Wakati taifa likikabiliwa na njaa na mafuriko wasomi wetu wanagomea chakula! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wakati taifa likikabiliwa na njaa na mafuriko wasomi wetu wanagomea chakula!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Omuregi Wasu, Jan 10, 2010.

 1. Omuregi Wasu

  Omuregi Wasu JF-Expert Member

  #1
  Jan 10, 2010
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 753
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Wanafunzi Muhimbili wagomea chakula
  Na Hellen Mwango  10th January 2010


  [​IMG]
  B-pepe  [​IMG]
  Chapa  [​IMG]
  Maoni

  Wanafunzi wa Taasisi ya Vyuo Shirikishi Muhimbili (Muhas) wamefanya mgomo wa kula wakipinga hatua ya kubadilishiwa ratiba ya chakula ikiwemo kukosa kuku, mayai na matunda.
  Hatua hiyo ilifikiwa juzi baada ya wanafuzi hao kukuta ratiba mpya ya chakula ikiwa imebandikwa katika bwalo lao chakula.
  Mgomo huo ulianza juzi usiku baada ya wanafunzi hao kuingia bwaloni mwao na kukuta wamepikiwa ugali na maharage badala ya wali na nyama kama ratiba ya awali ilivyokuwa inatakiwa.
  Akiongea na Nipashe Jumapili Rais wa taasisi hiyo, Richard Molega, alisema wamechoshwa na matukio ya kubadilishiwa chakula tangu Oktoba 12, mwaka jana.
  Molega alisema walipofungua chuo mwaka jana ratiba ya chakula ilibadilika ambapo waliondoa kuku, maziwa, mayai, matunda na nyama kutoka mara tatu kwa wiki na kubaki mara mbili.
  Alisema walipohoji kubadilishwa kwa ratiba hiyo hawakupatiwa ufafanuzi wala maelezo yoyote hali iliyosababisha wajilazimishe kula chakula hicho pasipokujua hatima ya ratiba hiyo mpya.
  "Hata hivyo tulisikia Rais Jakaya Kikwete anakuja kufungua jengo hapa Muhimbili tukauambia uongozi wa hospitali kama hawatabadilisha ratiba ya chakula tutagoma kula na kumfikishia malalamiko yetu mheshimiwa rais," alisema.
  Aliongeza kuwa uongozi ulibadilisha ratiba halisi ya chakula ikiwa ni kuku, maziwa, mayai, matunda na nyama kama ilivyopangwa.
  "Tumeshangaa jana (juzi) jioni kukuta imebandikwa ratiba ambayo inaonyesha kupunguzwa baadhi ya vyakula kama kuku, maziwa, mayai, na nyama kwa hiyo tumegoma kula kama ilivyo kawaida mtu akiwa na njaa hawezi kufanyakazi wala kusoma hata darasani itakuwa sio rahisi kuingia kama hakutakuwa na ufumbuzi," alisema Molega.
  Aliongeza kuwa ratiba hiyo iliyoonyesha mabadiliko ya chakula haina mhuri wala sahihi ya mtu aliyeitoa hali inayiowapa mashaka kufanyiwa mambo kienyeji.
  Naye Kaimu Mkrugenzi wa Taasisi Lalison Ndolele aliwasihi wanafunzi hao kula chakula kilichopo ili ifikapo kesho suala lao lizungumzwe na kufanyiwa kazi.
  Ndolele alikiri kuwapo kwa mabadiliko ya ratiba ya chakula hali inayosababishwa na mabadiliko ya mfumo wa bei za vyakula kwa sasa.
  "Mimi nawasihi kuleni chakula kilichopo ili kesho (Jumatatu) tukae chini kuliongelea suala lenu na hali itakuwa nzuri tafadhali," alisema.
  Hata hivyo bila kutarajia wanafunzi hao walisikika wakipaza sauti na kusema "Hatuli chakula hadi kieleweke tutaendelea kugoma."
  "Mimi sina la kusema kama mnaendelea kugoma sawa lakini wale ambao wataona sio vyema kugoma nawasihi wale chakula kilichopo," alisema Mkurugenzi huyo.
  Wanafunzi waliofanya mgomo huo ni zaidi ya 600 na kwamba hadi Nipashe Jumapili inaondoka bwaloni hapo ilishuhudia masufuria ya vyakula yakiwa yamejaa vyakula .  CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
   
 2. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #2
  Jan 10, 2010
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  Mafuriko yanahusiana vipi na watu kulishwa ugali na maharage
  bila ridhaa yao??????????????
   
 3. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #3
  Jan 10, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,284
  Likes Received: 19,437
  Trophy Points: 280
  hivi kumbe vyuo vikuu vya bongo wanapikiwa/ wanapewa msosi?..raha ilioje. ningejua ningesoma bongo
   
 4. M

  Magezi JF-Expert Member

  #4
  Jan 10, 2010
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Umeambiwa ni vyuo vingapi wanapikiwa??? Kumbuka Muhimbili ni chuo cha udaktari so huwa kuna baadhi ya mambo bado yanaendeshwa na utawala kama kuwapatia chakula badala ya pesa.

  Halafu kupikiwa siyo raha ndo maana unaona wanagoma......wangepewa pesa za mkopo usinge sikia mtu anagoma.
   
 5. M

  Magezi JF-Expert Member

  #5
  Jan 10, 2010
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Mtoa hoja unamawazo ya karne ya 17.........kwa kuwa kuna mafuriko basi mambo mengine ysiendelee.......watu wasi dai haki zao???
   
Loading...