidi kwa klabu.
 
Weka picha mkuu.

unnamed%2B%252868%2529.jpg

Manara akishangilia goli la pili la Yanga dhidi ya Simba.
 
Mimi nauliza tu, mbona biashara za Manji zinakuwa na kupanuka lakini Yanga haina biashara licha ya asset ilizonazo?

Manji ni walewale tu yupo Yanga kutimiza ajenda zake, kwahiyo akifa Manji na Yanga kwishney?
...Mbaya hata Duka la vifaa vya jezi za kwao na vitu vingine vya Yanga kama Azam hawana,wamebaki kuvaa midosho tu,
 
Kuna vimtu duni visivyo hata na kumi mfukoni huwa vinadumaza sana hizi klabu zetu. Umefikia wakati vijana kureplace wazee kwenye hizi klabu ndio tutaona tija. Haiwezekani klabu iwe na mwenyekiti anatinga mkutanoni na makubazi hata kusoma hajui anaongea mate yanamtoka mdomoni staha hana kazi ushirikina.

Azam ile pale, hamna majungu makubwa sababu hamna njaa. Simba imefeli sababu ya njaa. Tusibishe kwenye hili, ni Manji ndio kaileta hii Yanga ya kimataifa
 
Back
Top Bottom