Wakati mwingine mwl alikuwa na maneno magumu sana!!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wakati mwingine mwl alikuwa na maneno magumu sana!!!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Shagihilu, May 12, 2010.

 1. Shagihilu

  Shagihilu Member

  #1
  May 12, 2010
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 61
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 15
  ......Pengine kwa nchi yetu hili lisingekuwa jambo la kutisha kama tungekuwa tumeanza kuona chama kizuri cha upinzani ambacho kinaweza kuiongoza nchi hii badala ya CCM.
  Hakijaonekana bado!
  Chama cha Mapinduzi, kwa sababu ya uzito wa historia yake,hadhi ya jina lake, mfumo wa wavu wake, mazoea ya watu, na ubovu wa vyama vya upinzani, kinaweza kuendelea kuchaguliwa na watanzania,pamoja na kansa ya uongozi wake. Au watu wanaweza wakachoka, wakasema, "potelea mbali:" wakachagua chama chochote, ilimradi tu watokane na kansa ya uongozi wa CCM. Hainifurahishi kuyasema haya, lakini uhai wa nchi yetu unataka yasemwe.
  Uongozi wetu na hatima ya Tanzania- Julius K. Nyerere, Uk 61
   
 2. J

  JOHN KITABI Member

  #2
  May 12, 2010
  Joined: Nov 10, 2007
  Messages: 26
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu yangu wakikusikia!
  Shauri yako. Kitabu hicho nakitafuta sana.
   
 3. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #3
  May 12, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,197
  Trophy Points: 280
  At this point, lawama ya uongozi mbovu Tanzania, ingawa haiondoki kabisa kutoka CCM, pia inaanza kuenea kwa Watanzania wote kwa ujumla hususan wanaoipigia kura CCM.

  Huwezi kusema CCM wana nguvu kiasi hicho. Kwa kweli by African standards for example, Tanzania ni moja ya nchi zinazoongoza katika freedom of speech, watu wanapaka live, magazeti yanaandika kuanzia ukweli mpaka uzushi, tumekuwa na vyama vingi kwa kadiri ya miaka 18 sasa, kwa hiyo si haki kulaumu CCM kwa kila kitu.

  Mengine ni makosa yetu wote kama Watanzania, especially wote tunaopigia kura CCM na tunaoshindwa kutoa na ku articulate a better alternative.

  Watu wa CCM wanaoperate a dinousaric steam engine ambayo haiwezi ku adapt na the times in a flip like that, lakini kila mtu - hata huyo baba wa taifa- ana operate under the illusion kwamba the best leadership itatoka CCM or it's fractions.

  It's been 18 years already, we should know better.
   
 4. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #4
  May 13, 2010
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  Flip flop
   
 5. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #5
  May 13, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,656
  Likes Received: 35,418
  Trophy Points: 280
  Bosi kumbe umeshawahi kuipigia kura CCM? Come on son....

  Mimi sijawahi kabisa kuwapigia kura hao jamaa ktk ngazi yoyote ile.
   
 6. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #6
  May 13, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,197
  Trophy Points: 280
  Son,

  As far as I am concerned usipopiga kura against CCM umepiga kura for CCM. That goes for the diaspora crowd that sadly doesn't vote either due to circumstances or nonchalant attitudes, as well as for the TZ massive.

  Mie sijawahi kuipigia kura CCM directly, lakini kwa kutokuwepo bongo na kuipinga CCM directly -pamoja na kupigia chama kingine- naona ni sawa na kuipigia kura CCM.

  Plurals nyingine ni za usanifu kama vile kwenye Quran unapoambiwa mungu aliumba mbingu na nchi, waliumba.
   
 7. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #7
  May 13, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,947
  Likes Received: 2,093
  Trophy Points: 280
  Tuahakikishie maneno yako.
   
 8. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #8
  May 13, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,947
  Likes Received: 2,093
  Trophy Points: 280
  Mwaka huu kwenye uchaguzi mkuu inabidi tutumie mtindo huu kama msemo huu usemavyo: kuruka kutoka kwenye kikaango chenye mafuta ya moto bila kujali kama utaangukia kwenye moto. Uamuzi huu unaweza kupeleka kwenye moto au pazuri jamani. Cha msingi turuke kutoka kwenye kuungua na mafuta haya yasiyo poa! Tukishindwa njia hii basi tuwe "revolutionary" maanake mabadiliko lazima. Kwa kifupi tuwe "radicals" i.e. radical voters aidha anarchical (maamuzi lazima mabadiliko bila kujali matokeo) or revolutionary (mabadiliko lazima na kujali matokeo - lakini mabadiliko lazima)!
   
 9. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #9
  May 13, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  Kwenye bold ndio mziziz wa shida hii yote! Hapo ndipo panapohitaji mwamko!
   
Loading...