Wakati umefika kwa Serikali kubadili Noti

Fursa Pesa

JF-Expert Member
May 30, 2012
4,431
3,250
Nilikuwa nafikiri kama itaonekana inafaa kwa serikali kutengeneza noti mpya, sijui wadau wa Uchumi wanaonaje?
Nini faida na hasara iwapo serikali itaamua kuleta Noti mpya?
 
Mkuu zibadilishwe kwa sababu ipi..? Je hazina ubora au sababu ni nini..? Unaweza kuwa na hoja nzuri tena yenye kujenga, hebu funguka Mkuu.
 
Sasa mtu hajui kwanini zibadilishwe lakini kaleta hoja! Nimegundua matatizo yetu yanaanzia huku tukija kupewa uongozi ndio tunafanya kila kitu kwa mwendokasi
 
Mleta maada jifunze kujenga hoja, msingi wa hoja (premise) yako hauna mantiki, hujui ni kwanini zibadilishwe halafu unasema wakati umefika...!! Nini sasa
 
Noti ya Sh 500/- ni aibu. Inachakaa haraka mno pia haina hadhi. Ni kidunchu mno. Nimewahi kudokezwa kuwa tenda yake BoT ilimpa yule kada wa CCM aliyeachana na "siasa uchwara" a.k.a Dowans/ Al Adawi.
 
Mkuu zibadilishwe kwa sababu ipi..? Je hazina ubora au sababu ni nini..? Unaweza kuwa na hoja nzuri tena yenye kujenga, hebu funguka Mkuu.
Serikali ni vyema ikabadilisha Noti zote ili
1.kubaini Noti bandia.
2.kuhakiki mzunguko wa fedha.
3.kubaini ni kina nani wamehodhi Noti nyingi ambazo hazimo katika mzunguko.
4.Kutengeneza noti zenye ubora zaidi kuliko sasa.
Kama siko sawa mnaweza nisahihisha au kuongeza vilivyokosekana.
 
1.KUEPUKA NOTI BANDIA PENDA KUFANYA MALIPO KUPITIA BENKI.
2.TUANZE MAZOWEA YA KUTUMIA MIFUMO YA KIBENKI MZUNGUKO UTAHAKIKIWA.
3.KUBAINI WALIOHODHI PESA UKIPATA PESA PAKA SUPA GLUU MIFUKONI WANAOKUNYANG'ANYA WAHODHI WAO WATASHINDWA NA KULEGEA.
4.KUPATA ZENYE UBORA TUTENGENEZE ZA PLASTIKI KAMA YEBOYEBO.
SULUHISHO NI WATZ TUENDANE NA MIFUMO YA UCHUMI WA KISASA DUNIANI
 
  • Thanks
Reactions: MC7
Noti ya Sh 500/- ni aibu. Inachakaa haraka mno pia haina hadhi. Ni kidunchu mno. Nimewahi kudokezwa kuwa tenda yake BoT ilimpa yule kada wa CCM aliyeachana na "siasa uchwara" a.k.a Dowans/ Al Adawi.

Huyo mhindi kila tenda ya maana ya SERIKALI yupo
 
Serikali ni vyema ikabadilisha Noti zote ili
1.kubaini Noti bandia.
2.kuhakiki mzunguko wa fedha.
3.kubaini ni kina nani wamehodhi Noti nyingi ambazo hazimo katika mzunguko.
4.Kutengeneza noti zenye ubora zaidi kuliko sasa.
Kama siko sawa mnaweza nisahihisha au kuongeza vilivyokosekana.
Haya yaongezee pale juu......
 
Serikali ilitolea ufafanuzi hili vizuri sana.

Noti ya 500 ilitakiwa itumike miezi saba tu kisha irudi benki kuu. Ila ndiyo imegoma kwenye mzunguko kama "chenji". Kwa kutumiwa sana (mzunguko kuwa mkubwa) zinachakaa haraka.

Hivyo serikali inakusudia kuanzisha sarafu ya 500.

Sababu ya kubadilisha walisema "sarafu inawezakutumiwa kwa muda mrefu zaidi ya noti".
sarafu ya mia tano ipo kama haipo! nchi ya kujaribu kila kukicha hii.
 
Serikali ilitolea ufafanuzi hili vizuri sana.

Noti ya 500 ilitakiwa itumike miezi saba tu kisha irudi benki kuu. Ila ndiyo imegoma kwenye mzunguko kama "chenji". Kwa kutumiwa sana (mzunguko kuwa mkubwa) zinachakaa haraka.

Hivyo serikali inakusudia kuanzisha sarafu ya 500.

Sababu ya kubadilisha walisema "sarafu inawezakutumiwa kwa muda mrefu zaidi ya noti".
mbona hipo iyo sarafu ya500 ilakuigusa sio mchezo
 
Back
Top Bottom