Wakati umefika sasa umefika tubadilishe wimbo wetu wa taifa

Tulimumu

JF-Expert Member
Mar 11, 2013
14,305
12,968
Baada ya kusoma makala mbali mbali za historia ya wimbo wimbo wa taifa tunaoutumia, nimeshawishika kutoa pendekezo sasa mamlaka husika kufikiria kubadisha wimbo wetu wa taifa kutoka huu wa sasa tulioukopi na kupest kutoka Afrika ya Kusini na kuwa na wetu wenyewe kama wenzetu wa nchi nyingine kama Zimbabwe walivyofanya baada ya miaka kadhaa ya uhuru wakabadili wimbo wao kutoka huo unaofanana na wa Afrika ya kusini.

Kwa kuzingatia makala hii hapa chini mimi napendekeza hata kama hatuwezi kutunga mwingine, basi tutumie huu wa TANZANIA TANZANIA NAKUPENDA KWA MOYO WOTE. Huu ni wimbo rahisi sana kuimbika na mirindimo yake ni mizuri. Vile vile wimbo huu unaoonesha uzalendo kwa nchi. Baada ya miaka zaidi ya 50 ya uhuru bado tunatumia wimbo wa taifa wa kukopi ni aibu!

Nukuu:
"Historia ya Wimbo wa Taifa wa Tanzania na mtunzi wake.

Wimbo huo Ulitungwa na Enoch Sontonga ,
Alizaliwa mwaka : 1873, Uitenhage, Eastern Cape, South Africa
Alifariki mwaka: April 18, 1905, Johannesburg, South Africa
Mkosa (a Xhosa), wa Afrika Kusini.

Wimbo huo, Nkosi Sikelel' iAfrika, yaani "God Bless Africa," ni wimbo wa taifa letu la Tanzania na la Zambia.

Pia ulikuwa ni "wimbo wa taifa" wa African National Congress (ANC) walipokuwa wanapambana na wakandamizaji wao Makaburu. Na bado unatumika katika nchi hiyo ya Afrika Kusini. Sehemu za wimbo huo pia ziko katika wimbo wa taifa wa nchi ya Afrika Kusini.
Kwahiyo ni wimbo wa taifa wa nchi tatu: Tanzania, Zambia, na South Africa.

Umeimbwa pia katika nchi zingine, kwa mfano Zimbabwe na Namibia, na labda hata Botswana, Lesotho Swaziland, na Malawi kwa miaka mingi.
It has been one of the most inspiring songs in the struggle for freedom on our continent. It's considered to be a classic.

Hata kabla ya TANU (Tanganyika African National Union) kuanzishwa mwaka wa 1954, wimbo huo, Nkosi Sikelel' iAfrika, ulikuwa unaimbwa Afrika Kusini.

Chama cha Afrika Kusini, African National Congress (ANC), kilianzishwa miaka mingi kabla ya chama chetu cha TANU. Na kwenye mkutano wa kwanza uliofanyika Bloemfontein, South Africa, kuanzisha chama hicho mwaka wa 1912, waliimba Nkosi Sikelel' iAfrika. Nyerere alikuwa bado hajazaliwa. Na Hatukuwa na chama cha TANU miaka ile.

Chama cha kule Afrika Kusini kilichoanzishwa mwaka wa 1912 kiliitwa South African Native Congress chini ya uongozi wa John Dube, Mzulu, na Pixley ka I. Seme pia kutoka Natal kama Dube. Kikabadilishwa jina baadaye na kuitwa African National Congress (ANC).

Kuanzia mwaka wa 1925, wana ANC waliuchagua wimbo huo, Nkosi Sikelel' iAfrika, kama wimbo wao wa taifa. Na bado unaimbwa leo.

Katika nyimbo za mataifa yetu ya Kiafrika, hakuna wimbo mwingine unaojulikana kama wimbo huo. Hata katika nchi za Afrika Magharibi, watu wengi wanajua Nkosi Sikelel' iAfrika ni wimbo gani na unamaanisha nini.
Watu wangapi nchi mbali mbali katika bara letu wanajua jina la wimbo wa taifa wa nchi ya Ghana ingawa ilikuwa ni nchi ya kwanza kupata uhuru miongoni mwa nchi zetu kusini ya jangwa la Sahara? Wangapi wanajua jina la wimbo wa taifa wa nchi ya Nigeria, nchi kubwa inayojulikana sana? Lakini ukienda huko, utawakuta wanaosema wanajua kuhusu Nkosi Sikelel' iAfrika.

Ndiyo maana hata Kenya wanaimba wimbo huo. Unaimbwa na unafahamika katika nchi nyingi katika bara letu hata kaskazini ya bara hili. Ukienda Egypt, Algeria na nchi zingine huko, utawakuta watu wengi wanaojua kuhusu Nkosi Sikelel' iAfrika. Wangapi katika nchi zingine za Kiafrika wanajua kuhusu wimbo wa taifa wa Uganda, au Malawi, au Burkina Faso? Lakini waulize kuhusu Nkosi Sikelel' iAfrika. Utawapata wengi waliousikia wimbo huo.

Enoch Sontonga alitoka Eastern Cape Province, jimbo la Wakosa (Xhosa), ambako pia ni nyumbani kwa Mandela. Alitunga wimbo huo katika lugha yake ya Kikosa na alitunga kama wimbo wa kanisa.

Alipotunga wimbo huo mwaka wa 1897, haukuimbwa hadharani mpaka mwaka wa 1899. Uliimbwa kanisani kwa mara ya kwanza mwaka huo. Halafu, baada ya miaka kumi na tatu, uliimbwa kwenye mkutano wa kwanza wa South African Native Congress mwaka wa 1912 uliofanyika Bloemfontein kuanzisha chama hicho kugombea haki za Wafrika.

Hata Watanganyika wengi waliokwenda kufanya kazi migodini Afrika Kusini miaka ya 1940s na 1950s waliujua wimbo huo. Walikuwa wanaimba Nkosi Sikelel' iAfrika pamoja na watu wa Afrika Kusini walipokuwa huko na waliporudi Tanganyika. Ninawafahamu wengi wao.

Na nina hakika kuna Watanganyika wengi, mara tu tulipopata uhuru, waliokuwa au walioziona music sheets za wimbo huo nchini Tanganyika. Na ikiwa kuna ambao bado wanazo music sheets hizo, wanaweza kukuonyesha jina la Enoch Sontonga kama ndiyo mtungaji wa wimbo huo.
Nakumbuka sana nililiona jina lake kwenye music sheet hiyo kwa sababu hata mimi nilikuwa nayo. Na si mimi tu niliyekuwa nayo au niliyeiona music sheet hiyo ya wimbo huo. Ilikuwa katika lugha mbili, Kiswahili na Kiingereza, na kichwa chake kilikuwa ni Mungu Ibariki Afrika, God Bless Africa, yaani Nkosi Sikelel' iAfrika.

Melody ya Nkosi Sikelel' iAfrika ilitungwa na Enoch Sontonga. Ukiisikiliza melody hiyo, hakuna tofauti hata kidogo na melody ya wimbo wetu wa taifa, Mungi Ibariki Afrika, au melody ya wimbo wa taifa kule Zambia. Sikiliza wimbo huo Youtube ambao mmoja wa waimbaji wake katika video ni Miriam Makeba. Pia lyrics za Nkosi Sikelel' iAfrika ziliandikwa na Enoch Sontonga, ingawa wimbo wetu una lyrics zake sehemu mbali mbali. Lakini chanzo chake ni wimbo uliotungwa na Enoch Sontonga: Nkosi Sikelel' iAfrika.

Kama nilivyosema kabla ya hapa, wimbo huo siyo wa watu wa Afrika Kusini tu. Enoch Sontonga aliandika na alitunga wimbo huo kama ni wimbo wa bara lote. Ndiyo maana alisema Nkosi Sikelel' iAfrika, God Bless Africa, na siyo God Bless South Africa.

Nyimbo zake nyingi zilikuwa ni nyimbo za huzuni kuhusu maisha magumu ya Wafrika chini ya utawala wa Wazungu waliokuwa wanawakandamiza Wafrika katika bara lote. Wimbo wake, Nkosi Sikelel' iAfrika, ulitokana na maumivu hayo ya Wafrika ingawa pia ulikuwa ni wimbo wa kuwapa tumaini kwamba hawako peke yao. Mungu yuko nao, au yuko nasi, ingawa tunaumia na tunateswa na wanao tutawala kutoka nchi za Ulaya.

Wimbo huo, Nkosi Sikelel' iAfrika, uliwekwa kwenye sahani ya santuri kwa mara ya kwanza, London, mwaka wa 1923. Uliimbwa na Solomon Plaatje, mwimbaji maarafu wa Afrika Kusini ambaye pia alikuwa ni mmoja wa Wafrika walioanzisha chama cha South African Native Congress, Bloemfontein, South Africa, mwaka wa 1912.

Ni wimbo wetu pia kwa sababu Afrika ni moja. Ndiyo maana Enoch Sontonga alitunga wimbo unaosema Nkosi Sikelel' iAfrika - God Bless Africa.

Kwahiyo hatukuiba, na hatukuazima, wimbo huo. Ni wetu kama wao kule Afrika Kusini na nchi zingine. Na Enoch Sontonga alipewa full credit kwenye music sheets za wimbo huo nchini Tanganyika, na baadayeTanzania, kama ndiyo mtungaji wa God Bless Africa.

Miaka yote hii, tangu nilipokuwa kijana mdogo miaka ya 1960s, nimejua kwamba wimbo huo ulitungwa na Enoch Sontonga kutoka Afrika Kusini. Kuna Watanzania wengine wanaojua ukweli huo. Si mimi tu.

Utumizi wetu wa wimbo huo, ambao pia ni wimbo wa taifa, Zambia, unaonyesha pia umoja na undugu wetu kama Wafrika. Ndiyo maana kulikuwa hata vyama vilivyopigania uhuru ambavyo majina yao yalifanana au yalikuwa karibu sana. Kwa mfano, African National Congress (ANC) iliyoundwa Tanganyika na kuongozwa na Zuberi Mtemvu na katibu wake mkuu John Chipaka ilikuwa na jina sawa na la chama cha Africa Kusini cha akina Mandela na wenzake.

Pia chama cha kwanza kupigania uhuru Northern Rhodesia kilicho ongozwa na Harry Nkumbula kilikuwa kinaitwa African National Congress, na kiliendelea kuitwa hivyo hata baada ya wanachama wengine waliondoka na kuunda chama kingine, United National Independence Party (UNIP), chini ya uongozi wa Kenneth Kaunda.
Kenya kulikuwa na Kenya African Union (KAU) kabla ya Tanganyika African National Union. Baadaye KAU ikabadili jina kidogo na kuitwa KANU. Na ndugu zetu Zimbabwe waliunda chama kinachoitwa ZANU baada ya baadhi yao, pamoja na Robert Mugabe, kuondoka na kuachana na ZAPU.

Majina hayo, katika nchi zetu mbali mbali, yanafanana kwa sababu tunajiona kama ni ndugu, na ni kweli sisi sote ni ndugu. Pia inaonyesha ushirikiano wetu. Hata Uganda, jeshi lao ni Uganda People's Defence Forces (UPDF), jina linalotokana na jina la jeshi letu: Tanzania People's Defence Forces (TPDF).

Ni sawa na wimbo wa Nkosi Sikelel' iAfrika kuwa wimbo wa taifa Tanzania, Zambia, na South Africa.
Africa ni moja. Sisi sote ni ndugu bila kujali ukabila, rangi, dini, au asili.
Mungi Ibariki Afrika. Nkosi Sikelel' iAfrika



12802706_1105012329523679_3931301953924678038_n.jpg
 
Nchi ina mambo mengi ya kufanya katika kipindi hiki. Unatuletea hoja ambazo wakifanya hata wajukuu zetu haina madhara kiuchumi.

Nimekuwa wa kwanza kujibu
 
Huo wa Tanzanian Tanzania nakupenda kwa moyo wote nao tulikopi na kupesti kutoka china
 
Ingekuwa vizuri huu wimbo wa Taifa uendelee kupigwa na ikiwezekana nchi zote za SADC ziuimbe.

Bado tupo kwenye ukoloni wa mtu mweusi.
 
Huu wimbo ni kiwakilishi cha umoja wa africa. Kama unadhani unaweza kutunga wimbo wa kwako peke yako, unajidanganya. Wapare wana methali, hakuna ambacho hujakiona, utakuwa tu umesahau.
 
hoja ninzuri lakini Tunasisita upendo na umoja wa wanaafrika ,mtunzi ni mwafrika na nchi zote za Afrika lazima tumuenzi kwani maudhii take ni mazurir
 
Tulimumu katupa historia ya Waafrika na jinsi walivyoanza kuunda vyama vya siasa vya ukombozi kutoka makucha ya ukoloni na hakuna haja kabisa ya kubadilisha wimbo wa taifa since that does not show/indicate development ila ni jinsi ya kudharau mazuri ya wazee wetu wa zamani! Ni vema pawe na pendekezo la kuwa na Africa moja na wimbo mmoja na not just simple amendments which are just valueless. Walianza na Afrika ikiwa vipande vipande sasa sisi tuwe na Africa ya kweli and not to put what was achieved by our old learned friends and put their achievements asunder!
 
Naona unawatafutia watu fursa ya kupia hela.

Maana utasikia sasa ndii tumeunda kamati ya kutafuta wimbo mpya, hivyo mchakato huo utachukua miezi 9.

Hiyo kamati ukute ina watu 30 piga sasa posho zao za malazi, usafiri na mishahara yao.

Tubaki tu na wimbo wetu huu huu.
 
Huu wimbo ni kiwakilishi cha umoja wa africa. Kama unadhani unaweza kutunga wimbo wa kwako peke yako, unajidanganya. Wapare wana methali, hakuna ambacho hujakiona, utakuwa tu umesahau.
Huu msemo nimeupenda
 
Mbona historia inanivutia kwa wimbo kubaki wa Taifa letu. Naupenda, historia naipenda na uzidi kudumu daima na daima
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom