Wakati nikiwa siwataki tena Makocha Gomez na Hitimana, Wafuatao upesi sana Wafukuzwe na Wasimamishwe Simba SC

Nimekuelewa sana sana Mwamba....
Kama hizi Tuhuma Hujuma ni za Kweli!
Naomba MUNGU afanye Kazi yake,
Either kuoitia Mkono wa Serikali Au MUNGU mwenyewe....
Mkuu nina swali hapo,
Hivi Kwani hata kama CEO angekubali kuwaweka Kambi angewanyang’anya simu? Si bado wangewasiliana na wahunumu kwa Simu tuu hata Kama wapo Kambini?na Mzigo ukawekwa kwa Bank account?
SI kambi tu bali kambi yenye ulinzi mkali wa makomandoo wa timu,ambao wanakuwa wanafatilia nyendo zote za wachezaji kila muda,na kwa wachezaji wetu wa kiswahili na hawa ambao wamekaa sana Tanzania,bila usimamizi wa hali ya juu kwenye mechi za umuhimu usitegemee matokeo.

Unajua Tanzania wapo watu ni mafioso watu wa misheni town wazee wa kuuza ramani na ndio kazi zao,wapo kote kote Simba na Yanga timu ngeni ikija uwa wanaenda kufanya udalali wakidai wanajua ramani na mbinu za wenyeji hivyo uwa wanadai wapewe mzigo kiasi fulani,mzigo ukiwa mkubwa watavutwa wachezaji kadhaa, na kiongozi snitch mambo yanawekwa sawa watu wanatoboa mtumbwi wakiwa na uhakika wao wana maboya tiyali mfukoni,pesa uwa hawawekewi kwenye account watashtukiwa wanapewa chao cash mkononi!!
Kabla ya MO kuja Simba michezo hio imefanyika sana hasa kwenye mechi za kimataifa,kuna mtu mmoja mwenye asili ya kisomali aliwahi kuwa kiongozi wa Simba enzi zake ameuza sana mechi za kimataifa za Simba kwa timu za kigeni,anapewa mzigo anaita wawili watatu wachezaji wanapewa lesso kadhaa za kujifutia jasho,timu inapigwa hata tano ugenini biashara inaishia hapo hakuna kufuzu kwenda popote.

Hawa viongozi wasikie hivi hivi kuna uchafu mwingi kwenye game la bongo,angalau MO amekuja ndio anataka mafanikio ya kweli hasa ili ategeneze pesa yake irudi apate faida,ndio maana viongozi matapeli wengi hawamkubali maana ameziba mianya ya kuitumia simba kuchuma.
 
Back
Top Bottom