jkipaji
JF-Expert Member
- Sep 22, 2019
- 5,690
- 7,556
Wwe bado hujawa hata na familia,kuna misukosuko mingine huko nje lazima upambane nayo kimyakimya bila kuitaarifu familia yako, maana ukiitaarifu mapema unaweza sababisha maafaa zaidi kwa familia yako!!Utake usitake , Vita ya Urusi na Ukraine lazima itaathiri uchumi. Bei ya mafuta ya petroli katika soko la dunia inayumba sana hasa kutokana na vikwazo vya uchumi ambavyo bara Ulaya na Marekani wameiwekea Urusi. Nchi ndogo ndogo kama za kwetu - lazima zitatii vikwazo hivyo kwa kuwa makampuni mengi makubwa ya mafuta yanatii vikwazo hivyo kwa kuogopa kupigwa faini na Marekani. Kama ulifuatilia vizuri taarifa toka Zanzibar - ilifafanua kwamba kuna taarifa vitu vingi viliingia Zanzibar kabla ya vita ya urusi na Ukraine. Vita hii imedumu kwa mwezi mmoja sasa - Mfanyabiashara anayeweka shehena ( stock) ya zaidi ya mwezi mmoja yupo vizuri sana! Wa-Tz tunatakiwa kuanza kuzoea kuambiwa ukweli na viongozi wetu wakuu. Tusifurahia kudanganywa , vitisho na uonevu wa aina yoyote ile.