Medecin
JF-Expert Member
- Nov 29, 2011
- 7,896
- 21,303
Picha hizi nimezipiga mahali fulani sitapataja jina maana ntahatarisha vibarua vya watu lakini uhalisia ni kuwa wananchi wameanza kung'oa mataluma ya reli na kwenda kuyatumia kwa shughuli zao nisizozijua. Hii ni baada ya serikali kuitelekeza reli hii kwa muda mrefu bila matumizi yeyote.
Tafakuri ninayowaachia leo je ni sahihi kutumia matrilioni ya walipa Kodi kujenga reli mpya wakati iliyopo tumeshindwa kuilinda na kuitumia? Je tukimaliza kujenga SGR, utawala utakaokuja miaka ijayo utaweza kulinda miundombinu yake? Au yatajirudia hayahaya!
Picha kwa hisani yangu