Wakati sakata la Ndege halijakwisha, Symbion Power wameleta RB

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,597
215,272
1566771960529.jpeg


Ni kampuni ya kufua umeme
 
Kwa jinsi wanavyonyanyasa watumishi kwa kutolipa madai yao kwa wakati(wengine mpaka wanafariki hawajalipwa),wacha tu tunyooshwe ingawa ni kodi zetu.

Kwa kifupi,kuna kesi nyingi tu na inawezekana zikaibuka na zingine.

Cha ajabu,waliofanya maamuzi haya yanayotugharimu wanadunda, ila wapinzani ndio kila kukicha wanafunguliwa kesi kisa tu chuki za kisiasa!!

Tuacheni na usiri wa mikataba na maamuzi yanayokwenda kinyume na mikataba tunayosaini wenyewe tukiwa na akili zetu timamu, vinginevyo tusitafute huruma kutoka kwa yeyote yule.
 
Aisee hili jina la Mabeberu linaumiza, binafsi uniumiza. Hiyo kauli imeanza kufanya kazi sasa Beberu wamesimamisha vichwa.

Note: Namuunga mkono Mh. Rais John Magufuli.

Kukulacho kii nguoni mwako. Mababeru wakuu ni viongozi waliosaini mikataba mibovu. Na walijua ni mibovu ndiyo sababu waling’aka sana tuliposema tuione.

Baadhi ya fedha walizonazo viongozi wetu kwenye mabenki Uswizi na Cayman Islands wamezipata kama hongo ya kuridhia mikataba iliyouza taifa. Lakini wanajidai wazalendo sana.

Viongozi wetu wengi wanadharauliwa sana huko nje. Mtu anayefahamu kwamba ukipewa fedha utasaini mkataba wa kuumiza nchi yako ni lazima akudharau. Na hizi fedha pia wanapewa mawakili wanaotuwakilisha ili wanaotudai washinde.
That is why I keep saying : It’s broken, it can’t be fixed, it needs to be changed. Tumaini la kutumia watu walewale waliotukwamisha kutukwamua ni pitiable.
 
Back
Top Bottom