nasrimgambo
JF-Expert Member
- Jan 10, 2017
- 1,898
- 2,459
Wadau, leo katika tafakuri zangu, nimepata kufikiria sana juu ya huu mji wetu watanzania, mji wetu tunaojivunia kuwa ndo wa kisasa na uloendelea zaidi, ijapokuwa una kasoro zilizokithiri zinazohitaji kushughulikiwa, na tathmini yangu ikawa kama ifuatavyo:
Majiji mashuhuri duniani hayasifiwi kwa kushonana watu na majengo tu, bali pia hata uwepo na ubora wa maeneo ya wazi hasa bustani 'city parks'
kwa mfano jiji la New York linasifiwia dunia nzima kwa kuwa na bustani lao la central park, London wana mabustani kama vile kensington gardens na hyde park, Nairobi wana Uhuru park na hata zenji wametushinda wana kaji ka forodhani. (japo kabustani kadogoo ila jina kuuubwa)
Kwa hapa kwetu bongo, tuna huu mji umeshonana weee, na ambao serikali inahangikia kuboresha miundo mbinu yake, ila bado huu mji unafeli katika jambo moja la muhimu sana, ambalo ni aibu kubwa kwa jiji la hadhi yake,
jambo lenyewe ni kuwa jiji hili halina 'city park', city park yenye hadhi iendanayo na sifa za dar es salaam kubwa jiji mashuhuri kuliko yote Tanzania (Dar ina paswa kuwa na mbwembwe na kashkashi za aina yake)
kwanza kabisa bustani zilizokuwepo hazilingani na hadhi ya jiji
tukianza na mnazi mmoja,
hii bustani ni ndogoo na ambayo ishajazwa hospitali ya mnazi mmoja, mnara wa kumbukumbu na 'taka' nyeginezo, (tusiogope kuita taka kwa maana hayo mengine yalojengwa eneo la bustani ya mnazi mmoja yameharibu mandhari ya bustani na jiji kwa ujumla.)
haya tuangalie park ya pale gymkhana,
pale, pangefaa sana kuwa bustani ya wazi kwaajili ya wakazi ila pale ni eneo la wacheza gofu haparuhusiwi kupafungia safari ya kupungia upepo tu.
na ile garden ya samora avenue ng'ambo ya karimjee hall ni ni ndogoo.
hivyo mji hauna park yenye sifa na hadhi.
Tukumbuke pia Tibaijuka enzi zake za uwaziri wa ardhi aliwahi kuzungumzia kuwa Jangwani itageuzwa kuwa city park, (na hili lisitushtue kwa maana yapo maeneo duniani ambayo huwa park zinazofurika zikinyesha ila kiangazi kikija kuna nyasi miti na hewa ya kupendeza) ila toka ang'atuliwe waloshika hatamu wakalisahau suala hilo.
hivyo ktk tafakuri yangu nikaona mamlaka za jiji zilivalie njuga suala la public city park, jiji linahitaji bustani mpya, kubwa kuliko zilizoko ambazo wakazi wa jiji na wageni kwa ujumla wanaweza enda kupunga upepo, kuona miti na kufurahi siku za wikendi ama sikukuu
(si lazma kwenda beach ama club,
kufurahia wikendi yako ama sikukuu, bustanini pana raha yake kubarizi pia na huo ni uzungu wa aina yake pia)
tena hili mbona linawezekana, kwa kuanza tu, jiji hili lina nafasi kubwa sana kigamboni, tena huko kuna mradi wa Dar mpya ya kigamboni city, kukawa na bustani yenye hadhi huko kutaleta maana zaidi.
sasa wadau wa jiji na watanzania kwa jumla karubuni kutoa views zenu, ikiwezekana wahusika waone uzi huu wabebe hili suala wakalifanyie kazi kwa manufaa ya jiji na watu wake wa leo kasho na huko baadae, vizazi na vizazi
au kuweka public city park hapa dar nalo ni suala la kuhitaji mwekezaji wa china na misaada ya uturuki!!!!?????!!!!!!!