Wakati unapanga mipango yako ya biashara mwakani usisahau yafuatayo

miamiatz

JF-Expert Member
Dec 4, 2017
504
926
1. Kodi lazima iwe jambo la kwanza kuwaza. Hebu waza kwanza ni biashara gani nifanye ambayo haitonilimbikizia mzigo wa kodi? Ni lazima biashara utakayoichagua iweze kukupa faida ya kutosha kuliko kodi utazolipa serekalini. Hii huitwa tax planning.

2. Biashara gani itaakisi hali halisi ya uhaba wa pesa kwenye mzunguuko? Sio lazima ung'ang'ane na biashara ambayo haiakisi hali halisi ya upatikanaji wa pesa mtaani. Waza biashara za bidhaa ama huduma ambazo ni necessities.

3. Iwapo biashara itayumba back up niliyonayo itatosha kuendesha maisha? Kufeli kwa biashara ni kama kukatika kwa umeme wa tanesco. Usipoweka UPS kwenye desktop yako basi umejiandalia balaa.

Ukishapata majibu ya haya masuala matatu basi unaweza kuendelea kujiuliza maswali mengineyo ya ziada.
 
Soko vp mkuuu
Skuizi kodi ni swali namba moja kabla ya soko mkuu mana unaweza fanya maamuzi kwa kuangalia soko afu kodi zikakumimina. All in all kodi kwanza kisha maswali mwngine pamoja na soko yanafata.
 
diamond platnumz biashara yake sio ya lazima...ila anapiga hela kuliko wauza chakula..

biashara yeyote ni passion, ujuzi, experience, creativity na location... hayo ndiyo ya kuzingatia
 
diamond platnumz biashara yake sio ya lazima...ila anapiga hela kuliko wauza chakula..

biashara yeyote ni passion, ujuzi, experience, creativity na location... hayo ndiyo ya kuzingatia
Branding and brand management ndio mpango wa biashara za kisasa. Ukijenga brand kwa nguvu hata kama unauza ubuyu utatoboa tu.
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom