Wakati umepigika kazi gani ya ajabu uliwaza kufanya?

ANKO JEI

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2018
Messages
541
Points
1,000

ANKO JEI

JF-Expert Member
Joined Jul 21, 2018
541 1,000
Habari za muda huu wakuu, naimani mko poa na January inaendelea kuyoyoma. Naomba niende moja kwa moja kwenye swali langu.

Kwanza kabisa lazima tukubali kuna muda mtu unapigika na life hadi unaanza kuwaza kazi za ajabu au ambazo hukuwahi dhani utayafanya. Wengine wanafikia maamuzi na wanafanya, na wengine wanaishia kuwaza tu na kabla hawajafanya wanabadili maamuzi au wanapaka kazi nyingine ya kawaida.

Binafsi wakati nimemaliza elimu yangu ya hali ya juu Dar es salaam nilipitia wakati mgumu sana kimaisha kwani sikuwa na wakumtegemea. Nilikuwa napenda sana kuingia JF kujipotezea mawazo.

Siku moja nikakutana na uzi wa jamaa fulani akidai kuwa amepata mchongo wa kuigiza video za kikubwa huko majuu na akadai kuwa yeyote atayehitaji yupo tayari kumuunganishia.

Kiukweli nimelelewa vizuri tu lakini ilibaki kidogo tu nimtafute jamaa aniconnect nizame majuu. Lakini huwa napenda kufanya utafuti wa jambo kabla halijafanyika, hivyo nikazama Google kutafuta undani wa industry ya video za kikubwa.

Nikafahamu mengi sana, faida na hasara, gharama wanazolipa na mambo kibao, mwisho wa siku sauti ndani yangu ikawa inakataa sana hizo shughuli, basi nikaacha nikapambana kutafuta ishu nyingine.

Je wewe ni kazi gani ya ajabu kwako ulifikiria kuifanya kipindi ukiwa huna kazi na life limekunyoosha.

Karibuni.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pendael24

JF-Expert Member
Joined
Feb 13, 2014
Messages
2,584
Points
2,000

Pendael24

JF-Expert Member
Joined Feb 13, 2014
2,584 2,000
2011 ilivyostishwa kazi yangu ktk kampuni nilipigika sana nikaamua kukimbilia katika kisiwa kimoja kilichopo ziwa victoria (Ikuza) nikiwa huko nilijikuta nimefanya kazi ambayo ni tamaa ya pesa

niliingia ktk hifadhi taifa ya rubondokinyume na taratibu kwenda kutega samaki usku wa manane nikiwa mgeni mimi pekee wenzangu walikua wenyeji siku nyingi walikua wakiingia ikiwa ndio malayangu ya tatu kuingia tulikamatwa na watu wa dolia gemu

kipondo tulichopewa ni cha mbwa koko miaka mi3jera hadi leo mguu wangu wa kulia una hitilafu

Sent using Jamii Forums mobile app
Pole sana ndugu yangu, haya maisha bwana!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pendael24

JF-Expert Member
Joined
Feb 13, 2014
Messages
2,584
Points
2,000

Pendael24

JF-Expert Member
Joined Feb 13, 2014
2,584 2,000
Aisee, nakumbuka chuo boom limekata maisha magumu mno, nikafikiria nifanyaje, nikapata mawazo ya biashara nikaanza...
kuuza bubblegum/bigijii hizi super golila @500, nikanunua 8000 pakti ukiuza faida ni 5000 hivi, nashukuru ilikua tukienda class kabla lecture haijaanza nawatangangizia nnazo so wanachukua fresh,namaliza hata pkt 2 per day.

Nikaona niongeze biashara ya biscuits fulani hivi tamuu, nilikua nanunua pakti ya biscuit sh 900 nakuja kuuza 2000/=

Nikaongeza biashara ya crips za ndizi, nilikua napika mwenyewe nakumbuka nilikua nakaa hostel na hamruhusiwi kupika, so nikamuomba rafiki yangu alikua amepanga nje ya hostel nikawa napikia huko, nakumbuka siku ya kwanza nimepika crips hazikukauka vizuri dah,lainii kufika nazo hostel roommates wakanichekaa ila nilikomaa nikaziuza zingine nikawapa wale tu, siku 2, nikapika zimeungua nilikua nashindwa kukadiria moto, baada ya hapo nikawa napika vizurii, nikapeleka hadi blocks za wakaka faster zinaisha, napigiwa simu nipeleke zingine kama zipo hadi raha, faida ilikua ni nusu kwa nusu.

Nakumbuka nilikusanya faida hadi nikapata mtaji wa viatu flani vya kimasai ambao ulinisaidia hadi nilivomaliza chuo nikaendelea nao, nikafanikiwa kusave hadi sh 70,000/= per week kwa hiyo biashara,nakumbuka nilikua namsaidia hadi babe wangu vihela kidogo vya vocha,kabla hajapata kazi, japo alikuja akaniacha mfyuuu zake. Changamoto humpa mtu akili aisee.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hamna kitu nisichopenda kama kuachana, tatizo sijui tunakosea kupata watu sahihi ama vipi misijui!!!
Lakini pongezi nyingi mkuu naweza kusema ni moja kati ya wapambanaji wachache naamini upo mbali sana kimaendeleo kwa sasa nakutakia heri.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
faokipe

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2015
Messages
695
Points
1,000

faokipe

JF-Expert Member
Joined Jan 20, 2015
695 1,000
Mm nimetoka skuli moja kwa Moja nkaanza mishe ,na nkapata pesa nzuri,nkaoa nkajenga nyumba nzuri tu!!yaani nkiwa bado 23 yrs nlikua nshamaliza kua na kila kitu ambacho kijana wa kisasa anatani kua nacho!!
Mikosi ilianza baada ya kuacha kazi baada ya kuzinguana na boss ,nkaona hizi kazi ,za kumnyenyekea mwanaume mwenzangu siwezi nkaanza maisha ya biashara wajanja Wakanipiga pesa ndefu kwenye madini !!
Nkakimbilia mwanza nkaanzisha kambi ya uvuvi nkawa fresh pesa ikakubali hatari !!kumbe zile shuguli Zina ushirikina sijapata kuona!!baada ya muda was miaka 6 ya kua kwenye uvuvi nlijikuta Nina madeni kila Kona!!hakuna kitu kibaya Kama madeni unakua mtumwa na unakua muoga (nidhamu)ya uoga

Sent using Jamii Forums mobile app
 
faokipe

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2015
Messages
695
Points
1,000

faokipe

JF-Expert Member
Joined Jan 20, 2015
695 1,000
Baada ya muda mrefu kutaabika nkajikuta Sina kila kitu!yaani from hero to zero!!kitu pekee nlikua nimebaki nacho ni nyumba ila Sasa utakula nyumba?lazima maisha yaendelee! Nkauza nyumba nipate msingi Cha ajabu mtu aliyenipa wazo la biashara mpya ndie alinunua nyumba tena kwa kuilipia nusu nusu nkajikuta pesa imeisha na Niko ndani ya hiyo hiyo nyumba!!nkageuka kuwa mpangaji akaanza kuniomba Kodi ya nyumba

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bhagavan

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2017
Messages
1,490
Points
2,000

Bhagavan

JF-Expert Member
Joined Oct 28, 2017
1,490 2,000
Nilipokuwa chuo mwaka wa pili, bum limekata home siwezi kuomba kwani nilikuwa najisomesha mwenyewe . Nikafikiria nikaona nikipata bum nikanunue jezi niwe nauza, biashara ikakubali ikawa inanilipa, ghafla mtaji ukakakata nyumbani kulikuwa na mamatatizo ikanilazimu kusolve. Nakumbuka siku hiyo ilikuwa alhamis nili lala njaa. Ijumaa naamka njaa yaniuma vibaya Sana utumbo unawasha halafu Sina ramani ya kupata pesa.siku hiyo nikamkumbuka mungu niaksema wacha niende masjid na Leo ijumaa. Nikaenda msikiti mmoja uko town msikiti wa waarabu. Sasa bhana Yule sheikh wa pale msikitini akajichanganya akaniona mstaarabu sijui kwa kuwa navaa miwani ya macho. Akanipa bahasha ya kaki akaniomba nisimame mlangoni Ili waumini wakiingia kusali waweke sadaka kwenye Ile bahasha ya kaki. Nikasimama waumini wakioita wanaupia sadaka mpaka muda wa khotuba ulipofuka nikaenda kukaa nisikize khotuba. Happy njaa inauma utumbo na akili havikuwana ushirikiano. Utumbo unawasha, kichwani naona Kama wadudu wanatembea. Nikaenda chooni haja ndogo, nilipomaliza nikaitoa Ile bahasha kuifungua nakuta noti za 10000 za kutosha. Akili ikanambia to " Mungu ana samehe Saba mara sabini, utakufaa njaa kizembe " Sikuhesabu nikapita na misimbazi 3( 30000) nikarudi ndani msikitini .Tulipomaliza kusali fasta nikamfuata Yule sheikh nikamkabidhi bahasha yake nikamwambia nawahi chuo. Akapokea, nikatembea sikugeuka nyuma.

Mungu atusamehe kwa kweli, kupigika kubaya
 
rip faza_nelly

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2018
Messages
2,661
Points
2,000

rip faza_nelly

JF-Expert Member
Joined Feb 19, 2018
2,661 2,000
Allah akbar

Danpol

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2013
Messages
3,328
Points
2,000

Danpol

JF-Expert Member
Joined Aug 15, 2013
3,328 2,000

Duuh

Sent using Jamii Forums mobile app
 
GIRITA

JF-Expert Member
Joined
Jul 4, 2016
Messages
1,332
Points
2,000

GIRITA

JF-Expert Member
Joined Jul 4, 2016
1,332 2,000

Mungu aliamua kukupima imani yako,matekeo ya mtihani ukaangukia pua,kama uliomba toba mungu atakusamehe.....unatakiwa uwe muumini Wa kweli sasa Wa kuswali sana na kufuga uchebe!!!
 
feyzal

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2016
Messages
2,257
Points
2,000

feyzal

JF-Expert Member
Joined Apr 20, 2016
2,257 2,000

Forum statistics

Threads 1,389,939
Members 528,059
Posts 34,039,264
Top