Wakati Rais Magufuli amegoma kusaini hukumu za waliohukumiwa kifo Rais Trump ameendelea kunyonga hadi wiki yake ya mwisho!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,821
141,727
Kiukweli binadamu tumetofautiana sana.

Rais Magufuli Magufuli alisema hajasaini hukumu yoyote ya kifo kwa wafungwa waliohukumiwa kunyongwa hadi kufa kwa sababu akifanya hivyo na yeye atakuwa anauwa. Rais Magufuli alisisitiza kuwa hana mpango wa kusaini hukumu yoyote ya kifo hadi anatoka madarakani.

Hali ni tofauti kabisa kule Marekani ambako Rais Trump ameshanyonga watu 13 na wa mwisho kanyongwa juzi ikiwa ni siku tatu tu kabla ya Trump kuachia madaraka kwa Rais mteule wa Marekani mh Biden.

Mungu mbariki Rais Magufuli.

Nawatakia Dominica yenye baraka.

Maendeleo hayana vyama!
 
Hivi kuidhinisha kunyonga ni mpaka tu utie saini kwa mbwembwe kwa hao wafungwa walio hukumiwa kunyongwa?

Vipi kuhusu yale matamko ya kuviruhusu vyombo vya dola kujichukulia sheria mkononi kutoka kwa swahiba wako john, tena dhidi ya watuhumiwa tu!!

Wanakuambia "Turirikamata rituhumiwa! wakati rinaenda kutuonesha ziripo siraha/watuhumiwa wenzake, ghafra risasi zimkamrukia na kumjeruhi! Na wakati tunariwahisha hospitari, rikafia njiani"!!!
 
Hawa wauwaji huku mitaani naona wawe wanahukumiwa huku mitaani, maana wanauwa asiye na hatia wao Wana hatia hawauwawi badala Yake tunaanza kuwalisha huko magerezani maisha yao yote.
 
Uongo, ujuha na upotoshaji mtupu , unafikiri kwa sababu kwako ni hadi Rais asaini ili mfungwa anyongwe mambo ndio yanafinyika hivyo duniani kote.Trump wala hasaini chochote ili mtu anyongwe.
 
Uongo, ujuha na upotoshaji mtupu , unafikiri kwa sababu kwako ni hadi Rais asaini ili mfungwa anyongwe mambo ndio yanafinyika hivyo duniani kote.Trump wala hasaini chochote ili mtu anyongwe.
Sasa unabishana na msemaji wa serikali ya Marekani?!

Bavicha bure kabisa!
 
Magufuli kwa kutia sahihi kwenye miswada ya sheria za bodi ys mikopo ya elimu ya juu na mifuko ya hifadhi za jamii atambuwe kuwa ameuwa watu wengi mno na ataendelea kuua hata akiwa nje ya madaraka kama sheria hizo hazitobadilika.
 
Acha upotoshaji! Adhabu za vifo Marekani haziidhinishi na Rais bali huidhinishwa na Magavana wa majimbo. Pia kumbuka Marekani siyo majimbo yote yana adhabu ya kifo!
We ndio hujui, kuna wafungwa wamehukumiwa na federal government na waliohukumiwa na state governments, hao wanaoidhinishwa kunyongwa na magavana walihukumiwa na state governments.
 
Back
Top Bottom