The Assassin
JF-Expert Member
- Oct 30, 2018
- 4,355
- 17,320
Wakati nchi ikiwa kwenye changamoto lukuki, mfumuko wa bei, hakuna maji, hakuna umeme, hakuna mikopo watoto wa vyuo hawajalipwa pesa cha ajabu viongozi wakuu na mawaziri waandamizi wako nje ya nchi kwa inayoitwa mialiko ya kitaifa.
Rais wa nchi yuko China, Makamu wa Rais yuko Ivory Coast, Waziri mkuu yuko Korea Kusini, mwanziri wengine wako Misri, wengine Kenya, wengine ulaya.
Kusafiri ni jambo jema lakini kusafiri safiri sio jambo jema.
Sielewi, viongozi wetu akili zao zinawaza kwamba tutatatua changamoto zetu kwa wao kusafiri safiri kweli? Kikwete alitumia miaka 2 ya uongozi wake kua nje ya nchi lakini bado tuko masikini.
Ingekua safari za nje zinaleta maendeleo kwa safari za Kikwete Tanzania ingekua kama California ama Texas kwa maendeleo ama hata kama Ujerumani maana kwa kikwete viongozi wote wakubwa Duniani walikuja Tanzania lakini mwisho wake tuliishia kuibiwa kwa mikataba ya hovyo.
Rais ni mfariji mkuu wa nchi lakini wakati huu ambao taifa linakabiliwa na changamoto kibao, viongozi wetu wao ni safari na kumtupia lawama mungu kwamba ndio ameyaleta haya sio wao.
Tanzania alieturoga alituweza.