Wakati Raila Akigomea Kura Rais Uhuru Kenyatta Afanya Kampeni Kwa Bidii

Bowie

JF-Expert Member
Sep 17, 2016
4,372
6,078
Rais Uhuru Kenyatta wa chama cha Jubilee ameendesha kwa kasi kampeni zake za kusaka kura kwa ajili ya uchaguzi wa marudio utakaofanyika tarehe 26 October 2017.
Chama cha Jubilee kimejizatiti kutaka kuungwa mkono katika ngome za chama cha upinzani NASA huko Magharibi ya Kenya, kwasasa chama hicho kinauhakika kupata kura za uhakika kutoka bonde la ufa na mkoa wa kati ambayo ina wapiga kura wengi zaidi. Jubilee kwa kutumia wabunge, masenate na magavana walio wengi bungeni wamejipanga kuhakikisha wanapata ushindi wa kishindo.
Chama cha NASA chini ya Raila Odinga hakifanyi kampeni ipasavyo na imekuwa ni chama cha kulalamika na migomo, hali ya kifedha ya chama hicho nalo limekuwa tatizo katika kuendesha kampeni hizo. Jubilee wameweka mikakati mikubwa kuhakikisha wanapata ushindi wa kishindo.
 
Raila anafanya kampeini zake kwenye press conference, na mahakamani.
He hopes to use the courts to postpone the election.
 
Raila angepumzika tu ni dhaifu sana,amwache uhuru aendelee kupiga jaramba
 
Aisee sasa bila kampeni kweli Babaa ana nafasi tena ya kuingia Canaan...huyu anatafuta nusu mkate si kingine
 
Raila anafanya kampeini zake kwenye press conference, na mahakamani.
He hopes to use the courts to postpone the election.

Supreme Court ishatoa uamuzi(order) uchaguzi wa marudio ufanyike kabla ya siku 60 kwisha na 26/10/2017 ni ndani ya siku ambazo mahakama ya mwisho Kenya kutoa, hakuna mahakama ingine juu ya hiyo kwa hiyo Baba wa vitendawili yamemkuta, lazima aoge kwani maji kayatayarisha yeye mwenyewe kupitia koti. Tatizo lake kwa sababu ni fedha ya kufanyia kampeni hana ndiyo maana kabaki na press conferences na maandamano kugiribu akili za wachache ambao hawanazo! Supreme Court ilisema IEBC haikuwa na kosa na akawaamuru wasimamie uchaguzi wa marudio.
 
Kugoma ni dalili ya kuishiwa sera na kushindwa.
I know Odonga, he is just a political loser. Keshaona dalili za kushindwa anatafuta visingizio tu.
 
Ama kwa hakika mshika mpini ndio mwenye kisu.....
 
Back
Top Bottom