Wakati umepigika kazi gani ya ajabu uliwaza kufanya?

Unafaa kabi
Aisee, nakumbuka chuo boom limekata maisha magumu mno, nikafikiria nifanyaje, nikapata mawazo ya biashara nikaanza...
kuuza bubblegum/bigijii hizi super golila @500, nikanunua 8000 pakti ukiuza faida ni 5000 hivi, nashukuru ilikua tukienda class kabla lecture haijaanza nawatangangizia nnazo so wanachukua fresh,namaliza hata pkt 2 per day.

Nikaona niongeze biashara ya biscuits fulani hivi tamuu, nilikua nanunua pakti ya biscuit sh 900 nakuja kuuza 2000/=

Nikaongeza biashara ya crips za ndizi, nilikua napika mwenyewe nakumbuka nilikua nakaa hostel na hamruhusiwi kupika, so nikamuomba rafiki yangu alikua amepanga nje ya hostel nikawa napikia huko, nakumbuka siku ya kwanza nimepika crips hazikukauka vizuri dah,lainii kufika nazo hostel roommates wakanichekaa ila nilikomaa nikaziuza zingine nikawapa wale tu, siku 2, nikapika zimeungua nilikua nashindwa kukadiria moto, baada ya hapo nikawa napika vizurii, nikapeleka hadi blocks za wakaka faster zinaisha, napigiwa simu nipeleke zingine kama zipo hadi raha, faida ilikua ni nusu kwa nusu.

Nakumbuka nilikusanya faida hadi nikapata mtaji wa viatu flani vya kimasai ambao ulinisaidia hadi nilivomaliza chuo nikaendelea nao, nikafanikiwa kusave hadi sh 70,000/= per week kwa hiyo biashara,nakumbuka nilikua namsaidia hadi babe wangu vihela kidogo vya vocha,kabla hajapata kazi, japo alikuja akaniacha mfyuuu zake. Changamoto humpa mtu akili aisee.

Sent using Jamii Forums mobile app
Unafaa kabisa kuwa Mke
 
Nimeuza ubuyu chuo. Wateja dharau mingi sana. Wanakopa kulipa deni mpaka ugomvi.

Nachukua ubuyu kwa babu issa packet moja 1000, naagiza packet 100 hiyo inakua tsh 100,000/=. Plus cost ya kusafirishia 20,000/=. Nikiuza mmoja 2000/= hapo faida napata kama 80,000/= it's alot faida nzuri. Sema nlikua nauza packet moja Hadi 4 kwa siku. Biashara ilikua slow lakini nikawa sikosi pesa ya kula kila siku

Changamoto niliokutana nayo kwenye hiyo biashara kuna mama mmoja nae alikua mwanachuo, mzanzibari yeye akamwambia mume wake amnunulie ubuyu nae awe ana uza. Akaja na mbwembwe eti anauza mmoja 1500/= mimi nikienda na wangu wa 2000/= wateja wanaleta dharau mbona flani anauza bei ya chini. Nikarudi zangu maskani nikakaa kuwaza sasa next step. Pesa naitaka lakini bei sitaki kushusha. Baada ya kuwaza na kuwazua nikaona sio mbaya nikaenda supermarket nikanunua vile vikopo vina mfuniko nikaja kufanya packaging, kwenye ile packet ya 2000/= mimi nikawa natoa vikopo vitatu, kila kopo nauza buku. So nikawa napata 3000/= nikamuacha yule shoct anauza 1500/= . Biashara ni akili asiee

Nilijaribu hadi kujifunza kupika kashata, nikanunua raw material zote , nikazama utube kucheki jinsi ya kupika kashata. Aisee hii ilinishinda kashata zilikua zinatoka ngumu kama mawe. Nikaachana nazo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ukitaka kujifunza kashata na kama Bado unauhitaji njoo nikufundushe bureeeee....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
@kidukulilo akija kutoa ushuhuda wake mambo yatakuwa hivi:..

"Nimeteseka sana mimi..
Wakati nimemaliza shule pale IST nikaamua kuliko kukaa bure bora nitafute kazi
Nikaongea na mzee wangu anitafutie connection

Mzee akaniambia kuna issue canada nikasema sawa..
Nimeenda nikakuta kazi yenyewe ni kupanga mafile katika ofisi flani kwa masaa matatu kwa siku
Halafu mshahara wenyewe mdogo tu usd 300 kwa siku, nilisikitika sana...

niliteseka mimi, nyie acheni tu..

Ngoja aje humu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yaani hata mikosi ilipoanzia sijui nlijikuta nauza kila kitu changu ili kulipa madeni na kufufua baadhi ya miladi iliyokufa lakini wapi!!pesa ikiamua kwenda inakwenda hata uizuie vipi

Sent using Jamii Forums mobile app
Dah kumbe tuko wengi nilidhani ni mimi tuu, usikate tamaa mkuu. Me nimemalizwa kabisaa bora ww sasa unayo hata nafasi ya kukimbizana na wanyam wakali me nimelala tuu muda huu. Lakini usikate tamaa tafta njia mpya, zipo njia utatoka tuu me bado nina imani ndio maana sijajiua mpaka sasa? Mungu ni mmoja tu.
 
Baada ya muda mrefu kutaabika nkajikuta Sina kila kitu!yaani from hero to zero!!kitu pekee nlikua nimebaki nacho ni nyumba ila Sasa utakula nyumba?lazima maisha yaendelee! Nkauza nyumba nipate msingi Cha ajabu mtu aliyenipa wazo la biashara mpya ndie alinunua nyumba tena kwa kuilipia nusu nusu nkajikuta pesa imeisha na Niko ndani ya hiyo hiyo nyumba!!nkageuka kuwa mpangaji akaanza kuniomba Kodi ya nyumba

Sent using Jamii Forums mobile app

Daah hii kali


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maisha bwana unawexa kusema ww unahaghaika kumbe kuna wenzako wana ck mbili hawajaona kitu kinaitwa chakula ....,Mungu uguse watu wako ...wakati kuna wengine hawajui kitu kinaitwa shidah .....

Umenikumbusha mbali uwono ,nilikuwa nauoenda nikipata na mbilimbi mashalah ugali unashuka haswaa

Sent using i phone x
Wewe, kwani huwezi kuandika herufi sahihi!?
 
Mchawi wa watu wengi ni comfort zone. Ni kazi ngumu kutoka kwenye comfort zone

Sent using Jamii Forums mobile app


Mimi kuna kipindi nakua mpweke sana...yaan nna kila kitu nilichokua nawishi nipate ila sasa upweke unaniandama...kuna kpindi nilipanga nirudi nirelax...aisee huwez amini..hubby alinishangaaaa😂😂..akasema unafurah tena kuja tu ukose hela..acha ubabaifu mane...akaja yy!..ukiiweza hyo situation bas your a different person! Hakikisha unapiga chini kbs wale marafiki wasio na faida kwako(hapa ndp pananitia upweke zaid)..
 
Baada ya muda mrefu kutaabika nkajikuta Sina kila kitu!yaani from hero to zero!!kitu pekee nlikua nimebaki nacho ni nyumba ila Sasa utakula nyumba?lazima maisha yaendelee! Nkauza nyumba nipate msingi Cha ajabu mtu aliyenipa wazo la biashara mpya ndie alinunua nyumba tena kwa kuilipia nusu nusu nkajikuta pesa imeisha na Niko ndani ya hiyo hiyo nyumba!!nkageuka kuwa mpangaji akaanza kuniomba Kodi ya nyumba

Sent using Jamii Forums mobile app


Maskini ...inaumiza sana
 
Nilipokuwa chuo mwaka wa pili, bum limekata home siwezi kuomba kwani nilikuwa najisomesha mwenyewe . Nikafikiria nikaona nikipata bum nikanunue jezi niwe nauza, biashara ikakubali ikawa inanilipa, ghafla mtaji ukakakata nyumbani kulikuwa na mamatatizo ikanilazimu kusolve. Nakumbuka siku hiyo ilikuwa alhamis nili lala njaa. Ijumaa naamka njaa yaniuma vibaya Sana utumbo unawasha halafu Sina ramani ya kupata pesa.siku hiyo nikamkumbuka mungu niaksema wacha niende masjid na Leo ijumaa. Nikaenda msikiti mmoja uko town msikiti wa waarabu. Sasa bhana Yule sheikh wa pale msikitini akajichanganya akaniona mstaarabu sijui kwa kuwa navaa miwani ya macho. Akanipa bahasha ya kaki akaniomba nisimame mlangoni Ili waumini wakiingia kusali waweke sadaka kwenye Ile bahasha ya kaki. Nikasimama waumini wakioita wanaupia sadaka mpaka muda wa khotuba ulipofuka nikaenda kukaa nisikize khotuba. Happy njaa inauma utumbo na akili havikuwana ushirikiano. Utumbo unawasha, kichwani naona Kama wadudu wanatembea. Nikaenda chooni haja ndogo, nilipomaliza nikaitoa Ile bahasha kuifungua nakuta noti za 10000 za kutosha. Akili ikanambia to " Mungu ana samehe Saba mara sabini, utakufaa njaa kizembe " Sikuhesabu nikapita na misimbazi 3( 30000) nikarudi ndani msikitini .Tulipomaliza kusali fasta nikamfuata Yule sheikh nikamkabidhi bahasha yake nikamwambia nawahi chuo. Akapokea, nikatembea sikugeuka nyuma.

Mungu atusamehe kwa kweli, kupigika kubaya
Hahahahaaa watu wameshaiba hadi sadaka dadekiii
 
Mimi kuna kipindi nakua mpweke sana...yaan nna kila kitu nilichokua nawishi nipate ila sasa upweke unaniandama...kuna kpindi nilipanga nirudi nirelax...aisee huwez amini..hubby alinishangaaaa..akasema unafurah tena kuja tu ukose hela..acha ubabaifu mane...akaja yy!..ukiiweza hyo situation bas your a different person! Hakikisha unapiga chini kbs wale marafiki wasio na faida kwako(hapa ndp pananitia upweke zaid)..
Manengelo inaonesha unatatizo moja unasaka sana pesa ila kuwekeza kwenye biashara za maana kwako ni tatizo ndio maana uki relax kidogo na Pesa huna.

Fanya kuwekeza sehemu ambayo unaona Final utaishi huo mkoa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Manengelo inaonesha unatatizo moja unasaka sana pesa ila kuwekeza kwenye biashara za maana kwako ni tatizo ndio maana uki relax kidogo na Pesa huna.

Fanya kuwekeza sehemu ambayo unaona Final utaishi huo mkoa.

Sent using Jamii Forums mobile app


Siku zote best kilio changu ni kimoja..sijui nisemeje...means ukiondoka mambo yanayumba!...zinatokea sababu nyinginyingi! Nina changamoto bado mkuu!

Kuna biashara usipokuwepo inaharibika!
Yes finally tumekubaliana tuhamie Rock city ASAP!
 
Mzee wangu hadi leo sidhani kama ananipenda. Nilipokuwa form three nikakosa hela ya kutumia kabisa nikatoroka shule nikaenda kufanya kazi ya ujenzi kwa shemeji yake yaani kwenye nyumba ya kina aunt yangu. Navaa sare za shule naingia mzigoni maana ghetto kali sana afu kubwa na walianza kuweka uzio, hawana njaa hata kidogo. Niko form three na mdogo, nikapiga kazi na mafundi yule fundi mkuu akagundua niko bright akawa ananipa kazi za kusimamia saidia fundi wengine na kwenye masuala ya hesabu. Nikawa nafanya hesabu za 'grout'? na vigae vyake, matumizi ya maji na makorokoro kibao. Nikawa napata hela sema nilichubuka mikono kwa sababu ya materials tulizokuwa tunatumia na safety haikuzingatiwa. Mpaka leo mimi ni mtaalamu wa kurusha tofali kwenda juu yani hata uwe kozi ya 14 nikirusha wala husogezi mkono. Niliacha kazi baada ya kuambiwa mume wa aunt atakuja kukagua , ningeambiwa nadhalilisha familia. Hata home nishawahi kuwa saidia fundi kwa nyumba yetu, hata nilipomaliza six nilifanya kazi kampuni ya ujenzi. In short nikipigika kimbilio langu ni kwenye ujenzi. Sema ni jeuri tu ukoo wetu si wa kunifanya nife njaa.
 
Kama una kamtaji flani

Ingia kwenye real estates mdogo mdogo, uza na kununua viwanja na nyumba au kupangisha

Ndani ya miaka 5 utakuwa unakula pension kama mstaafu,

Yaani wekeza kwenye business ambazo sio lazima uwepo muda wote
Siku zote best kilio changu ni kimoja..sijui nisemeje...means ukiondoka mambo yanayumba!...zinatokea sababu nyinginyingi! Nina changamoto bado mkuu!

Kuna biashara usipokuwepo inaharibika!
Yes finally tumekubaliana tuhamie Rock city ASAP!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom