Wakati Tanzania tunatambaa kama viwete, Kigali wakata mbuga - heko Kagame ! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wakati Tanzania tunatambaa kama viwete, Kigali wakata mbuga - heko Kagame !

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mag3, May 13, 2010.

 1. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #1
  May 13, 2010
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Tumelogwa nini Watanzania ? Kwa miaka kumi na miwili Kigali wameweza, sisi kwa miaka karibu hamsini tumekwama pale pale utadhani viwete. Cha ajabu tunaendelea kuuchagua uongozi ule ule na watu wale wale,what's wrong with us jamani ? Heko Kagame !
   
 2. T

  Tata JF-Expert Member

  #2
  May 13, 2010
  Joined: Dec 3, 2009
  Messages: 4,737
  Likes Received: 657
  Trophy Points: 280
  Ni amani, utulivu na mshikamano wetu mheshimiwa.

  Hawa jamaa walifanikiwa kuondoa uongozi na uoza wote uliokuwepo na kuanza upya wakiwa na viongozi wapya wenye mawazo mapya na mwelekeo mpya. Hiki ndiyo kitu ambacho hapa kwetu hatuna.
   
 3. l

  lebabu11 JF-Expert Member

  #3
  May 13, 2010
  Joined: Mar 27, 2010
  Messages: 1,651
  Likes Received: 518
  Trophy Points: 280
  Amani na mshikamano haijatuloga, bali tumeshindwa kuitumia kuwaondoa wachache wanaotupeleka pabaya.
  Ili tuendelee tunahitaji kwanza kabisa kukubali mabadiliko, na hilo ndilo hao wachache hawalitaki na wameteka kwa muda mrefu mawazo ya wananchi maskini.
  MAENDELEO NI MABADILIKO KUTOKA HALI DUNI KWENDA HALI BORA ZAIDI. NA HILI LAWEZEKANA TU KWA KUBADILISHA MARA KWA MARA WATAWALA ILI KUZIPA NAFASI FIKRA MPYA!
   
 4. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #4
  May 13, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Hta rais wako JK anajiuliza swali hilo hilo.
   
 5. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #5
  May 13, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Kikwete aliulizwa swali kama hilo kwanini Tanzania ni masikini akasema hata yeye hajui, wanaojua ukweli wote walio hai kwa sasa ni Kingunge, Malecela na Msekwa, ndio sumu iliyotuloga Period, utakwenda kulia utakwenda kushoto lazima utarudi kwa hao watu watatu.
   
 6. Shalom

  Shalom JF-Expert Member

  #6
  May 13, 2010
  Joined: Jun 17, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Si CCJ inakuja na sera ya ujamaa? tutawapita tu muwe na subira!

  Tunaaacha kuungana na kuwatoa hawa mashetani madarakani halafu tutengeneze mfumo mzuri wa siasa ndiyo tuanza kupractice idiology, yanakuja majitu na utuititri wa vyama kila siku ukiwauliza eti sisi ni wajamaa, nani mjamaa katika nchi hii kwa sasa mpendazoe au tutaanza na ccj?
   
 7. M

  Mzawa Halisi JF-Expert Member

  #7
  May 13, 2010
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 500
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Hapana, nakataa, JK ana jibu la swali hilo. Anajua tatizo ni yeye na mfumo wake wa uongozi. Na hana analoweza kufanya kwani ni mfumo unaomlinda yeye, na hata kama hautaki hana la kufanya kwani hao waliomweka hapo wanafaidika na mfumo huu.
   
 8. babukijana

  babukijana JF-Expert Member

  #8
  May 13, 2010
  Joined: Jul 21, 2009
  Messages: 4,817
  Likes Received: 1,164
  Trophy Points: 280
  i dnt buy this propaganda,situation there is worser than what it say here,haya yote yanafanyika under dictatorial regime,where everyone has to follow the rules,otherwise prepare to be jailed at any time for simple reason.mbaya zaidi when minority rules majority anything can happen anytime,kumbuka theres milion rwandan just in uganda and other millions in congo and they never want to go back until then,sidhani kama kutakua na amani katika hali km hiyo.mi nimechoka hata kuripoti matukio ya huko hapa.
   
 9. JS

  JS JF-Expert Member

  #9
  May 13, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 2,065
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Pia utawala wa kibabe wa Kagame(udikteta) umeisaidia sana Rwanda kusonga mbele kimaendeleo. tunahitaji mbabe mmoja tu kwa miaka hiyo hiyo mitano wala si mingi akisema sheria hii ifuatwe itafuatwa na siyo kuwasihi watu waifuate kama unvyomwomba mtoto au mgonjwa ale chakula.
   
 10. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #10
  May 13, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,801
  Likes Received: 83,173
  Trophy Points: 280
  Kuhusu usafi sasa hivi Wanyarwanda wanasifia sana hilo la usafi wa hali ya juu katika miji ndani ya nchi yao. Sisi tumekaa kupiga domo tu jiji la Dar linanuka kwa uchafu ikinyesha mvua hata hutaki kutoka nje jinsi kulivyo jaa uchafu, lakini the so called Viongozi hawasemi lolote lile kuhusu uchafu uliokithiri katika jiji la Dar na majiji yetu mengi. Kwa maana nyingine hawaoni tatizo lolote la uchafu huo!!!
   
Loading...