Wakati umefika wananchi wasaidie wabunge wanaonyanyaswa

Mshangai

JF-Expert Member
Feb 16, 2008
468
1,086
Imekuwa ni tabia ya kuwaonea wabunge watetezi wa wananchi kupitia kiti cha spika au wabunge wa ccm kwa wingi wao.

Hivi kitendo cha Mnyika kutupwa nje ya Bunge namna ile kwa kutaka mwongozo wa jike moja lililomwita "mwizi' ni sawa? Kisha anatolewa na wabunge wa ccm wanashangilia ni sahihi?
Wakazi wa Kibamba wanaojua juhudi za Mnyika kuwapigania mambo mengi hasa hili suala la kuvunjiwa Nyumba wanajisikiaje kama sio chuki?

Sasa wananchi wawasaidie wabunge wao ili wasijione kama yatima kwa kusema kwao kweli, wawashikishe adabu Spika kila apitapo kwa kumzomea au kumuonyesha ishara za kuuzi. Wabunge nao wa ccm wafundishwe adabu kwa njia hizo hizo mbele ya jamii ili wajue kuwa watendayo hayana baraka za wananchi.

Mkapa aliwahi kufanyiwa hivyo mpaka serikali ikaingilia kati kubembeleza kuwa sio jambo zuri.
Yaweza onekana kama wazo LA kihuni, lakini Mbunge atakapo jikuta yuko na familia yake na kukumbana na hali hiyo ndio atajua ujinga ule wa bungeni ni wa kuacha.

Ndio msaada pekee wa kuwasaidia wale " yatima" wapambanaji ili wasikate tamaa kwa wanayotendewa.
 
kuna wakati unaweza kutamani kucheka au kulia ukashindwa, basi unabaki kuduwaa tu, katika masuala haya ya siasa yanatakiwa kutengwa na hoja za utetezi wa jambo lolote lenye manufaa kwa wanachi
 
Wabunge wa CCM wanajua wazi kuwa kilio kikubwa cha wabunge wa upinzani ni mikataba mibovu ya madini yetu ambayo inanufaisha kampuni za kigeni kuliko nchi yetu.

Wakati wote huo wabunge wa CCM wamekuwa wakiwapuuza wabunge wa upinzani na kuwaita wazushi na wakawa wanatuhakikishia wananchi kuwa mikataba hiyo ipo perfect by 100%

Hivi sasa baada ya Mwenyekiti wao wa CCM Magufuli kusema kuwa mikataba hiyo ya madini ni mibovu na kama nchi tunaibiwa, wabunge hao hao wa CCM wanamshangilia Mwenyekiti wao na hivi sasa wanawaita wabunge wa upinzani eti ndiyo wanaowatetea wezi hao wa makanikia!

Hivi katika mazingira hayo tujaribu kuwa wakweli bila kuweka ushabiki wa vyama, hivi ni wabunge wapi haswa wanaopaswa kupimwa akili zao, hivi ni wa CCM au wa upinzani?
 
Imekuwa ni tabia ya kuwaonea wabunge watetezi wa wananchi kupitia kiti cha spika au wabunge wa ccm kwa wingi wao.
Hivi kitendo cha Mnyika kutupwa nje ya Bunge namna ile kwa kutaka mwongozo wa jike moja lililomwita "mwizi' ni sawa? Kisha anatolewa na wabunge wa ccm wanashangilia ni sahihi?
Wakazi wa Kibamba wanaojua juhudi za Mnyika kuwapigania mambo mengi hasa hili suala la kuvunjiwa Nyumba wanajisikiaje kama sio chuki?
Sasa wananchi wawasaidie wabunge wao ili wasijione kama yatima kwa kusema kwao kweli, wawashikishe adabu Spika kila apitapo kwa kumzomea au kumuonyesha ishara za kuuzi. Wabunge nao wa ccm wafundishwe adabu kwa njia hizo hizo mbele ya jamii ili wajue kuwa watendayo hayana baraka za wananchi.
Mkapa aliwahi kufanyiwa hivyo mpaka serikali ikaingilia kati kubembeleza kuwa sio jambo zuri.
Yaweza onekana kama wazo LA kihuni, lakini Mbunge atakapo jikuta yuko na familia yake na kukumbana na hali hiyo ndio atajua ujinga ule wa bungeni ni wa kuacha.
Ndio msaada pekee wa kuwasaidia wale " yatima" wapambanaji ili wasikate tamaa kwa wanayotendewa.
Hayo ni Machadema acha yapigwe yanahongwa na ACCACIA ili madini yetu yatoroshwe !!!
 
Hivi wananchi na wabunge nani ananyanyasika?
Mtoa mada inabidi ututake radhi,kunyanyasika huku unaingiza laki tatu kwa siku,wakati mwananchi haingizi hata 500
Mtu kama Mnyika ni vizuri hata angen'golewa jino moja ili awe na adabu
 
Na : Dotto Bulendu

Hili bunge hili nalo linataka tuliamini kwenye sakata la madini nchini kwetu?liaminiwe kwa lipi?

1.Ni mhimili huu huu mwaka 1997,ulipitisha kwa dharura sheria mbili,ile ya kodi na ya uwekezaji,sheria zilizohalalisha wawekezaji kukwapu madini yetu,sheria ambazo zilifuta kodi nyingi kwenye sekta ya madini,mhimili huu huu ukiitika ndiyooo,kuhalalisha wawekezaji kusamehewa na kufutiwa kodi!.

2.Ni hawa hawa mwaka 2007,walimfukuza bungeni Zitto Kabwe baada ya kutaka ufanyike uchunguzi kwenye mkataba kati serikali na huyuhuyu Acacia wakati huo akiitwa Barrick,hawahawa walitetea huo mkataba uliowaruhusu Barrick kusafirisha haya Makinikia,hawahawa walikataa waziri aliyesaini mkataba huo asijadiliwe bungeni na kumuadhibu aliyeibua hoja kuhusu Mkataba huo ulioidhinisha wana Kahama wafukuzwe kwenye maeneo yao kuwapisha hawa Acacia!.

Tena waliotetea mkataba huu uliovuja mpaka kwenye vyombo vya habari,baadhi yao bado wamo bungeni,wengine ni viongozi bungeni!.

3.Ni hawa hawa,na wengine wamo bungeni tena ni viongozi,mwaka 2010 waliitetea sheria ya madini na kupiga kura za ndiyooo sheria hii inayowapunja wazawa kwenye malipo ya fidia baada ya kuhamishwa kupisha wawekezaji wakiwemo Acacia!.

Hii sheria ya ajabu inayosema eti mtanzania yeye anamiliki sehemu ya juu ya ardhi ,huko chini siyo mali yake,ni mhimili huu huu ndiyo mwaka 2010 ulitunga sheria ya kuwafanya watu wanaoishi pembezoni mwa migodi wawe masikini wa kutupwa pamoja na kuishi sehemu yenye utajiri!

4.Ni mhimili huu huu,mwaka 2009,ukifumbua macho unyama wa Barrick pale wananchi wa Nyamongo walipotiririshiwa sumu,baadhi wakababuka,wengine wakapoteza maisha,mifugo ikafa,ardhi ikachafuliwa na sumu,mhimili huu huu uliunda kamati mwaka 2009,kamati ambayo mwisho wa siku iliwakumbatia wawekezaji na kuwaita waathirika wa sumu kuwa ni wavamizi/wizi,kinachonidikitisha baadhi ya wajumbe wa kamati ile bado wamo bungeni,waliwasaliti wana wa wanyongo kwa kuwaambia wamejitakia kwa kuwavania wawekezaji,leo wanaidai kuongea kwa hasira wakati mwaka 2009 waliwasaliti watanzania na kuwatetea wawekesaji,leo wanataka tuwaone vinara wa kwenye wizi huu wa madini!.

5.Mwaka 2004,watanzania waliokuwa wanaishi kijiji cha Mtakuja,wakihamishwa kinyama,usiku wa manane,kamati ya mhimili huu ilikwenda Geita,ikashuhudia watanzania wakiishi kwenye jengo chakavu la mahakama eneo la Sofia town,baadhi yao mpaka leo wamo bungeni,walifumbia macho unyama huu,waliwaita watu wa mtakuja wavamizi,leo wanataka tuwaamini kuwa wana uchungu na wizi huu!.

6.Hivi hawa wabunge hawajui chochote kinachoendelea Geita?hawajui kinachoendelea Nyamongo ,hawajui kinachoendelea Mererani?.Wanasubiri nani aseme kinachoendelea huko?je wao wanachojua ni makinikia tu?

7.Huu mhimili huu umekaa kimya miaka yote,kamati ya Bomani,kamati ya Lau,kamati ziliundwa zaidi ya tatu kabla ya hii,ripoti mbali mbali zimetoka zikithibitisha uporwaji wa mali zetu,huu mhimili ulikuwa unatazama tu,nakumbuka baada ya mto Tigithe kumwagiwa sumu,kamati ya viongozi wa dini iliinda timu ya wataalam kuchunguza kama kweli mto tigithe ulichafuliwa na sumu kutoka Barrick,ripoti ilitoka,ikathibitisha kuwa mto ulichafuliwa na sumu,huu mhimili kimyaaaaa,haukuwahi hata itumia tafiti hiyo kusaka haki ya waathirika wa sumu za Tigithe!.

8.Ni mhimili huu huu ndiyo ulitunga sheria ya sisi kupata mrahaba/mrabaha wa asilimi 4 tu,ni hawa hawa walipitisha sheria hii,sasa wanataka tuwaamini kwa lipi?

Mhimili huu ujitafakari unapojadili mambo mazito ya nchi hii,ujipime uzalendo wake,ujipime uwezo wake kuisimamia serikali,ujipime uwezo wake kuwawakilisha watanzania!.

Huu mhimili huu?any way!usiku mwema!.
 
Imekuwa ni tabia ya kuwaonea wabunge watetezi wa wananchi kupitia kiti cha spika au wabunge wa ccm kwa wingi wao.
Hivi kitendo cha Mnyika kutupwa nje ya Bunge namna ile kwa kutaka mwongozo wa jike moja lililomwita "mwizi' ni sawa? Kisha anatolewa na wabunge wa ccm wanashangilia ni sahihi?
Wakazi wa Kibamba wanaojua juhudi za Mnyika kuwapigania mambo mengi hasa hili suala la kuvunjiwa Nyumba wanajisikiaje kama sio chuki?
Sasa wananchi wawasaidie wabunge wao ili wasijione kama yatima kwa kusema kwao kweli, wawashikishe adabu Spika kila apitapo kwa kumzomea au kumuonyesha ishara za kuuzi. Wabunge nao wa ccm wafundishwe adabu kwa njia hizo hizo mbele ya jamii ili wajue kuwa watendayo hayana baraka za wananchi.
Mkapa aliwahi kufanyiwa hivyo mpaka serikali ikaingilia kati kubembeleza kuwa sio jambo zuri.
Yaweza onekana kama wazo LA kihuni, lakini Mbunge atakapo jikuta yuko na familia yake na kukumbana na hali hiyo ndio atajua ujinga ule wa bungeni ni wa kuacha.
Ndio msaada pekee wa kuwasaidia wale " yatima" wapambanaji ili wasikate tamaa kwa wanayotendewa.

Utoto unawasumbua mwenye akili kubwa mlimwita majina ya kejeli mmebaki watoto watupu.Mnyika aliomba mwongozo wa spika badala ya kufanya alichoomba akadandia hoja ya mhuni anayewamudu Lusinde a.k.a Kibajaji akaambiwa na spika kaa chini mwenye nafasi aendelee anaendelea kubishana na spika

Rudisheni baba wa akili kubwa Dr.W.Slaa awarudishe kina Mnyika na Lisu relini wamepotoshwa na mliowatusi hawajui hata hoja za kuzitetea.

Tulia mlidai anawaonea tukauliza wanaume wazima mnakimbiaje hoja za mwanamke bungeni mkadai mnamtaka Ndugai,kawazidishia deko mnataka kumshika kidevu.Pole Mnyika,umepeleka wapi akili yako nzuri ya awali?
 
Wanachi wenyewe ni waoga balaa
Mkuu si woga tu bali wamejaa unafiki na uzandiki! hawana makuu wakipewa t-shirt bila nguo ya kustiri maungo nyeti na chumvi bila mboga aaah maisha ni murua miluzi na nyimbo kwa sauti pana!!
 
Utoto unawasumbua mwenye akili kubwa mlimwita majina ya kejeli mmebaki watoto watupu.Mnyika aliomba mwongozo wa spika badala ya kufanya alichoomba akadandia hoja ya mhuni anayewamudu Lusinde a.k.a Kibajaji akaambiwa na spika kaa chini mwenye nafasi aendelee anaendelea kubishana na spika

Rudisheni baba wa akili kubwa Dr.W.Slaa awarudishe kina Mnyika na Lisu relini wamepotoshwa na mliowatusi hawajui hata hoja za kuzitetea.

Tulia mlidai anawaonea tukauliza wanaume wazima mnakimbiaje hoja za mwanamke bungeni mkadai mnamtaka Ndugai,kawazidishia deko mnataka kumshika kidevu.Pole Mnyika,umepeleka wapi akili yako nzuri ya awali?
Nyie kweli wazee kinyonga. Kama mnavyoweza kusema Leo Mnyika mwizi wa dhahabu hatushangai Dr Slaa mliyemwita Dr wa Canon asiyejua kitu Leo mnasema akili kubwa. Mnahitaji maombi nyie
 
Back
Top Bottom