Wakati vikosi vya JKT vilipokuwa matawi ya Chama

MIGNON

JF-Expert Member
Nov 23, 2009
4,080
5,045
Wa zamani wanalikumbuka hilo.Vikosi vya JKt vilikuwa matawi ya CCM na mkuu wa Kikosi ndiye alikuwa mwenyekiti wa CCM wa tawi.Kwa kuruta kikao cha Chama kilikuwa ndiyo kikao cha kuelezea kero zote,hatushibi,tunaamshwa usiku mno,kuna afande huyu na yule n.k.Kawaida mwenyekiti wa tawi alikuwa anatoa msimamo kwa kila swali na mara nyingi majibu yake yakiwafurahisha kuruta.
Mwenyekiti akifunga kikao na kuondoka alikuwa anasimama RSM (Regiment Surgent Major) na zoezi zima lilibadilika na kuwa "Makamanda mnafanya kazi gani mpaka kuruta wanapata muda wa kupiga majungu?"
Nimekumbuka hili nikihusisha na mkutano wa jana kati ya namba moja na wafanyabiashara.Naamini baada ya wafanya biashara kuondoka wakichekelea huku nyuma,mmmh.Sijui!!
 
Uwiii!
Kwa hiyo jana baada ya Yohana kuondoka kwenye kikao, nani alikuwa
Regiment Surgent Major?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom