Mbwa dume
JF-Expert Member
- Jan 15, 2014
- 5,832
- 9,974
Heshima kwenu bandugu,
Kama kawa leo mwanaume wa bara niko Dar tangu jana kwa ajili ya kukamilisha process za kuchukua "kausafiri" Ila hali niliyoikuta hapa imenifanya nigundue kitu.
Ni kweli maisha ya sasa yamechange kiasi tofauti na enzi ya Jk
lakini hii isiwe sababu ya vijana kushindwa kujishughulisha na kutengeneza maisha.
Amini usiamini wakati wewe unashinda umekaa na kulalamika hali ngumu kuna watu wanakuja ulipo na wanaziona fursa zinazokuzunguka ambazo ukiweza kuzitumia vizuri utapiga hela mpaka watu watashangaa.
Binafsi hakuna muujiza utakaokuja kutokea ukaamka na kukuta pesa mezani na pia ni vizuri kwa kijana kujifunza kuishi na kukabiliana na mabadiliko yoyote yanayojitokeza.
Badala ya kushinda umekaa na kupiga "mizinga" kwa washkaji uliosoma nao kwa kisingizio cha kukosa ajira,
we tumia muda wako kutafuta mawazo na ushauri wa kujiajiri mwenyewe, elewa kuna fursa nyingi sana zinazokuzunguka ambazo siku ukifunguka mawazo ukajua kuzitumia tu umetoka.
Ujumbe kwa vijana wa chuo;
mara nyingi unapokuwa masomoni huwa tunaona maisha ni rahisi sana na wengi huamini ukipata degree tu umepata kazi.
Ukweli ni kwamba kuwa unasoma ili kuondoa ujinga na kuongeza uelewa, wakati unawaza kutumia pesa ya mkopo kununua simu ya gharama na nguo za gharama ni bora utumie pesa hiyo kuwekeza mwenye mradi mdogo kama ufugaji nk. Kwa faida ya baadae ili unapomaliza chuo ukisubiri ajira uwe na sehemu ya kujishkiza na kujipatia kipato.
Mimi binafsi sikubahatika kusoma kwa sababu sikuwa na akili ya darasani lakini Leo hii namiliki mradi ambao nimeweza kuajiri vijana wenzangu japo sijafanikiwa sana lakini naamini ipo siku nitafika ninapopataka.
Kijana tumia fursa.!