Wakati tunafurahia kichekesho cha TRAB na TRAT tukumbuke trilioni 360 ni pesa nyingi sana

Habari JF,

Nimeona niwakumbushe Watanzania wenzangu maana asilimia kubwa tumezoea kushabikia vitu visivyo vya msingi. Triloni 360 ni pesa nyingi sana zinaweza kututoa tulipo kuwa donor country.

Hivyo tusiishie kushare video na kucheka bali ni vizuri tufuatilie kwa umakini tuone muenendo wake zisije ishia kwa wenye mifuko mipana.
Maprof. walimwongopea Magufuli, hakuna pesa za hivyo. Lisu aliposema zile report ni za kupika na hazina ukweli wowote, nusura wamtoe roho.
 
Madai ya TZS 360Tn katika lile suala la makinikia yalikuwa yanakosa uhalisia. Ni kama vile Tundu Lissu alivyoiita ripoti iliyotoa ushauri uliopelekea madai hayo kuwa ni "professorial rubbish"

Prof. Osoro na timu yake pengine kutokana na hadidu rejea za ajabu alizopewa na JPM ndipo akalazimika kuja na "recommendation & conclusive remarks" za madai ya fedha hizo. Kitu cha ajabu ni pale serikali ilivyoipokea kwa mbwembwe ripoti ile, huku ikishindwa kutambua ukweli kuwa thamani ya madini yalipo ndani ya makinikia baada ya mchakato wa kuchenjuliwa haiwezi kuwa kubwa kiasi hicho.

JPM alitumia hisia zaidi ya kutazama suala husika kiuhalisia. Ndiyo! Alikuwa na tamaa kubwa sana ya maendeleo, lakini alijikuta akiishi ndani ya matamanio ya kufikirika kutokana na ndoto zake za alinacha.
Serikali inapaswa kumwita Prof Osoro na waongozane kwenda Ofisi za Barrick ili Osoro akafafanue vizuri yale mambo aliyoyaandika kwenye report yake.
 
Mwenye mashaka na uwongo wa marehemu, mtafute Mruma privately akueleze kilichotokea.

Kwa ujumla, uchunguzi wao haukugundua wizi wowote, lakini walilazimishwa. Baada ya wakilisho lao la mwanzo, wakatumwa kwake wasiojulikana, akaambiwa, "mkuu wa nchi amekwishawaambia wananchi kwamba tunaibiwa, hamwezi kwenda kutoa report kuwa hatuibiwi. Kaandikeni upya report itakayoendana na maneno aliyoyasema mkuu wa nchi". Timu nzima walikuwa kwenye wakati mgumu, wakalazimika kusema uwongo.
Magufuli alikua fiksi yule mzee..japo kuna maeneo alifanya poa nampa 1/10

Sent using Jamii Forums mobile app
 
JPM alitumia hisia zaidi ya kutazama suala husika kiuhalisia. Ndiyo! Alikuwa na tamaa kubwa sana ya maendeleo, lakini alijikuta akiishi ndani ya matamanio ya kufikirika kutokana na ndoto zake za alinacha.
Kwahio reality ni sasa mgao wa umeme kurudi kutafuta crane ya Bwawa kama needle in the haystack na mkuu wa nchi kuzurura hovyo hadi kupelekea kukaa ugenini zaidi ya wiki kwa kufanya kazi za akina Diamond, bila kusahau kuwazima wanaoongea kwa kuwatafutie vikazi vya ajabu ajabu...?

Kama huo ndio U-Alinacha Had rather live kwenye ndoto yenye ahueni kitaa kuliko uhalisia wenye faida ya wachache wakati majority ndio tuna-facilitate their extravagant lifestyles
 
Hizi Tirilion 360 ndiyo tumezikosa kwa sababu serikali legevu.Kwa sasa hakuna mwenye uwezo wa kuzidai
 
Habari JF,

Nimeona niwakumbushe Watanzania wenzangu maana asilimia kubwa tumezoea kushabikia vitu visivyo vya msingi. Triloni 360 ni pesa nyingi sana zinaweza kututoa tulipo kuwa donor country.

Hivyo tusiishie kushare video na kucheka bali ni vizuri tufuatilie kwa umakini tuone muenendo wake zisije ishia kwa wenye mifuko mipana.
Hizo trilioni we umeziona wapi achana na mambo ya kusadikika. Huo ni utopolo wa genge la wasukuma likiongozwa na kina Luhaga Mpina. Alikuwa wapi mpk asubiri kutemwa uwaziri? Msikubali kutimika kwa maslahi ya wajanja wachache pambana na mambo yako
 
Tunao vijana wajinga sana nchi hii. Wale wenye influence na kuweza kupata wa kuwasikiliza wamejawa na mambo ya kipuuzi.
*****

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
Kwann unashutumu vijana tu wakati nafasi nyeti zote zimeshikiliwa na wazee? Kuanzia jpm, kabudi, maprofesa waliotoa ile ripoti, mpaka walio-negotiate kutoka trilioni 300+ mpaka bilioni 700 kuna kijana hata mmoja?. Vijana maisha yanatupiga sana huku mtaani tupumzisheni kidogo na masimango basi
 
Habari JF,

Nimeona niwakumbushe Watanzania wenzangu maana asilimia kubwa tumezoea kushabikia vitu visivyo vya msingi. Triloni 360 ni pesa nyingi sana zinaweza kututoa tulipo kuwa donor country.

Hivyo tusiishie kushare video na kucheka bali ni vizuri tufuatilie kwa umakini tuone muenendo wake zisije ishia kwa wenye mifuko mipana.
Hayo madai yalikua halali au zilikua siasa? Tuanzie hapo kwanza
 
Kwann unashutumu vijana tu wakati nafasi nyeti zote zimeshikiliwa na wazee? Kuanzia jpm, kabudi, maprofesa waliotoa ile ripoti, mpaka walio-negotiate kutoka trilioni 300+ mpaka bilioni 700 kuna kijana hata mmoja?. Vijana maisha yanatupiga sana huku mtaani tupumzisheni kidogo na masimango basi
Badala ya kupambania maovu yanayofanywa na kuangamiza vijana wenzso, wao wanajikita kwenye mizaha
 
Aisee kweli sisi ni wajukuu wa Chief Mangungo.

Tunauza haki yetu hivi hivi na kuwakejeli wanaoipigania.
 
Hizo trilioni we umeziona wapi achana na mambo ya kusadikika. Huo ni utopolo wa genge la wasukuma likiongozwa na kina Luhaga Mpina. Alikuwa wapi mpk asubiri kutemwa uwaziri? Msikubali kutimika kwa maslahi ya wajanja wachache pambana na mambo yako
mkuu na 700billioni vp ?
 
Back
Top Bottom