Wakati Siku Saba Za Masha Zinakwisha - Mengi Katunukiwa na Rais? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wakati Siku Saba Za Masha Zinakwisha - Mengi Katunukiwa na Rais?

Discussion in 'Celebrities Forum' started by Allien, Dec 11, 2008.

 1. Allien

  Allien JF-Expert Member

  #1
  Dec 11, 2008
  Joined: Jul 6, 2008
  Messages: 5,548
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  Rais JK siku ya Jumanne alimtunukia Bw. Reginald Mengi pamoja na watu wengine Nishani mbalimbali kama inavyojieleza katika picha.


  Source: Guardian of 11th December 2008
   

  Attached Files:

 2. Allien

  Allien JF-Expert Member

  #2
  Dec 11, 2008
  Joined: Jul 6, 2008
  Messages: 5,548
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  Je inawezekana JK akawa kocha mchezaji katika hili? Kama si hivyo then looks like vikao vya kumhujumu Mengi JK hakuwepo.
   
 3. Mwawado

  Mwawado JF-Expert Member

  #3
  Dec 11, 2008
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 998
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 35
  Mkuu Allien utakuwa unamuangalia JK kwa jicho moja....Inapaswa uwe makini sana na huyu Muungwana,Yeye anajua kila kitu kinachoendelea kwenye sakata hilo la Masha Vs Mengi.Kama kawaida yake kwenye mambo mengi anajifanya hausiki...Hakuna anayeweza kutoa kauli "siku saba" zimekwisha na Bwana Waziri yupo Switzerland (Geneva),Kuna habari kuwa anarudi Tanzania Kesho....Ngoja tusubiri!!!

  Muungwana kama ilivyo Mugabe Nchi imemshinda......
   
 4. Allien

  Allien JF-Expert Member

  #4
  Dec 11, 2008
  Joined: Jul 6, 2008
  Messages: 5,548
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  Kiongozi Mwawado;

  Najizuia sana kutaka kujua nini hasa kiliongelewa katika katika hivyo vikao vya siri vya kumhujumu Mengi (Any way kama kweli vilikuwepo):

  Je JK alikuwepo na je anajua kinachoendelea?

  Kama anajua, je hii Tuzo aliyopewa Mengi na JK (sijui ni ipi) labda kwa ajili ya mchango wake kwa taifa, je alimezea tu wakati wa kumpa lakini moyoni anajua lazima tumfilisi Mengi?

  Kama hajui, je inawezekana kijana wake Waziri Msomi amechezea rafu Mengi na yeye JK amekuja tu kusikia tu katika Media?

  NB: Check distance ya kupeana mikono kati ya Muungwana na Bwana IPP!!
   
 5. m

  mwanibhoyo Member

  #5
  Dec 11, 2008
  Joined: Dec 4, 2008
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Body language inatoa ujumbe mwingine. Inaonyesha taadhima aliyonayo bw.JK kwa mh. Mengi. Isitoshe Mengi amekuwa mchangiaji mkubwa katika kampeni mbalimbali za CCM, kwa hiyo naamini viongozi muhimu wa CCM ikiwamo NEC,CC na mabaraza mbalimbali hususan la wazee, wako upande wa Mengi. Kimsingi, Masha anapiga kelele tu, huku akijua fika kuwa hana ubavu wa kupambana na mzee wa Kishumundu, Mengi. Huyo Masha mwenyewe anadharaulika na kubezwa na idadi kubwa ya wenye chama.

  Lakini kwa upande mwingine, nashindwa kuelewa kiwango halisi cha influence aliyonayo huyu 'waziri kijana' kwa mh.Rais. Inawezekana nikawa nimeteleza lakini inasemekana watoto wawili wa marais wetu, mmoja wa kule visiwani na mwingine wa Muungano ni waajiriwa wa kampuni ya kisheria ambayo bw.Masha ana hisa kubwa. Conflict of interests? sijui!!

  Lakini kwa mfumo ulivyo nchini kwetu, sio rahisi ati rais hana taarifa kabisa na mikakati hiyo. Na kama atakuwa anafahamu mikakati hiyo na asichukue hatua zozote, basi itatuletea maswali kuhusu udhati wa vita yake dhidi ya mafisadi.
   
 6. B

  Boma Senior Member

  #6
  Dec 11, 2008
  Joined: Apr 5, 2008
  Messages: 190
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  habari hii si ya kweli. mimi nilihudhuria sherehe hiyo ikulu. waliotunukiwa nishani walikuwa askari wa JWTZ, POLISI & MAGEREZA. Raia pekee alikuwa mh. Benard Membe pekee kwa vile alikuwa kiongozi wa mawaziri wa nje wa AU ambao niyo walipendekeza kupeleka wanajeshi comoro na yeye akawa na jukumu la kusimamia mpango huo. otherwise, kina mama wawili walienda kuwapokelea waume zao (maaskari) nishani kwa vile waume ho ni marehemu kwa sasa .
  R. Mengi alikuwa mwalikwa tu kama wengine na si kupokea nishani. jamani tuweke heshima ya JF kwa kuandika ukweli hapa
   
 7. Allien

  Allien JF-Expert Member

  #7
  Dec 12, 2008
  Joined: Jul 6, 2008
  Messages: 5,548
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145

  Kiongozi Boma;

  Kwanza Usini-question juu ya heshima kwa JF juu ya kuandika ukweli. Sijaandika Uongo na ndio maana unaona title ina question mark.

  Pili nimekuonyesha source ya habari na kuna picha ambayo inajitosheleza kwa maelezo, hivyo badala ya kuniqu-estion juu ya ukweli, question juu ya source na mwandishi wake na elezea juu ya credibility ya huyo mwandishi badala ya kunituhumu kutokuandika ukweli. I hope moderators watali-observe hili.

  Binafsi jana niliona sehemu fulani katika kipindi cha TBC cha Jambo Africa lakini niliona sehemu tu sherehe hizo hasa pale askari walipokuwa wanatunukiwa.

  Hata hivyo bado kuna maswali ya kimsingi juu ya ufahamu na Uhusika wa wa Muungwana katika sakata la Waziri Kijana na Mzee IPP.
   
 8. Allien

  Allien JF-Expert Member

  #8
  Dec 12, 2008
  Joined: Jul 6, 2008
  Messages: 5,548
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  Kama Muungwana atakuwa anafahamu au alishiriki katika mpango huu, basi kazi ipo.

  Ama akiona mambo mazito anaweza kumwambia Waziri Kijana aachane na mpango huo, ama akaendelea kumshughulikia kinamna kitu ambacho kinanipa wasiwasi. Muungwana wakati mwingine yuko makini kusoma alama za nyakati.
   
 9. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #9
  Dec 12, 2008
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Unfortunately, muungwana is sleeping on the job na wapambe wake wakina Jairo are taking advantage of the situation kufanya madudu yao; kwahiyo sintaona ajabu kama muungwana hafahamu kitu gani kinaendelea!!
   
 10. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #10
  Dec 12, 2008
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Mengi asubiri misuli ya Masha
  Na Ramadhan Semtawa


  MFANYABIASHARA maarufu nchini, Reginald Mengi hajawasilisha uthibitisho wa madai yake aliyotoa hadharani kuwa waziri mmoja kijana anataka kumuhujumu biashara zake, na sasa zamu ya Waziri wa Mambo ya Ndani, Lawrence Masha kuchukua hatuia baada ya siku saba kuisha.


  Masha, ambaye ni mwanasheria, alimpa Mengi siku saba kuwasilisha uthibitisho wa madai aliyoyatoa kwa waandishi wa habari kuwa kuna waziri kijana aliyewasilisha hoja katika kikao nyeti ya kutaka mfanyabiashara huyo abambikiwe kodi kwenye biashara zake ili ashindwe kuzilipa na hivyo kufilisiwa.


  Siku hizo saba ziliisha jana huku mamlaka za usalama wa raia zikiwa hazijapokea uthibitisho wowote kutoka kwa mfanyabiashara huyo, wala maelekezo kutoka kwa Waziri Masha, ambaye ameripotiwa kuwa safarini nje ya nchi na ambaye alionya kuwa iwapo mmiliki huyo wa makampuni ya IPP atashindwa kuwasilisha uthibitisho, atachukuliwa hatua za kisheria.


  Lakini inaonekana Mengi ametunisha msuli kusubiri kuona waziri huyo akichukua hatua hizo.


  Hadi jioni saa 11:30 jana, Mengi hakuwa amewasilisha uthibitisho huo, si wizarani wala makao makuu ya Jeshi la Polisi, huku waziri huyo akielezewa kuwa Geneva, Uswisi ambako yumo katika msafara wa Waziri Mkuu Mizengo Pinda kuhudhuria mkutano wa wa kimataifa wa wakimbizi.


  Mengi aliripotiwa kuwa mkoani Arusha kwa shughuli za kijamii.


  Akiongea na Mwananchi, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) Kamishna Robert Manumba aliweka bayana kwamba hadi jana hawakuwa wamepata maelekezo ya serikali kuhusu namna ya kushughulikia suala hilo.


  Naye msemaji mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Isaac Nantanga alithitibisha kwamba hadi jana jioni Mengi hakuwa amewasilisha taarifa yoyote wizarani.


  Alisema baada ya kuisha kwa siku saba alizopewa mfanyabiashara huyo, kinachosubiriwa ni kuona hatua ambazo zitachukuliwa kwa mujibu wa Waziri Masha.


  "Kwa kuwa alipewa barua ya wiki moja na wiki imekwisha, tusubiri tuone hatua itakayofuata, nafikiri tusubiri waziri atakachosema hapo baadaye," alifafanua.


  Msemaji huyo aliongeza kuwa hakukuwa na mawasiliano yoyote na Mengi na hakukuwa na haja ya kufanya hivyo kwani, tayari alipewa barua na waziri hivyo alichopaswa kufanya ni kujibu.


  "Yeye alipewa barua, kwa hiyo hakukuwa na haja ya kufanya naye mawasiliano alichopaswa kufanya ni kujibu tu barua ya waziri," alisisitiza msemaji huyo mkuu huyo wa wizara.


  Kutowasilishwa kwa ushahidi huo kunamaanisha kuwa Masha sasa anasubiriwa kuchukua hatua dhidi ya mfanyabiashara huyo, ambaye pia aliwahi kupambana na aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-Utawala Bora, Wilson Masilingi, katika serikali ya awamu ya tatu.


  Habari kutoka kwa watu walio karibu na mfanyabiashara huyo zinasema kuwa Mengi ameweka msimamo ambao haubadiliki kuhusu tuhuma hizo na kwamba badala ya kuwasilisha ushahidi, ni vema waziri huyo akaenda mahakamani.


  Awali Mengi alikaririwa na vyombo vya habari akisema kuwa kipindi hicho cha siku saba ni kirefu na kwamba ni vema hata angetoa siku moja.


  Msemaji wa Mengi, Abdulhamin Njovu hakutaka kuzungumzia suala hilo baada ya Mwananchi kuwasiliana naye kwa njia ya simu.


  Sakata hilo tayari limechukua sura na mwelekeo tofauti kutokana na maoni ya watu kugawanyika. Baadhi wanamtetea mfanyabiashara huyo na kuishushia lawama serikali, wakati wengine wanampinga mfanyabiashara huyo na kuitetea serikali.


  Wiki iliyopita, Baraza la Wazee Mkoa wa Dar es Salaam, bila ya kutaja majina lilitoa tamko kali ambalo liligusa pande zote mbili kwenye mgogoro huo, likiweka bayana kuwa kauli zinazotolewa si fikra za Watanzania, bali ni utashi binafsi wa kibiashara na kisiasa.


  Lakini viongozi wengi wa vyama vya siasa wamemtetea Mengi na kulaumu serikali kwa kufanya njama dhidi ya wafanyabiashara wazalendo.
   
 11. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #11
  Dec 12, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  nasdhani hakuja hana ya malumbano kwa hili. Ukweli ni kuwa mengi hakutunukiwa nishani yoyote, hivyo question mark kwenye mada inaweza kuondoka kwa kuwa jibu limepatikana. Na baada ya kujulikana kwa ukweli huo, je, mada hii bado inaswihi kwa jinis ambavy0 ilivyo?
   
 12. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #12
  Dec 12, 2008
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280

  Mada hii ifungwe kwani si kweli Mengi alipewa nishani. Kama ni kuchangia kuhusu Mengi Vs Masha basi ifnyike kwenye zile thread inayoendelea kuhusu hawa fahali wawili. Mods, please,, members hawatakiwi kupoteza muda kwa jambo ambalo sio kweli,, limeshathibitishwa so close it!!!! My observation tu!!!
   
 13. Gembe

  Gembe JF-Expert Member

  #13
  Dec 12, 2008
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 2,505
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135


  Mwawado..

  Kwa wanaojua jinsi Muungwana anavyotawala bwana unaweza kucheka.Leo anweza kumtuma Salva aseme hivi then anapima upepo watu wakija juu anabadilisha.

  1.Rejea suala la OIC,alimtuma Bernard baadaye akaja akaruka!

  2.suala la Balali hivyo,Mara ya kwanz aSalva alisema Hawamhitaji balali ila serikali inamkono mrefu ikimhitaji itampata..baadaye kafukuzwa kazi

  3.Wakati wa sakat la EPA ,Mkulu alienda kumuona mkapa na kumuliza afanyeje..Haya ya kina Mramba na JJJeetu Patel Mzee aliulizwa akabariki

  4.Hata suala la watu wengine wa EPA,Mkulu alibariki kwa kuwaambi kina hoseah na DPP watofautishe Siasa na Sheria.

  Hii inasaidia sana kumfana asionekane ana chuki na watu.Hata kipindi cha kina msabaha nasikia aliwapa pole baada ya kuwamwaga.


   
 14. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #14
  Dec 12, 2008
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Alien , there needs to be some substantive evidence kwamba Hon Mengi alitunukiwa nishani.Nami nieona ile picha kwenye gazeti Hon Mengi aki chat na JK lakini je akitunukiwa? BOMA anaapa kuwa hakutunukiwa kwa vile alikuwepo.Kutunukiwa si jambo baya , and of course from body language Hon JK kumualika Mengi ikulu by itself is an issue considering sakata la Mengi vs Waziri Kijana.
  How ever lets get the facts straight.
   
 15. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #15
  Dec 12, 2008
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Na hiyo kama ni strategicaly ...it might priempty kijana waziri if he isnt that carefull.
   
 16. N

  Nurujamii JF-Expert Member

  #16
  Dec 13, 2008
  Joined: Jun 14, 2007
  Messages: 414
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Jamani hapa kuna ujumbe mzito kutoka kwa JK kwenda kwa Masha! Tena kama Mengi angekuwa ni mmoja wa waliotunukiwa zawadi ningeweza kuamini kwamba ni kitu ambacho kilipangwa hata kabla ya huu ugomvi na kwa hiyo sakata la Masha lisingekuwa na uhusiano wala uzito wowote hapa. Lakini kwa kuwa amealikwa tena baada ya huu mzozo kutokea basi hapa kuna kitu jamani.

  Mesage sent
   
 17. M

  Mundu JF-Expert Member

  #17
  Dec 13, 2008
  Joined: Sep 26, 2008
  Messages: 2,719
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Nadhani Serikali ya Tanzania inamhitaji Mengi zaidi kuliko Masha. Masha ni mfanyakazi wa kawaida tu kama walivyo wafanyakazi wengine Serikalini. Yeyote anaweza kuwa Masha Serikalini, lakini si kila mtu anaweza kuwa Mengi Tanzania. JK alisema uwaziri hausomewi.
   
Loading...