Wakati Tanzania na Kenya tukiendelea kutekenyana Uganda wao mbioni ku launch kinu cha nyuklia na kuwa nchi ya pili Afrika

TheDreamer Thebeliever

JF-Expert Member
Feb 26, 2018
2,437
2,000
Habari wadau.!
Wakati Tz na Kenya wao mambo yao yanalega lega na kupinda pinda huku mama akipambana kuyanyoosha wao waganda wapo mbioni ku launch kinu cha nyuklia kwa "mpango wa amani" ambapo nuklia hiyo itazalisha takribani 41,700Megawatts mpaka kufikia 2040.

Uganda wameingia mkataba na wachina ambao watasanifu, watajenga na kuendesha mradi wa nyuklia,hii inafanya Uganda kuwa nchi ya pili kwa Afrika kwa uzalishaji wa umeme kupitia nyuklia ukiachia mbali SA ambayo ni ya kwanza.

Tukumbuke pia waganda hawa hawa wana mafuta ghafi ambayo yatasafirishwa kuja Tanzania,inaonyesha waganda wamejipanga sana kuliko hata nchi nzingine.

Tanzania sio kwamba hatuna haya madini ya nyuklia ,yapo mengi sana kule kwa kina Komba kule Namtumbo Ruvuma pia yapo maeneo kama Namtumbo (Mkuju), Bahi, Galapo, Minjingu, Mbulu, Simanjiro, Lake Natron, Manyoni, Songea, Tunduru, Madaba and Nachingwea.

Hizi ni fursa ambazo serikali na wizara inabidi iwalete wawekezaji waje kuwekeza kwenye hii "Mkuju River Project "waache kusuasua na sisi twende kwenye huo umeme wa nyuklia ,pia nyuklia ina matumizi mengi hata mahospitalini n.k japo tuna bwawa la Nyerere ila mahitaji ya umeme yanaweza yakawa makubwa sana siku za usoni.

Pia miradi kama hii itasaidia kuongeza ajira kwa vijana wetu ,swala kama hili linatakiwa wizara ya madini kufanya fasta kuakikisha maeneo yenye deposit yanapata wawekezaji haraka sana ili kazi iendelee.
 
wolfpack

JF-Expert Member
Aug 6, 2013
847
1,000
Habari wadau.!
Wakati Tz na Kenya wao mambo yao yanalega lega na kupinda pinda huku mama akipambana kuyanyoosha wao waganda wapo mbioni ku lunch kinu cha nyuklia kwa "mpango wa amani" ambapo nuklia hiyo itazalisha takribani 41,700Megawatts mpaka kufikia 2040.

Uganda wameingia mkataba na wachina ambao watasanifu, watajenga na kuendesha mradi wa nyuklia,hii inafanya Uganda kuwa nchi ya pili kwa Afrika kwa uzalishaji wa umeme kupitia nyuklia ukiachia mbali SA ambayo ni ya kwanza.

Tukumbuke pia waganda hawa hawa wana mafuta ghafi ambayo yatasafirishwa kuja Tanzania,inaonyesha waganda wamejipanga sana kuliko hata nchi nzingine.

Tanzania sio kwamba hatuna haya madini ya nyuklia ,yapo mengi sana kule kwa kina Komba kule Namtumbo Ruvuma pia yapo maeneo kama Namtumbo (Mkuju), Bahi, Galapo, Minjingu, Mbulu, Simanjiro, Lake Natron, Manyoni, Songea, Tunduru, Madaba and Nachingwea.

Hizi ni fursa ambazo serikali na wizara inabidi iwalete wawekezaji waje kuwekeza na sisi twende kwenye huo umeme wa nyuklia ,pia nyuklia ina matumizi mengi hata mahospitalini n.k japo tuna bwawa la Nyerere ila mahitaji ya umeme yanaweza yakawa makubwa sana siku za usoni.

Pia miradi kama hii itasaidia kuongeza ajira kwa vijana wetu ,swala kama hili linatakiwa wizara ya madini kufanya fasta kuakikisha maeneo yenye deposit yanapata wawekezaji haraka sana.
Tukiachana na hayo, nuclear energy ni alternative kwasababu maji hupungua na iko siku in future kina cha maji kitasumbua tu hapo but how iw our thinking, how is their thinking Magu had the will power and was practical wengine ni leimans I hope mama will prove it
 
UmkhontoweSizwe

JF-Expert Member
Dec 19, 2008
5,184
2,000
Kama watu wanapinga hata umeme wa maji ili tuendelee kupigwa kwenye umeme wa mafuta na gesi, unadhani wataelewa issue ya nyuklia kweli? This dude Mwendazake, pamoja na mapunfufu yake, alikuwa na uwezo mkuwa wa kudiriki mambo ambayo aliona na kuamini yatakuwa na manufaa kwa taifa.
Ni wakati wa mama sasa, tumuunge mkono ili awe na the same courage ya kufanya makubwa zaidi kupita hata hayo aliyofanya Mr Stone!
 
tathmini

JF-Expert Member
Feb 10, 2011
311
250

Naona unachanganya uelewa. Umeme wa kutumia mafuta ulikuwa kidogo na wa dharura. Hata wakati wa dharura hiyo hizo mashini za kukodi nyingi zilitumia gesi. Gesi ndiyo mbadala wa maji/hydro, maana maji huisha haraka nyakati hizi za matumizi makubwa mengine ya maji. Jawabu la umeme haliko kwenye nyuklia bali mchanganyiko wa vyanzo vyote
 
Vyura99tu

Senior Member
Jan 14, 2017
176
250
Bora basi ungliandika kiswahili badala ya kujidai kuweka neno usilolijua kuandikwa kwake.!!
 
Kalamu1

JF-Expert Member
Jul 7, 2018
10,956
2,000
waganda wapo mbioni ku lunch kinu cha nyuklia kwa "mpango wa amani" ambapo nuklia hiyo itazalisha takribani 41,700Megawatts mpaka kufikia 2040
Hawawezi kamwe ku'lunch', bali wata'launch'.

Hata hivyo hii habari bado ni maneno mengi tu, kama ni ya 2040. Hapo jirani Kenya wao walishapanga na kuunda shirika kabisa la kusimamia kazi ya namna hiyo, na wanakula hela bila ya jasho, takribani miaka zaidi ya kumi sasa, nao ni maneno mengi bila vitendo.
 
Mlaleo

JF-Expert Member
Oct 11, 2011
12,232
2,000
Hapo kwenye ajira umechemsha.. sema vibarua... na mama ntilie
 
TheDreamer Thebeliever

JF-Expert Member
Feb 26, 2018
2,437
2,000
Tukiachana na hayo, nuclear energy ni alternative kwasababu maji hupungua na iko siku in future kina cha maji kitasumbua tu hapo but how iw our thinking, how is their thinking Magu had the will power and was practical wengine ni leimans I hope mama will prove it
kweli boss sasa tunapaswa kuwaza kuhusu nyuklia ndipo dunia inapoelekea kwenye nishati ya nyuklia .
 
TheDreamer Thebeliever

JF-Expert Member
Feb 26, 2018
2,437
2,000
Hapo kwenye ajira umechemsha.. sema vibarua... na mama ntilie
Kwa nini vibarua boss ???wakati wahandisi tupo wengi tu hata hapa Jf , tunapiga soga tu hapa Jf jua likizama tunaenda kudowea msosi wa shikamoo.

Tunaweza fanya practical ya miaka kadhaa na wachina au Russia yaani tutakuwa tunaendesha nao mradi huku wakitufundisha mdogo mdogo then baadae baada ya kupata uzoefu wanatuachia tuendeshe wenyewe vinu vya nyuklia.
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
TheDreamer Thebeliever

JF-Expert Member
Feb 26, 2018
2,437
2,000
Hawawezi kamwe ku'lunch', bali wata'launch'.

Hata hivyo hii habari bado ni maneno mengi tu, kama ni ya 2040. Hapo jirani Kenya wao walishapanga na kuunda shirika kabisa la kusimamia kazi ya namna hiyo, na wanakula hela bila ya jasho, takribani miaka zaidi ya kumi sasa, nao ni maneno mengi bila vitendo.
Mkataba ushawekwa saini kazi imekwisha anza boss sio chai hizi ni kweli.

Sasa waza Mu7 akimiliki nyuklia japo wanasema ni mpango salamaπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Resurrection

JF-Expert Member
Jun 8, 2020
349
500
Mkataba ushawekwa saini kazi imekwisha anza boss sio chai hizi ni kweli.

Sasa waza Mu7 akimiliki nyuklia japo wanasema ni mpango salamaπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
The Dreamer Mm nimeona Watz wengi hawana vision ni watu wapo wapo kama mazombi fulani huwezi kuwa na maendeleo ya kweli kama huna infrastructure na vile vile huwezi kupata maendeleo au hata kupata wawekezaji wa kweli ikiwa huna ENERGY ya kutosha na ya uhakika so tunahitaji serikaki ipiganie mambo haya(UMEME .MAJI.NA BARABARA ZA KISASA) halafu uone kama hawakuja wawekezaji kwa maelfu .Duniani hakuko hivyo ushazimwa ushawaka maji hayatoki maji yamekatwa toka karne ya 21 lkn Tz mpk umeme ushazimwa badae ushawaka au maji yamekatwa au bara bara mbovu c,mon GOV.
 
