Wakati umefika CHADEMA ichukue ruzuku yake kuendesha shughuli za chama

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
39,761
71,144
Nimesikiliza vizuri hotuba ya Rais kuhusu siasa kwa mwaka 2023 na nimeona ni wakati muafaka sasa kwa CHADEMA kuchukua ruzuku yake kutoka serikalini hata kama kiwango sio sahihi kutokana na uchaguzi kuwa haukuwa huru na haki.

Wanachama na wafuasi wa CHADEMA ni walipa kodi na pesa zao sasa zinatumika kwa wengine basi na wao chama chao kichukue kilichopo ili kugharamia hii mikutano inayoanza kurindima nchi nzima na inahitaji fedha pia.

Hotuba ya Rais inaonyesha wazi kuwa mabadiliko yanayotokea ni juhudi za msukumo wa CHADEMA ndio zimezaa haya. Chukueni pesa hizo zisaidie chama kwa sasa.

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
 
Wakati walikua wanachukua toka muda mrefu, na akina halima wataendelea na ubunge wao kama kawaida,
 
Wakati walikua wanachukua toka muda mrefu, na akina halima wataendelea na ubunge wao kama kawaida,
Unao ushahidi kuwa wanachukua? Issue ya kina Halima sio ya kisiasa bali ni JINAI. Na Rais Samia anapaswa kuliangalia jambo hili kwa tahadhari tofauti na wengine wanavyoliona maana kufoji nyaraka za serikali na kuzitumia kupata watu wakuingia Bungeni ni NAJISI

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
 
Nimesikiliza vizuri hotuba ya Rais kuhusu siasa kwa mwaka 2023 na nimeona ni wakati muafaka sasa kwa Chadema kuchukua ruzuku yake kutoka serikalini hata kama kiwango sio sahihi kutokana na uchaguzi kuwa haukuwa huru na haki.
Wanachama na wafuasi wa Chadema ni walipa kodi na pesa zao sasa zinatumika kwa wengine basi na wao chama chao kichukue kilichopo ili kugharamia hii mikutano inayoanza kurindima nchi nzima na inahitaji fedha pia.
Hotuba ya Rais inaonyesha wazi kuwa mabadiliko yanayotokea ni juhudi za msukumo wa Chadema ndio zimezaa haya.
Chukueni pesa hizo zisaidie chama kwa sasa.

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app

CHADEMA wapewe credit kwa haya tuliyopata. Msimamo wao ndio umemlazimisha mama kuchukua hatua.
 
Kuchukua ruzuku ni kuhalalisha yaliyofanyika kwenye uchaguzi wa 2020 , naamini katika maridhiano ila hili la ruzuku hapana
 
Viongozi wakuu wa Chadema Kuna mahali wanavuta Hela ndefu, hawawezi kuwakumbuka wa chini yao
 
Kuchukua ruzuku ni kuhalalisha yaliyofanyika kwenye uchaguzi wa 2020 , naamini katika maridhiano ila hili la ruzuku hapana
Mkuu, sasa hivi kukaa na Rais na serikali yake ya CCM huku tukitambua wao ndio watawala ni kama sehemu ya kukubali matokeo ya 2020 ambayo hakuna ubishi ni wizi mtupu.
Lakini juhudi zilizofanywa na chama hadi sasa ni salamu tosha kuwa hata wao wamekubali kuwa uchaguzi haukwenda sawa huku wakimtupia lawama marehemu kuwa ndio aliharibu.
Sasa tufanyeje? Ruzuku ni kodi za wananchi hata kama hesabu zinapigwa kwa formula haramu lakini Chadema kinastahili kuhudumiwa na kodi zetu maana hizo hela sio za CCM.
Kukubali mazungumzo ambayo yamezaa faida ni salamu tosha kuwa sasa lazima chama kihudumiwe na wananchi kwa kuwapa ruzuku yao hata kama ni pungufu

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom