Wakati mwingine nawaza ni bora Mungu asingempa mwanadamu "utashi" wa kujua mema na mabaya akafanana na wanyama wengine

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
46,993
144,329
Kitu kikibuwa kinachomtofautisha binadamu ambae kibailojia ni mnyama na wanyama wengine ni utashi aliopewa na mwenyezi Mungu wa kutambue mema na mabaya.

Mwenyezi Mungu hakuishia hapo bali akashusha amri kumi ambazo kila mwandamu anapaswa kuzifuata na kuzitii na mojawapo ikiwa ni "usiue."

Hata katika mamlaka na tawala za kibinadamu kuua ni kosa kubwa na ambalo lina adhabu kali kuliko makosa yote ambayo ni adhabu ya kifo(kwa hapa kwetu ni kunyongwa hadi kufa)

Cha kushanga,kuumiza na kusikitisha ni kuona mwanadamu huyu aliejaliwa utashi wa kujua jema na baya na mwenye kujizijua amri kumi za Mungu, yuko teyari kutetea au kufumbia macho mauji na mateso ya mwanadamu mwenzake mradi tu anaetekeleza unyama huo kuna chochote anachompa.

Kwakweli jambo hili mimi huwa linaniumiza sana na ninashindwa kabisa kuelewa hawa binadamu wana tofauti gani na wanyama wa mwituni wasio na utashi,wasiomjua Mungu na wala wasiozijua amri kumi za Mungu.

Inashangaza zaidi pale unapoona hata baadhi ya viongozi wenye elimu kubwa ya theology nao wakitumika kutetea uovu wa aina hii kisa tu wana mahusiano na wanaotekeleza unyama huu kwa binadamu wenzao.

Kwa mfano,mtu mwenye elimu kubwa na aliesoma theology anapotamka hadharani kuwa eti mtu kupigwa risasi ni jambo la kawaida tu.

Hivi mtu huyu angepigwa risasi mama yake angetamka maneno hayo?

Binafsi naomba niseme ni bora mara mia moja kama Mungu angetunyima utashi wa kujua mema na mabaya ili tuishi kama wanyama wa porini wanaotembea bila kusitiri mili yao na kujamiaana bila kujali huyu ni kaka,dada,mama au baba.

Mtu unasikia mwenzako kapigwa risasi au kauwawa alafu wewe unabeza,unakejeli na kushangilia.

Swali ni je,yangemkuta ndugu yako au mzazi wako ungekejeli?

Je,utashi huu aliotupa Mungu sisi wanadamu una maana yoyote kama tunakosa utu kiasi hiki?

Tunafuata nini Makanisani na Misikitini kama tumekosa ubinadamu kiasi hiki?

Kwanini Mungu asingetuacha tufanane na wanyama kwa asilimia 100 ili ijulikane moja tu?

Binadamu ni kiumbe mnafiki na mbinafsi pengine kuliko hata wanyama wa mwituni.
 
Kitu kikibuwa kinachomtofautisha binadamu ambae kibailojia ni mnyama na wanyama wengine ni utashi aliopewa na mwenyezi Mungu wa kutambue mema na mabaya.

Mwenyezi Mungu hakuishia hapo bali akashusha amri kumi ambazo kila mwandamu anapaswa kuzifuata na kuzitii na mojawapo ikiwa ni "usiue."

Hata katika mamlaka na tawala za kibinadamu kuua ni kosa kubwa na ambalo lina adhabu kali kuliko makosa yote ambayo ni adhabu ya kifo(kwa hapa kwetu ni kunyongwa hadi kufa)

Cha kushanga,kuumiza na kusikitisha ni kuona mwanadamu huyu aliejaliwa utashi wa kujua jema na baya na mwenye kujizijua amri kumi za Mungu, yuko teyari kutetea au kufumbia macho mauji na mateso ya mwanadamu mwenzake mradi tu anaetekeleza unyama huo kuna chochote anachompa.

Kwakweli jambo hili mimi huwa linaniumiza sana na ninashindwa kabisa kuelewa hawa binadamu wana tofauti gani na wanyama wa mwituni wasio na utashi,wasiomjua Mungu na wala wasiozijua amri kumi za Mungu.

Inashangaza zaidi pale unapoona hata baadhi ya viongozi wenye elimu kubwa ya theology nao wakitumika kutetea uovu wa aina hii kisa tu wana mahusiano na wanaotekeleza unyama huu kwa binadamu wenzao.

Binafsi naomba niseme ni bora mara mia moja kama Mungu angetunyima utashi wa kujua mema na mabaya ili tuishi kama wanyama wa porini wanaotembea bila kusitiri mili yao na kujamiaana bila kujali huyu ni kaka,dada,mama au baba.

Mtu unasikia mwenzako kapigwa risasi au kauwawa alafu wewe unabeza,unakejeli na kushangilia.

Swali ni je,yangemkuta ndugu yako au mzazi wako ungekejeli?

Je,utashi huu aliotupa Mungu sisi wanadamu una maana yoyote kama tunakosa utu kiasi hiki?

Tunafuata nini Makanisani na Misikitini kama tumekosa ubinadamu kiasi hiki?

Kwanini Mungu asingetuacha tufanane na wanyama kwa asilimia 100 ili ijulikane moja tu?

Binadamu ni kiumbe mnafiki na mbinafsi pengine kuliko hata wanyama wa mwituni.
Tanzania imegawanyika vipandevipande,mhutu anafurahia lakini mhutu hana uwezo wa kuongoza nchi kwa amani na upendo,iliyobakia watu wapumbavu kama wa upako wamebaki kujipendekeza tu
 
Kuna kundi Fulani humu JF wakati mwingine unatamani wangekuwa mbuzi ili sherehe kama hizo za pasaka au IDD tuwafanye kitoweo na kula supu na nyama choma.
Iko siku nitawataja sio Leo, ila wanajijua kuwa walistahili kuwa mbuzi bali ni kwa Neema tuu ni watu
 
Kuna watu roho ngumu sana aisee.

Uzuri mtu hawezi kuishi milele...

Wapo waliokuwa majeuri zaidi yao, lakini kwa sasa imebaki ni historia na mwisho wao haukuwa mwema.
 
Kuna kundi Fulani humu JF wakati mwingine unatamani wangekuwa mbuzi ili sherehe kama hizo za pasaka au IDD tuwafanye kitoweo na kula supu na nyama choma.
Iko siku nitawataja sio Leo, ila wanajijua kuwa walistahili kuwa mbuzi bali ni kwa Neema tuu ni watu
Hawa watu wamekuwa kama wanyama kisa tu kuna chochote wao wanakipata.
 
Back
Top Bottom