Ndio Tz yetu ,watu hawajielewi na wanao jielewa wanajitoa ufahamu washibishe matumbo yaoπŸ˜‚πŸ˜‚
 
mkorinto

JF-Expert Member
Jun 11, 2014
23,967
2,000
Kama watu wanapinga hata umeme wa maji ili tuendelee kupigwa kwenye umeme wa mafuta na gesi, unadhani wataelewa issue ya nyuklia kweli? This dude Mwendazake, pamoja na mapunfufu yake, alikuwa na uwezo mkuwa wa kudiriki mambo ambayo aliona na kuamini yatakuwa na manufaa kwa taifa.
Ni wakati wa mama sasa, tumuunge mkono ili awe na the same courage ya kufanya makubwa zaidi kupita hata hayo aliyofanya Mr Stone!
mama yeye anadeal na mitandao hasa jf na twita,huku anakutana na vilaza kibao ndio anawasikiliza.

unadhani tutamsaidiaje???
 
DENLSON

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
638
1,000
Kama watu wanapinga hata umeme wa maji ili tuendelee kupigwa kwenye umeme wa mafuta na gesi, unadhani wataelewa issue ya nyuklia kweli? This dude Mwendazake, pamoja na mapunfufu yake, alikuwa na uwezo mkuwa wa kudiriki mambo ambayo aliona na kuamini yatakuwa na manufaa kwa taifa.
Ni wakati wa mama sasa, tumuunge mkono ili awe na the same courage ya kufanya makubwa zaidi kupita hata hayo aliyofanya Mr Stone!
Gesi ni yetu iweje tupigwe? Kama tunapigwa huyo unayemsifia anaepuka vipi lawama, hakuwa sehemu ya bunge? Hakuwa mjumbe wa baraza la mawaziri? aliwahi kupinga au kuongelea hilo jambo kuwa tunaibiwa?

Tatizo la nchi hii ni CCM na viongozi wake kupenda chama kuliko nchi.

Watu walipinga ujenzi wa gharama wa Bwawa ikiwa tayari kama nchi tumeshawekeza kwenye gesi tena kwa hela ya mkopo kisha ghafla mtu anakuja anataka umeme wa maji kwanini watu wasihisi kuwa kuna 10% ya watu hapo?

Inajulikana duniani kote umeme wa maji sio wa uhakika sasa tayari tulikuwa na gesi na mambomba yapo kwanini tusiendeleze kama kweli shida yetu ni umeme maana gharama ingepungua kwa kadili muda unavyokwenda na umeme kuzalishwa
 
Kalamu1

JF-Expert Member
Jul 7, 2018
10,956
2,000
Mkataba ushawekwa saini kazi imekwisha anza boss sio chai hizi ni kweli.

Sasa waza Mu7 akimiliki nyuklia japo wanasema ni mpango salamaπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Siyo rahisi hata kidogo kwa Uganda kuwa 'nuclear power' katika eneo hili.

Hiyo wanayojenga, kama ni kweli watajenga, ni matumizi ya umeme na mahitaji ya huduma za kiafya, hawawezi kwenda mbali zaidi ya hapo. Sioni Uganda wakiwa na 'audacity' kama ya Korea Kaskazini, au Pakistan, au Israel.
Si unaona jinsi Iran anavyohangaika sasa, pamoja na kulitaka bomu kwa udi na uvumba?
 
TheDreamer Thebeliever

JF-Expert Member
Feb 26, 2018
2,437
2,000
Siyo rahisi hata kidogo kwa Uganda kuwa 'nuclear power' katika eneo hili.

Hiyo wanayojenga, kama ni kweli watajenga, ni matumizi ya umeme na mahitaji ya huduma za kiafya, hawawezi kwenda mbali zaidi ya hapo. Sioni Uganda wakiwa na 'audacity' kama ya Korea Kaskazini, au Pakistan, au Israel.
Si unaona jinsi Iran anavyohangaika sasa, pamoja na kulitaka bomu kwa udi na uvumba?
nani anayefahamu kesho itakuwaje?Hata Iran walianza na mpango salama km Uganda.Sio rahisi kwa Uganda kutengeneza nuclear weapons ila watakuwa more respected kwenye EA than any other member.😁😁
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom