Wakati tunafurahia kichekesho cha TRAB na TRAT tukumbuke trilioni 360 ni pesa nyingi sana

RNA

JF-Expert Member
Mar 27, 2013
1,584
2,683
Habari JF,

Nimeona niwakumbushe Watanzania wenzangu maana asilimia kubwa tumezoea kushabikia vitu visivyo vya msingi. Triloni 360 ni pesa nyingi sana zinaweza kututoa tulipo kuwa donor country.

Hivyo tusiishie kushare video na kucheka bali ni vizuri tufuatilie kwa umakini tuone muenendo wake zisije ishia kwa wenye mifuko mipana.
 
Kwa wabongo ndio imeisha iyo na soon inaweza kutungiwa wimbo
IMG-20220924-WA0036.jpg
 
Madai ya TZS 360Tn katika lile suala la makinikia yalikuwa yanakosa uhalisia. Ni kama vile Tundu Lissu alivyoiita ripoti iliyotoa ushauri uliopelekea madai hayo kuwa ni "professorial rubbish"

Prof. Osoro na timu yake pengine kutokana na hadidu rejea za ajabu alizopewa na JPM ndipo akalazimika kuja na "recommendation & conclusive remarks" za madai ya fedha hizo. Kitu cha ajabu ni pale serikali ilivyoipokea kwa mbwembwe ripoti ile, huku ikishindwa kutambua ukweli kuwa thamani ya madini yalipo ndani ya makinikia baada ya mchakato wa kuchenjuliwa haiwezi kuwa kubwa kiasi hicho.

JPM alitumia hisia zaidi ya kutazama suala husika kiuhalisia. Ndiyo! Alikuwa na tamaa kubwa sana ya maendeleo, lakini alijikuta akiishi ndani ya matamanio ya kufikirika kutokana na ndoto zake za alinacha.
 
Habari JF,

Nimeona niwakumbushe Watanzania wenzangu maana asilimia kubwa tumezoea kushabikia vitu visivyo vya msingi. Triloni 360 ni pesa nyingi sana zinaweza kututoa tulipo kuwa donor country.

Hivyo tusiishie kushare video na kucheka bali ni vizuri tufuatilie kwa umakini tuone muenendo wake zisije ishia kwa wenye mifuko mipana.
Siyo country ni kantri.
 
Gazeti la economist la marekani walitukejeli Sana wakidai kuwa kiwango hicho cha pesa cha trillion 360 ni zaidi ya budget ya NASA....ndoto za mchana za magufuli zilitupeleka puta
 
Hawakuomba ridhaa ya Bunge kuachana na hizo hela....

Kashfa mbaya kuliko zote nchini ukizikusanya kwa pamoja
 
Madai ya TZS 360Tn katika lile suala la makinikia yalikuwa yanakosa uhalisia. Ni kama vile Tundu Lissu alivyoiita ripoti iliyotoa ushauri uliopelekea madai hayo kuwa ni "professorial rubbish"

Prof. Osoro na timu yake pengine kutokana na hadidu rejea za ajabu alizopewa na JPM ndipo akalazimika kuja na "recommendation & conclusive remarks" za madai ya fedha hizo. Kitu cha ajabu ni pale serikali ilivyoipokea kwa mbwembwe ripoti ile, huku ikishindwa kutambua ukweli kuwa thamani ya madini yalipo ndani ya makinikia baada ya mchakato wa kuchenjuliwa haiwezi kuwa kubwa kiasi hicho.

JPM alitumia hisia zaidi ya kutazama suala husika kiuhalisia. Ndiyo! Alikuwa na tamaa kubwa sana ya maendeleo, lakini alijikuta akiishi ndani ya matamanio ya kufikirika kutokana na ndoto zake za alinacha.
Si bora huyo hata kama alikua na ndoto za alinacha, alidhubutu kuwa na ndoto za namna hiyo kiliko hawa tulio nao hawana ndoto za namna yoyote.
 
Gazeti la economist la marekani walitukejeli Sana wakidai kuwa kiwango hicho cha pesa cha trillion 360 ni zaidi ya budget ya NASA....ndoto za mchana za magufuli zilitupeleka puta
Tanzania ilipata bil 700 ambayo haikuwa nazo juzi, imepata hisa barrick ambazo hazikuwepo kabla, hata JPM alikuwa anajua hamna mtu atakayetoa tril 360 lkn alkuwa akiwavuta wake wakutane sehemu fulani
 
Yule mwizi mkuu aliyepiga 1.5 trillion!
Tutaachaje kuamini alivuta 10% katika hii makenikia?
Ndio maana East & southern Africa hatotokea corrupt leader Kama mwendazake
 
Tanzania ilipata bil 700 ambayo haikuwa nazo juzi, imepata hisa barrick ambazo hazikuwepo kabla, hata JPM alikuwa anajua hamna mtu atakayetoa tril 360 lkn alkuwa akiwavuta wake wakutane sehemu fulani
Hivi unajua ukubwa wa hizi tuhuma?
Unajua huko Tax revenue appeal board (TRAB) na Tax revenue appeal tribunal (TRAT) kuna wataalum wangapi ambao walitumika kushusha 360 tril to 700 bil?
Haiwezekan 10% ilihusika kwani rais alisema ana uhakika na vyombo vya vyake
 
Si bora huyo hata kama alikua na ndoto za alinacha, alidhubutu kuwa na ndoto za namna hiyo kiliko hawa tulio nao hawana ndoto za namna yoyote.
Na ungejua kama taifa, ni kitu hatari sana kuwa na ndoto za alinacha usingeandika hivyo.
Hizo ndoto za alinacha ndio sababu ya Lissu kuonekana adui wa muota ndoto hadi kujaribu kumuua lakini Mungu akamkatalia alinacha.
Taifa haliendeshwi kwa ndoto bali maono.

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
 
Kweli unamdai mtu milioni 1,000,000 anakulipa 1,900 yaani 0.19% unakubali...magufoool lilikuwa kichaa lenye boardguards
 
Tr 360 ndio ikasemekana kila mtanzania angepata Noah kama ingelipwa. Yaani bajeti ya Tanzania ya karibu miaka 15. Rubbish kabisa yule marehemu aliwaona watanzania ni malofa
 
Madai ya TZS 360Tn katika lile suala la makinikia yalikuwa yanakosa uhalisia. Ni kama vile Tundu Lissu alivyoiita ripoti iliyotoa ushauri uliopelekea madai hayo kuwa ni "professorial rubbish"

Prof. Osoro na timu yake pengine kutokana na hadidu rejea za ajabu alizopewa na JPM ndipo akalazimika kuja na "recommendation & conclusive remarks" za madai ya fedha hizo. Kitu cha ajabu ni pale serikali ilivyoipokea kwa mbwembwe ripoti ile, huku ikishindwa kutambua ukweli kuwa thamani ya madini yalipo ndani ya makinikia baada ya mchakato wa kuchenjuliwa haiwezi kuwa kubwa kiasi hicho.

JPM alitumia hisia zaidi ya kutazama suala husika kiuhalisia. Ndiyo! Alikuwa na tamaa kubwa sana ya maendeleo, lakini alijikuta akiishi ndani ya matamanio ya kufikirika kutokana na ndoto zake za alinacha.
Mwenye mashaka na uwongo wa marehemu, mtafute Mruma privately akueleze kilichotokea.

Kwa ujumla, uchunguzi wao haukugundua wizi wowote, lakini walilazimishwa. Baada ya wakilisho lao la mwanzo, wakatumwa kwake wasiojulikana, akaambiwa, "mkuu wa nchi amekwishawaambia wananchi kwamba tunaibiwa, hamwezi kwenda kutoa report kuwa hatuibiwi. Kaandikeni upya report itakayoendana na maneno aliyoyasema mkuu wa nchi". Timu nzima walikuwa kwenye wakati mgumu, wakalazimika kusema uwongo.
 
Kwenye sakata TRAT/TRAB tatizo lilikuwa kwa Mpina na Speaker ndio viongozi walioonyesha ulimbukeni kutokuwa up to date na development za sakata la trillion 360, wakati ata wananchi wakawaida wengi tu wanaelewa lilivyoishia.

Ndio maana Mwigulu alipokuwa ana elezea mara ya kwanza speaker akawa anampachika maswali mengine yasiyokuwa na kichwa wala miguu.

Unaweza msamehe Mpina kwa siasa za utoto lakini speaker anatakiwa kuwa na background ya mambo ya zamani ambayo yalikuwa na miadala mpana kwenye jamii na jinsi yalivyomalizwa.

If anything speaker ame onyesha kukosa umakini kwa kutokuelewa swali, majibu ya waziri, ku entertain upuuzi na kupelekea kuzua mjadala usio na lazima kwenye jamii all due to her ignorance on the matter.

Kwa upande wa serikali ya Tanzania sijui ata kama wanaelewa namna ya kupambana na ‘information war’ au hata umuhimu wa serikali ku control narrative katika maamuzi yake.

Ukiona mpaka muda huu kuna wananchi wengi awajaelewa sakata la makanikia lilivyoishia, wengi elimu yao kuhusu huo mzozo ni thread ambazo full misinformation from JF na vyanzo vingine vya mitandao au experts uchwara. Ni kwamba serikali aina control ya narrative kwenye sakata husika na pengine hakuna jitihada za makusudi zinazofanyika kuelimisha jamii; nchi makini mkurugenzi wa mawasiliano serikalini keshatimuliwa awezi propaganda.
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom